Saturday, 11 June 2016

JIEPUSHE KURUDIANA NA MPENZI WAKO WA ZAMANI, NI HATARI SANA KWAKO


Mapenzi/Mahusiano ni kama chuo/darasa, unapata mengi ya kujifunza toka
kwa mwenzako uliyenaye kwenye huo uhusiano. Mnaweza achana kwa makubaliano mazuri au kwa vurugu na dharau pamoja na kejeli kibao.

Hutokea mara nyingi mmoja wenu akarudi kama rafiki mwema aliyebadilika na kuhitaji nafasi ya pili ya mahusiano/mapenzi tafadhali usikurupuke kuingia katika mtego huo.

Unaweza kuhatarisha afya yako bila kujua.Baadhi ya wanaorejea na kuomba mrudiane wanakuwa na agenda za siri kama hizi.

1) Kule alikoenda aliyempata kashindwa kufikia vigezo vya ubora ulivyonavyo wewe ndo maana karudi mazingira yamemrudisha kwako vinginevyo asingerudi, sio upendo.

2) Anaweza kuwa na kinyongo moyoni nawewe kwa namna uliyomuacha sasa anataka kulipa kisasi kwa gharama yoyote,sio lazima atoe uhai wako katika hili.

3) Maisha yamemshinda yamekuwa ni kinyume na matarajio yake, angefanikiwa asingerudi, akirudi huyu lazima akufilisi akirudi kwako.

4) Wako wanaorudi kujaribu hana nia ya dhati,lolote litakalokuwa liwe,mtu wa aina hii, ataishia kukupotezea mda na raslimali zako.

5) Wako wanaorudi huku bado wanamahusiano waliyoyaanzisha baada ya kuachana nawewe awali utashangaa mwanamke/mwanaume ana stress za mapenzi mda mwingi chanzo kumbe ni kule alikotoka bado yuko naye.

Ni hayo kwa leo, bado maamuzi ni yako kwani maswala ya mapenzi ni vigumu kumwamulia mtu, unampa ushauri kutokana na uzoefu ambao nao hauna kanuni, unatofautiana baina ya mtu na mtu.

Wakati mwema
Jerome Mmassy-Arusha,Tanzania

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI UTKAVYOKUONDOA KATIKA DIMBWI LA UMASKINI



MAHITAJI
Kuku(tetea) 10 na Jogoo 01
Banda bora
Vyombo vya chakula na maji
Chakula bora
Madawa na chanjo kwajili ya magonjwa
Chanzo cha nishati joto na mwanga
Elimu na ujuzi wa malezi bora
Chombo au chumba cha kutunzia vifaranga
Mayai ya kuku wa kisasa/mayai mabovu(ambayo hayakuanguliwa)
Madaftari au kitabu cha kutunzia kumbukumbu

KUKU 10

Wakati wa kuanza mradi wako hakikisha una kuku 10 (matetea) wenye umri sawa na hawajawai kutaga hata mara moja. Chagua kuku wenye rangi nzuri kutoka katika familia bora kutegemea malengo ya mradi wako. Mfano kama lengo lako ni kuzalisha kuku wa kienyeji kwajili ya nyama basi chagua mbegu ambayo inakuwa haraka na yenye uzito mkubwa. Au ikiwa lengo ni mayai basi ni vema kuchagua aina ya kuku yenye kukua haraka na kutaga mayai mengi.

Ili kupunguza gharama za manunuzi ya kuku na hivyo kuongeza faida kwa mfugaji ni vema kununua kuku wadogo ambao wametoka tu kuachishwa kulelewa na mama zao. Kuku hawa utawapata kwa bei ya chini, tena watafaa sana maana watakua na umri mmoja pia.

JOGOO 01

Jogoo mmoja tu anatosha kuwahudumia kuku matetea yote kumi. Hakikisha katika uchaguzi wa jogoo bora lililochangamka, rangi mzuri, upanga umesimama, macho angavu, uzito wa kutosha, rangi nzuri na uwezo mkubwa wa kuzalisha. Ni vema mfugaji akaelewa kwamba kuku wote watakaozalishwa watategemea ubora wa jogoo wake. Uwezo wa kutaga kwa kuku na upatikanaji wa mayai pia hutegemea kwa karibu ubora wa jogoo aliyechaguliwa.

BANDA BORA

Miongoni mwa mambo mhimu naya kwanza kuzingatiwa katika ufugaji wa kuku wa kienyeji kama mradi ni maandalizi ya banda bora. Kuku huhitaji banda bora ili wasiathirike na madhara mbalimbali. Mfugaji anatakiwa kuandaa banda lenye ukubwa wa mita 10 kwa mita 04. Yani urefu uwe mita 10 na upana upana wa mita 04. Kisha kata vyumba vya mita 2 urefu na upana mita 4 kutoka katika banda lako hivyo utakuwa na jumla ya vyumba vitano vyenye ukubwa unaolingana. Ujenzi uzingatie malighafi na vifaa vinavyopatikana kwa urahisi katika mazingira husika. Mfano katika maeneo ambayo fito zinapatikana kwa urahisi banda linaweza kuandaliwa kwa miti na kukandikwa kwa udongo. Au sehemu ambayo mabanzi hupatikana kwa urahisi basi banda laweza kujengwa kwa kutumia mabanzi. Vifaa vya kujengea banda vizingatie pia gharama na upatikanaji wake katika eneo husika. Baadhi ya vifaa hivyo ni kama ifuatavyo:-
Sakafu: Saruji, udongo, mbao, mianzi au fito
Kuta: Fito, mabanzi, mbao, nguzo mianzi,udongo, matofali, mawe, mabati na wavu
Paa: Nyasi, makuti, majani ya migomba, mabati na vigae.
Wigo: Matofali, mbao, fito nguzo, mabanzi, mianzi, matete, wavu na mabati

Banda bora la kuku linatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-
Imara, lenye uwezo wa kuwahifadhi kiafya na pia dhidi ya hali ya hewa hatarishi kwa mfano jua kali, upepo, baridi na mvua pamoja na wanyama hatari.
Lenye mwanga, hewa na nafasi ya kutosha inayoruhusu usafi kufanyika kwa urahisi.
Lijengwe sehemu yenye mwinuko isiyotuama maji, isiyo na upepo mkali na iwe mbali kidogo na nyumba ya kuishi watu.
Liwe na vichanja kwa ajili ya kuku kupumzika na kulala.
Liwe na sehemu ya kuwekea chakula, maji, kutagia, kuatamia na sehemu ya kulelea vifaranga.
Liwe na nafasi ya kutosha kulingana na idadi ya kuku na kuweka vyombo vya chakula na maji.
Kwenye mazingira ya joto banda liwe la ukuta mfupi na sehemu kubwa wazi yenye wavu hadi kufikia kwenye paa. Kwenye mazingira ya baridi banda liwe na ukuta mrefu unaokaribia paa na sehemu ndogo tu iwe wazi yenye wavu ili kupitisha hewa na mwanga.

JINSI YA KUFANYA

Wakuze kuku wako hadi watakapofikia muda wa kutaga. Wakianza kutetea ni kiashiria kwamba wakati wa kutaga umekaribia hivyo andaa viota kwajili ya kutagia.

Viota vinapaswa viwe na ukubwa stahiki ili kumwezesha kuku kuyafunika mayai yote vizuri wakati wa kuetamia, viota viwe vinavyozuia mayai kutawanyika, viwe mahali pakavu na safi.

Hakikisha kuku wote wanataga katika viota tofauti. Kuku anapotaga mayai matatu unapashwa kuchukua mayai mawili na kumwachia yai moja ili kumfanya aendelee kutaga zaidi. Kuku akifikia yai la kumi na mbili anza kumwachia mayai matatu ili kumwandaa kwa kazi ya kuetamia. Kwa kufanya hivi, kuku atataga mayai 15 au zaidi na ikiwa atataga mayai 15 au chini ya hapo nakushauri utafute mayai mengine ujazilizie ili kufikisha mayai 20 kwa kila kuku. Zingatia kwamba mayai unayoyatoa kwa kila kuku, yanatunzwa sehemu salama, mahali pakavu, pasafi na penye joto la wastani.

Kuku wote wanapaswa kuanza kuetamia kwa siku moja. Ili kufanikisha hili inapasa uwe karibu na kuku wako. Kuku mmoja akianza kuetamia mwekee mayai ya kuku wa kisasa au mayai mabovu ya kuku wa kienyeji. Utafanya hivi hadi kuku wako wote watakapoanza kuetamia mayai. Kuweka mayai mabovu au mayai ya kuku yaliyotumika humfanya kuku aendelee kuetamia akijua ni mayai yake.

Baada ya kuona kwamba kuku wako wote wapo tayari kwa kuetamia mayai, waandalie banda maalumu kwajili ya kuetamia yani chumba kimoja katika lile banda letu. Ninashauri kwamba chumba kwajili ya kuetamia kiwe chumba cha kwanza au cha mwisho katika mfuatano wa vyumba vya banda lako. Andaa viota bora vya kuetamia, weka mayai 20 kwa kila kiota, ikiwa hayajatimia unaweza kununua kwa wafugaji wengine ili kuifikia idadi yako.

Waamishe kuku kutoka wanapotagia na kuwaweka katika chumba ulichokiandaa kwajili ya kuetamia. Ili ufanikiwe katika zoezi hili inafaa lifanyike wakati wa usiku na unafanya katika giza. Mweke kuku katika kila kiota na asubuhi wajikute kila mmoja katika kiota chake. Wahudumie kwa chakula na maji ya kutosha. Wakati wa usiku waongezee joto la ziada kwa kuweka jiko au ndoo ya chuma yenye chengachenga za mkaa au kama una umeme weka taa za joto.

Baada ya siku 21-25 kuku wako wataanza kuangua vifaranga. Huu ndio wakati unaotakiwa kuwa karibu sana na kuku wako kuliko wakati wote. Watenge vifaranga mara tu baada ya kuanguliwa; waweke katika chumba chao maalumu mbali na kuku. Kama chumba cha kuetamia kilikuwa cha kwanza basi vifaranga wawe chumba cha mwisho n.k

Ukishawatenga vifaranga mbali na matetea wako, wawekee tena mayai mengine 20 kila tetea, mayai ambayo utayanunua kwa wafigaji wenzako. Hakikisha kuku waliotaga hayo mayai ni wazuri, hawana magonjwa na wanauzito/ukubwa unaofaa. Mayai yote yakaguliwe vizuri ili kujua kwamba yameharibika, yana nyufa au mabovu. Kabla ya kuweka mayai mengine hakikisha chumba chako ni kisafi na viota vimesafishwa, havina wadudu na uchafu wowote. Kuku wako bila kujijua wataanza kuetamia upya mayai uliowawekea.

Ukiwawekea mayai rudia mzunguko kama nilivyokwambia awali. Baada ya siku 21 hadi 25 tena utapata vifaranga wako wengine tena. Fuata kila hatua kama nilivyokwambia hapo awali. Lakini kwa awamu hii nashauri waache matetea wako wapumzike wala usiwapatie mayai mengine tena.

JINSI YA KULEA VIFARANGA

Ikikaribia siku ya 20 tangu ulipowawekea matetea wako mayai katika chumba cha kuetamia, andaa chumba kwa ajili ya kulea vifaranga. Safisha kwa kuondoa uchafu na wadudu wote.

Washa taa ya joto au weka chombo cha kutoa joto katika chumba cha vifaranga nusu saa kabla hujaanza kuingiza vifaranga wako. Weka pia chakula na maji ya kutosha katika vyombo vyenye umbile na ukubwa utakaowawezesha vifaranga kuvitumia. Tandaza magazeti, maboksi, makaratasi n.k katika sakafu ya chumba hicho. Hakikisha vifaranga wako hawajikusanyi sehemu moja maana wakifanya hivyo wengi wao watakufa ili ufanikiwe katika jambo hili, banda lako liwe la mduara katika kona zake.

Weka joto la kutosha. Joto la kutosha ni lile linalowafanya vifaranga watawanyike chini ya chanzo cha joto wakati kama joto limezidi vifaranya kukimbia mbali na chanzo cha joto na ikiwa joto halitoshi vifaranga hujukusanya chini ya chanzo cha joto.

Baada ya siku 3 utawapatia chanjo ya Gumboro na siku 7 wapatie chanjo ya New Castle, utarudia tena kuwapa chanjo hii baada ya mwezi mmoja kisha utafanya hivi kila baada ya miezi mitatu mitatu.

MAPATO YA MRADI WAKO

Katika uzazi wa kwanza utapata vifaranga 150 kwa wastani wa vifaranga 15 kwa kila kuku. Tuseme haujazingatia kanuni za ufugaji za makala hii ukapata vifaranga 100 yani wastani wa vifaranga 10 kwa kila kuku. Kisha baadaye wakakua wakafa kuku 50 yani watano kwa kila kuku utakuwa na jumla ya kuku 50.

Baada ya wiki 3 utapata tena kuku tufanye kwa mahesabu kama hayo hapo juu kwa hasara utakuwa na kuku wengine 50, na kufanya jumla ya kuku 100. Ikiwa kuku wako baada ya uzao wa pili uliwapumzisha kwa miezi miwili basi mwezi wa 3 utapata tena kuku vifaranga 100 na wiki 3 baadaye utapata wengine 100. Kwa mahesabu kama hayo awali wakikuwa utakuwa na kuku wengine 100 ambao watakuwa.

Baada ya miezi 6 utakuwa na kuku wakubwa wa uzao wa kwanza 50, uzao wa pili kuku 50 na utakuwa na kuku wenye umri wa miezi mitatu 50 wa uzao wa 3 na kuku wengine 50 wa uzao wa 4.

Katika kuku 100 wa uzao wa kwanza na pili, tufanye kuku 50 wawe matetea ukijumlisha na kuku 10 ulioanza nao mradi utakuwa na matetea 60. Ikiwa kila tetea atatotoa vifaranga 10 na vikakua vitano tu, mwishoni utakuwa na kuku 300 na baada ya miezi mitatu kuku wengine 900 toka katika kutoka kwa uzao wa kwanza, wapili na watatu. Hivyo mwaka wa pili utafunga na kuku si chini ya 1,200/= wanaotaga mayai.

Ukiuza majogoo yote 1,200/= kwa bei ya 8,000/= ili upate pesa ya kujenga miundombinu bora maana sasa utakuwa na kuku wengi wanaoendelea kuzaliana kwa kasi utapata pesa kiasi cha TZS 7,200,000/=. Sasa ongeza kuku wako wa kutaga hadi wafikie kuku 4,000 maana sasa utakuwa na pesa za kutosha kuendesha mradi wako.

Sasa ukiwa na kuku 4000 wa kienyeji wa kutaga mayai, ikiwa kuku 3000 tu watataga ukauza yai moja kwa bei ya haraka haraka ya TZS 250 tu, utapata TZS 750,000/= kwa siku ambayo sawa na TZS 22,500,000/= kwa mwezi na TZS 270,000,000/= kwa mwaka sawa sawa na 128,572 USD. Kumbuka mwamba makadilio haya niya chini sana. Ukifata kanuni zote kwa makini na maombi huku ukimtanguliza Mungu utafikia hata TZS 500,000,000/= kwa mwaka.

Kumbuka unapofanikiwa kupata mapato ya kila aina, umtolee Mungu zaka(x10%) ya mapato yako, pia ukatoe sadaka ambayo ni kubwa kuliko zaka na uwasaidie masikini na wahitaji.

Tunza kumbukumbu zako zote za fedha katika daftari maalumu kuhusu mapato na matumizi ya mradi wako. Pia hali ya kuku wako kuhusu tarehe za chanjo ya mwisho, siku walipoanza kuetamia, magonjwa yanayowasumbua mara kwa mara n.k.

Karibu tuendelee kujifunza
Jerome Mmassy-Arusha,Tanzania

Friday, 10 June 2016

USHAURI MURUA KWA WADADA NA WAKAKA CHINI YA MIAKA 30


Utu uzima dawa! Mnakopita sasa sisi tulishapita salama, lakini kuna uhitaji wa kukumbushana machache, kupeana mbinu na kutiana moyo pia (hapa kwa sehemu hata wadogo zangu wa kike watahusika). Naongelea mabadiliko ya makuzi kihomoni, kimtazamo, kimahusiano na kifikra pia.

Kwanza lazima niwapongeze kwa uamuzi wenu wa hiari wa kuachana au kutoka kwenye mitandao mingine isiyo na faida wala tija na kuja kujiunga JF(JamiiForums) penye kisima cha maarifa, ujuzi na hata ushauri.

Niwapongeze pia wengi wenu kwa kuwa wawazi kwa yale mnayopitia, wengi wenu hamfahamu kuwa ni sehemu ya makuzi hivyo kujaa hofu na woga mwingi hasa kwenye maeneo haya;

1. Haiba - hapa kila mmoja anajitahidi awezavyo ili aonekane wa kisasa kwa mavazi lugha na hata mikogo mingineyo, kukosa baadhi ya hivyo vitu husababisha maumivu makubwa sana bila kutambua kuwa wakati wako wa kupata bado

2. Ukakamavu/confidence ya kuongea na hadhira au jinsia tofauti, hapa ni kimbembe, wengi hujichukia na kujistukia na hivyo kusababisha kujitenga na jamii muda mwingi kwa kudhani wengine wanajiona bora au ni mahiri kuliko wao! Hiki ni kipindi tu na kitapita lakini siri ya kuongea na hadhira ni kutowaangalia watu machoni bali kuwaangalia juu ya macho yao kwenye paji la uso.

3. Mahusiano kipengele hiki ni muhimu sana na hapa namaanisha kwenye ishu nzima ya kufanya mapenzi. Asikudanganye mtu, mapenzi utayajua baada ya kuvuka miaka 30, hapo utakuwa umewazoea na kuwafahamu wanawake na utakuwa huna hofu tena. wengi sana hapa wanalalamika kukosa nguvu au kumaliza haraka hii yote inaletwa na hofu na mara nyingi kudate mpenzi ambaye tayari keshakutana na wataalam, usitegemee kamwe katika miaka yako 26 umridhishe mwanamke wa 18-23 atakuwa anakuibia tuu.



Mabinti wengi below 25 wapenzi wao ni 35+years. Hapo huwezi weka ligi.
Kinachowatisha wengi ni story za wanawake kufikishwa kileleni au kupiga show 30 nonstop wakati wewe dak5 nyingi. Usihofu, muda wako bado, wewe bado mchanga hujakomaa.

Lakini vile vile kuna wakati maungo yako huhitaji mapumziko. Hii hutokea yenyewe automatically, ndio maana kuna wakati unakuwa na ashiki sana na kuna wakati unakuwa kama hanithi. Usitishike, jitahidi mazoezi, epuka vyakula vya mafuta na makopo, jizuie kadiri uwezavyo kupiga punyeto labda mpaka uzidiwe sana.



4. Uko kwenye kipindi cha kuingia ukubwani, kwahiyo akili ya kiutu uzima inafunguka, hii hali huja na side effects kama za mama mjamzito. Hasira za ghafla, kukata tamaa, kulia au kutamani kulia, kuzira, kujitenga, kuwa mtu wa mawazo muda mwingi ni vitu visivyoepukika.

Hapa ndipo unapojishape kuwa wewe wa kesho, kwahiyo jitahidi sana yanapokutokea haya usiyaendekeze, vijana wengi huwin na kushindwa hapa. Ukiyapuuza na kusonga mbele mafanikio yako yataanzia hapo, utayachukulia kuwa ndio sehemu ya maisha yako, kushindwa kwako kutaanzia hapo.

Kama bado uko below 30 usiangalie mwili ulionao bali jipange kwa kuwa hii ndio hatua muhimu ya kuwa wewe wa kesho. Mustakabali wako umeubeba mwenyewe.

Mshana Jr.




TUMIA NJIA HII KUNASA MCHEPUKO WAKO


Mmmh! Najua wazee wakuchepuka wamevutiwa na heading sana.

Iko hivi kama una mke au mume na humuamini unahisi kabisa ana mtu nje fanya njia hii kupata uhakika ila angalizo kama huna moyo mpana acha au kama unampenda sana acha pia,kama anatumia simu na unahisi kwenye simu kuna namba zakutia mashaka fanya haya.

Nenda kwenye ile namba ifute tazama jina lililoandikwa kwenye hiyo namba ingiza namba zako nyingine ambazo hata yeye hazijui andika jina hilo hilo, kama mtumiaji anatumia whatsapp ndio rahisi zaidi, angalia picha gani ameweka mshukiwa wako na wewe weka hiyo hiyo, kwakuwa umeshafuta ile namba kwenye simu yake hataweza kushtukia.Sasa hapo we kula kona anza kuchat utajua kila kitu kuhusu huyo unaemtilia mashaka.

Naomba niwaambie tu kesi yoyote huko mimi simo,msisahau kuleta mrejesho pia hapa,

Mwisho kabisa michepuko haifai tulizaneni.





Kwa hisani ya jirani yangu hapa.......

SIFA KUMI ZA MJASIRIAMALI


DHANA ya ujasiriamali Tanzania imeshika kasi hasa katika karne hii ya 21 licha ya kuwapo duniani kwa muda mrefu.


Kimsingi, ujasiriamali Tanzania umeshika kasi miaka ya 2000, hasa kutokana na juhudi za Serikali kuboresha sera na sheria mbalimbali za uchumi kwa mfano, sera ya maendeleo ya biashara ndogo ndogo.


Kutokana na hili, tumeshuhudia watu wengi wakijitoa kimasomaso kuanzisha biashara au kufanya shughuli mbalimbali za ujasiriamali. Je, hao wote ni wajasiriamali halisi?


Kupima kama kweli wewe ni mjasiriamali halisi karibu kupitia mada hii inayotumia stadi ya David McClelland ambaye ni mwanasaikolojia kutoka chuo kikuu cha Havard nchini Marekani aliyegundua tabia za kisaokolojia zinazojengeka ndani ya mjasiriamali ambaye amefanikiwa kibiashara.


Stadi hiyo inaonyesha tabia kuu 10 kiujasiriamali na zilizovunjwa katika tabia ndogo ndogo 30 zikiwa kama viashiria vya mjasiriamali halisi kama inavyoelezwa hapa chini.


1.Kutafuta fursa na uwezo wa kujituma


. Katika hatua hii, mjasiriamali anakuwa na tabia ya kufanya mambo kabla kulazimishwa. Mjasiriamali ambaye anaona fursa kwa haraka na anafanya uamuzi kwa wakati kuboresha biashara yake kwa kuongeza ubora wa bidhaa au huduma kwa wateja wake.


2. Jitihada.


Mjasiriamali anachukua hatua bila kujali vikwazo wala matatizo, anatumia mbinu mbadala kuondokana na matatizo yanaomkabili. Pia anajiona anawajibika kwa mafanikio anapotimiza lengo alilokusudia. Kimsingi mjasiriamali hachoki na wala hakati tamaa, muda wote akishindwa hili hufanya hili au kubadilisha mbinu ili afikie malengo.


3. Mkweli na kutimiza ahadi


. Mjasiriamali anajitoa kwa hali na mali ili kumaliza kazi aliyojipangia, inapowezekana huuingilia hata majukumu ya wengine ili kumaliza kazi haraka na kwa wakati. Pia anahakikisha wateja wake wanaridhika. Pia anapokea oda na kutoa ahadi anazoweza kuzitimiza.


4. Ubora na ufanisi.


Mjasiriamali anatafuta mbinu mbalimbali kufanya mambo vizuri, haraka na kwa gharama nafuu. Pia anaweka utaratibu na kuzifuata ili kuhakikisha kazi inamalizika kwa muda na katika kiwango stahiki.


5. Anakuwa makini na vihatarishi.


Muda wote anachukua tahadhari na kutafuta njia mbadala zisizo na hatari kubwa, anachukua hatua kupunguza hatari na kudhibiti kutokea kwa hatari yoyote ya kibiashara.


6. Malengo


. Mjasiriamali, anajipangia mikakati na shabaha ya kupunguza matatizo kwa kutumia fursa. Pia anaweka malengo ya muda mfupi, wa kati na mrefu. Kimsingi mjasiriamali halisi hapati faida kwa bahati bali inapangwa.


7. Anatafuta taarifa.


Mjasiriamali anatafuta taarifa nyingi kutoka vyanzo mbalimbali kutoka kwa wateja, wagavi au washindani. Anafanya utafiti wa jinsi ya kutoa bidhaa au huduma bora, na vilevile anaomba ushauri kutoka kwa watalaamu katika mambo ya biashara au kitalaamu.


8. Mipango na ufuatiliaji.


Kupunguza majukumu makubwa na kuwa madogo yenye kutekelezwa ndani ya muda mahususi. Mjasirianali anapaswa kupitia mipango yake mara mara kutokana na tathimini katika ufanisi au kubadilisha mazingira. Vilevile anatunza rekodi na taarifa zake za fedha na huzitumia kufanya uamuzi.


9. Ushawishi na kujenga mtandao.


Anatumia mbinu mbalimbali kuwashawishi wengine (wateja). Anatumia watu mashuhuri au wenye nafasi fulani kama wakala wake kufanikisha lengo au shabaha, na pia anachukua hatua madhubuti kutafuta na kudumisha mtandao wa kibiashara.


10. Kujiamini na kujitegemea. 


Anapenda kujitawala mwenyewe na kutenda kulingana na msimamo wake. Anajiweka katika nafasi ya kuona kushindwa au kufanikiwa ni kwa sababu yake mwenyewe.


Pia anaonyesha dhahili ustadi na uwezo wake kufanya mambo magumu yenye changamoto.
Hizi nitabia kuu 10 walizonazo wajasiriamali. Wanafanikiwa katika biashara. Jipime tabia zako zikoje unapofanya biashara. Mjasiriamali anaweza kujifunza tabia hizi kama hana.










Endelea kutembelea mtandao huu tuendeleze kufundishana


Imeandikwa na Mmassy Jerome- Arusha,Tanzania





Wanandoa waliodumu muda mrefu kuanza kupewa Tuzo Tanzania




Imezoeleka kwamba ndoa za kikatoliki zikifungwa zimefungwa lakini pamoja na sharti hilo idadi ya ndoa zinazovunjika inaendelea kuongezeka ambapo sasa kanisa katoliki limekuja na hii ya kuanzisha tuzo maalumu kwa Wanandoa wakongwe zaidi kwa mwaka huu katika kanisa hilo.





BBC SWAHILI wameripoti kwamba Kanisa Katoliki jimbo kuu la Dar es salaam limeandaa kliniki ya ndoa ili kuweza kuwapa fursa Wanandoa kuimarisha ndoa zao kiimani, Padre Novatus Mbaula ambaye ni mkurugenzi wa ndoa na familia anaeleza lengo la kliniki hii ni kuwapa nafasi wanandoa kupata neno la Mungu na kuweza kuongea juu changamoto zao mbalimbali kuongea kuhusu maisha yao ya ndoa.

Ni nafasi ambayo wanandoa ambao wana uzoefu mkubwa katika ndoa wanaweza kuwafaidisha wanandoa wachanga na miongoni mwa watu waliohudhuria kliniki hii ni wanandoa wenye ndoa yenye miaka 61, Brigedia Jenerali mstaafu Francis Mbena mwenye umri wa miaka 86 alifunga ndoa akiwa na miaka 25 mwaka 1965 June,anasema wao zamani walikua wanafuata mtu na familia gani na ina vigezo gani.

Walikua wanaangalia tabia kama msichana hana tabia nzuri huoi huko, kama familia ina watu walevi bali unatafuta familia yenye watoto wenye tabia nzuri ili na wewe uweze kupata watoto wenye tabia nzuri.

HATUA SABA MUHIMU ILI KUWA MJASIRIAMALI MWENYE MAFANIKIO


Ujasiriamali ni neno la kiswahili linalotokana na maneno mawili yafuatayo
1.    Ujasiri 2.
2.    Wa mali
Hii ina maana ya mtu mwenye ujasiri wa kuwekeza mali alizonazo ili apate faida
 Hatua 7 muhimu ili kuwa mjasiriamali kamili (J7)
1. Jitoe bila woga na kuwekeza ulicho nacho
2. Jipange (mpango mkakati)
3. Jipime Ili kujua uwezo na madhaifu yako
 4. Jiwezeshe kwa kupata mafunzo
 5. Jihadhari ili usitumbukie kwenye hatari
 6. Jitadhmini, jikosoe kwa kujitathmini
 7. Jipange upya kwa kufanya maboresho


1. Jitoe Bila Woga na Kuwekeza Ulicho Nacho.
Maamuzi magumu yanatakiwa unapotaka kuwa mjasiriamali. mke, mume, wazazi, wajomba ndugu, marafiki, wakuu wa ukoo wako na hata mazingira yako yanaweza kukataa au kuwa pingamizi kubwa ili usifanye shughuli za kijasiriamali. Kwa mazingira haya ni rahisi kukata tamaa na kama hukuamua kutoka moyoni mwako fikra zako za kuwa mjasiriamali zitaishia hapo na hutakaa ufanye biashara. Kuamua na kujitoa ni muhimu sana ili uweze kuendelea an maono yako yatakayokukomboa kiuchumi Ili uweze kujenga himaya yako (ufalme wako) (your kingdom) wa utajiri unahitaji kufanya maamuzi yako peke yako wala sio ya hao waliotajwa hapo juu japo ushauri kutoka kwao ni ruksa na utakusaidia kufanya maamuzi bora zaidi. Kujitoa unakusaidia wewe kuhesabu gharama ya hatari zitakazokuwepo mbele yako kwenye ujasiriamali wako. Utahitajika saa nyingine kuwekeza mali ya kipekee uliyonayo. kama vile nyumba, gari, kiinua mgongo nk. Kama wewe ni mwoga hutadhubutu kuwekeza kajumba kako ka­pekee eti kwa sababu ya ujasiriamali. Kama kweli ukiamua na kujitoa maisha yako yatabadilika sana kuanzia siku ile ya maamuzi magumu. Safari ya ujasiriamali huwa na tabia ya kwenda juu au chini kama meli inayoyokabiliana na tufani baharini. Unashauriwa kutizama lengo na sio tufani ya bahari. Kama umeamua kutoka moyoni kuwekeza utafika tu kwenye lengo kuu. Epuka kukopa ili uanzishe biashara, ni hatari sana. Kusanya vyazo vyako vya mitaji (mali binafsi )

 2.Jipange (Mpango Mkakati)
 Weka maono ya biashara yako, unataka kufikia ngazi ipi kimafanikio. Je unataka kuwa na hoteli kubwa ya kitalii au kiwanda kikubwa cha kuuza nguo Tanzania au Afrika nzima? Weka na kazi muhimu utakazozifanya ili kufikia maono husika. Unaweza weka malengo mahsusi kila baada ya miaka mitatu au mitano. Inashauriwa malengo hayo mahsusi yawe kati ya 3 na 5. Jiwekee malengo ya muda mrefu na muda mfupi. Malengo yagawanywe mpaka kwenye kazi za kila siku. Jiwekee maadili na tunu za mafanikio. Bila hizi tunu na maadili huwezi kuyafikia malengo yako. Jiwekee ratiba mbalimbali za kiutekelezaji bila kusahau kuweka kwenye ratiba shughuli muhimu.
3. Jipime Ili Kujua Uwezo na Madhaifu yako Kiingereza wanaita SWOT Analysis
 Jipime juu ya mambo makuu manne yaliyogawanyika kwenye makundi mawili
 1. Mazingira ya biashara ya ndani
 2. Mazingira ya biashara ya nje
 AU
 1. Mazingira wezeshi
2. Mazingira hatarishi
Haya makundi mawili nayo yamegawanyika katika Mazingira ya ndani ni
 1. Uwezo wako kibiashara
 2. Udhaifu wako kibiashara
 Mazingira ya nje ni
 1. Fursa zilizopo ili kunufaisha biashara yako
2. Hatari zilizopo ili kuua biashara yako
 Mazingira wezeshi ni kama ifuatavyo
1. Fursa zilizopo ili kunufaisha biashara yako
 2. Uwezo wako kibiashara Mazingira hatarishi ni kama ifuatavyo
 1. Hatari zilizopo ili kuua biashara yako
2. Udhaifu wako kibiashara unaoweza kuzorotesha maendeleo ya biashara yako
4. Jiwezeshe kwa Kupata Mafunzo
 Jiwezeshe ni hatua inayojibu matokeo ya hatua ya kujipima ambayo imekuwezesha kugundua madhaifu yako na kuyapatia ufumbuzi kwa kujiwezesha ambazo mara nyingi ni mafunzo. Udhaifu ni yale mambo ya kimaarifa usiyoyajua kiutendaji ili biashara yako isonge mbele. Inaweza kuwa ni ujuzi wa kufuga samaki kama unataka kuanzisha mradi wa kufuga samaki nk.
5. Jihadhari ili Usitumbukie Kwenye Hatari
 Katika hii hatua hakikisha kila uamuzi au tendo unalofanya halitakuingiza kwenye hatari kubwa usiyoweza kumudu bali inakuweka kwenye changamoto ambazo unazimudu. Kingereza wanaita (Moderate Risk). Usijaribu kufanya biashara zenye hatari kubwa na ya uhakika. Usijaribu kuingia ubia/ushirika na watu ambao unawajua ni hatyari kwa biashara zako. Usijaribu kuingiza teknolojia kwenye biashara yako ambayo una uhakika kuwa sio rafiki.
6. Jitadhmini,
 Jikosoe kwa Kujitathmini. Fanya tathmini za mara kwa mara ili kujua kama unakwenda sawasawa na makusudio ya mwanzo. Fanya tadhmini ndogo kila baada ya nusu mwaka, na tadhmini kubwa kila baada ya miaka mitatu.
 7. Jipange Upya kwa Kufanya Maboresho
 Matokeo ya tadhmini yatumike kama msingi wa kujipanga upya na kufanya maboresho makubwa yatakayoitoa biashara yako kutoka kwenye ngazi moja ya mafanikio kwenda ngazi ya juu zaidi ya mafanikio. Tumia matokeo ya tadhmini zote mbili kujikosoa na kufanya maboresho yenye lengo la kujibu kasoro zilizoonekana kwenye ripoti ya tadhmini.

Karibu tuendelee kujifunza zaidi

Mmassy Jerome-Arusha,Tanzania


KANUNI ZA UJASIRIAMALI ZINAZOMWEZESHA AFANIKIWE


Kanuni za ujasiriamali zinaweza kusomwa au kufundishwa na mtu akaelewa na kuzifuata,lakini  tabia  zingine  hazifundishiki hizi ni zile tabia ambazo mtu anazaliwa nazo. Kila binadamu anauwezo tofauti katika kufikiri,kufanya maamuzi,kufanya kazi kwa bidii,tofauti hizi ndizo ambazo haziwezi kufundishika. Jambo la kutia moyo ni kwamba tabia ambazo zinafundishika ni muhimu sana kwa mjasiriamali au mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika biashara. Zifuatazo ni kanun muhimu  za ujasiriamali.
1.       Kuthubutu
hii ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali,hapa tunazungumzia uwezo na utayari wa kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu kuingia katika biashara,mradi n.k,watu wanaogopa hasara,hawajui jinsi ya kuendesha mradi weyewe. Mtu ili aitwe mjasiliamali ni lazima awe na uwezo wa kuhtubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye utafiti wa kutosha il baadaye limletee tija. Waswahili mwanasema” UWOGA NI UMASIKUNI”.
2.       Nidhamu
Hii pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali,mjasiriamali lazima awe na na nidhamu katika biashara yake,awe na nidhamu katika matumizi yake ya pesa na ni lazima awe na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii.nidhamu ni chanzo ch mafanikio. Mfano mfanyabiashara wa duka ni lazima awe na nidhamu kwa wateja wake ili wasimkimbie.
3.       Umakini na uelevu
Wale waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa katika kazi waliyokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila jambo,anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe muelevu wa kutambua mabadiliko yanayojitokeza katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
4.       Kuwa na uwezo wa kuongoza
Mjasiriamalia lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai uongozi  ni karama ombayo mtu anazaliwa nayo au anapewa na Mungu,ni kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha kuongoza,lakini mtu anaweza kujifunza na akawa kiongozi mzuri. Katika ujasiriamali uongozi ni jambo muhimu sana,mjasiliamli lazima aweze kuongoza biashara yake au mradi wake vizuri. Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kusimamia wafanyakazi na kutumia mbinu  za uongozi ili apate matunda kwa kile ambacho anafanya.
5.       Kupenda kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu kikubwa  hapa ni lazima mjasiriamli awe anaipenda kwa dhati shughuli anayofanya hii itamsaidia kufanya kazi kwa moyo.Kama unapenda kazi unayo fanya basi kazi hiyo haitakuwa mgumu,bali utakuwa unafanya kitu ambacho kwako ni hobi na mwisho wa siku utafanya kazi kwa bidii na maarifa. Watu waliofanikiwa ni wachapakazi.hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
6.       Uaminifu na ukweli
Hii nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,wateja wengi wanapenda mtu mwamifu na mkweli. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika mazingira ya uaminifu na ukweli ili upate wateja wengi,lazima uwe mkweli katika bei  zako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako mapema sana
7.       Dhamira
Mtu yeyote naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa wa kutosha,kufanya kazi kwa bidii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhamira. Lengo au dhamira ni motisha tosha itakaoyo kupa msukumo mpaka kufikia mafanikio. Dhamira ya kweli inahijajika kabla hujaingia katika biashara au mradi fulani.
8.       Kwenda na wakati
Mjasiriamali lazima aende na wakati ili aweze kutambua mabadiliko mbalimbali yanayo jitokeza katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa nafasi mjasiriamaili kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko huria,kwenda na wakati pia kunatoa fursa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na kusoma magazeti,kufanya utafiti,kurambaza katika mitandao mbalimbali.
Endelea kutembelea mtandao wetu tuendelee kujifunza zaidi.

Imeandaliwa na Jerome Mmassy-Arusha,Tanzania.




Thursday, 9 June 2016

MAMBO AMBAYO MJASIRIAMALI UNATAKIWA KUYAFANYA KILA SIKU ILI UFANIKIWE


Kati ya kitu ambacho kila mjasiriamali mwenye nia ya kufanikiwa anacho ni kule kutaka kuona anakifikia mafanikio makubwa ya kibiashara. Lakini pamoja na kuwa na nia hiyo ya kufikia mafanikio hayo, mjasiriamali huyu hawezi kufanikiwa mpaka ajue mambo ya msingi yanayoweza kumsaidia kufanikiwa na kuyafanya karibu kila siku. Kwa mjasiriamali yoyote atakayeelewa mambo hayo itamsaidia sana kuweza kufikia mafanikio makubwa anayohitaji. Kwa kujifunza kupitia makala haya, itakuonyesha mambo ya wazi ambayo unatakiwa kuyajua kama mjasiriamali na kuyafanya kila wakati ili kuweza kufanikiwa. Sasa twende pamoja kuweza kujifunza mambo unayotakiwa kuyazingatia kila siku katika safari yako ya mafanikio.


1. Panga siku yako mapema. 
Ni rahisi sana siku yako kuwa ya mafanikio ikiwa utaipangilia mapema. Ni vizuri ukaipangilia siku yako mapema ikiwezekana siku moja kabla ili kuweza kujua ni kitu gani utakachokifanya kesho. Hiyo itakusaidia kuweka malengo na kupanga mikakati muhimu ya kutekeleza mapema kichwani mwako kwanza. Kwa mfano usiku kabla hujalala andika kwenye kitabu chako ni nini utachokwenda kufanya kesho. Kwa kufanya hivyo kila siku itakusaidia kufanya mambo mengi kwa urahisi na bila kupoteza muda hovyo. Acha kulala na kuamka kiholela. Unaweza ukaona ni jambo kama dogo, lakini lina msaada mkubwa sana katika safari yako ya mafanikio na ni muhimu kufannya hivi kila siku

2. Amka asubuhi na mapema
Siku zote jifunze kuamka asubuhi na mapema. Unapoamka asubuhi na mapema inakusaidia sana kukamilisha zile kazi ngumu ambazo unatakiwa uzifanye kwa siku husika. Kuamka asubuhi na mapema ni muhimu hiyo yote ni kwa sababu akili yako inakuwa bado na nguvu kubwa ya kutenda mambo mengi na kwa ufanisi mkubwa bila kuchoka. Unaweza ukaamka asubuhi na mapema ukajisomea. Kama wewe ni mwandishi unaweza ukaamka asubuhi na mapema ukaandika au ukapitia malengo yako. Kwa kuamka asubuhi na mapema itakusaidia sana kama mjasiriamali kukufanikisha kwa sababu mipango yako mingi unaweza ukaifanya asubuhi na mapema hata kabla jua halijazama. 

3. Anza siku yako kwa kuwa chanya na maliza ukiwa chanya.
Amka asubuhi kwa kujifunza kuwa chanya. Hiyo itakuwa rahisi kwako ikiwa utajisomea kitabu au utasikiliza kitabu cha sauti kupitia simu au redio. Unapoianza siku yako ukiwa chanya utaifanya siku yako iwe nzuri zaidi. Mambo yako mengi utayafanya kwa hamasa kubwa. Kitu pekee kitakachokufanya uwe hivyo ni kwa sababu uliianza siku yako ukiwa chanya. Lakini si hivyo tu, kama ulivyoanza siku yako chanya ndivyo unatakiwa uimalize kwa namna hiyo. Imalize siku yako kwa kujikumbushia tena malengo yako. Imalize siku yako kwa kujisomea kitabu cha mafanikio hata kwa dakika kumi na tano. Hivi ndivyo unavyoweza ukawa chanya kwa siku yote na itakusaidaia kuwa mjasiriamali wa mafanikio.

4. Tunza na thamini muda wako.
Muda ni kitu cha thamani sana kwa mjasiriamali yoyote. Muda ndio unaotufanya tufanikiwe ama tusifanikiwe. Matumizi ya muda sahihi yanahitajika sana katika kila eneo la maisha yetu kuliko wengi wanavyofikiri. Hivyo kwa maana hiyo ni muhimu sana kuthamini muda tulionao na kufanya yale yaliyo ya muhimu kwetu. Kama ulikuwa ni mtu wa kupoteza muda, achana na hiyo tabia mara moja. Sasa unatakiwa kuishi maisha ya kimafanikio kwa kuthamni na kutunza muda wako sana. Usikubali mtu yoyote akakupotezea muda wako. Wajasirimali wengi wenye mafanikio wanatunza sana muda wao. Kama lengo ni kuwa mjasirimali wa mafanikio ni vyema kujifunza kutunza na kuthamini muda sana kila siku. 

5. Jiwekee lengo la kusonga mbele kila siku.
Mjasiriamali mwenye mafanikio lengo lake kubwa ni kusonga mbele. Haijalishi unakutana na nini? Lakini ukiwa kama mjasirimali unayetaka kufanikiwa thamani kuendelea mbele. Acha kuganda na kung’ang’ania sehemu moja ulipo hiyo haitakusaidia sana. Kikubwa uwe mtu wa kusogea hatua kwa hatua kila siku. Najua kuna wakati tunakutana na changomoto nyingi sana. Pamoja na changamoto hizo zichukulie kama ngazi ya kukupandisha kwenye mafanikio yako. Lakini ikiwa utakubali kukaa chini nakutulia basi elewa wewe mwenyewe utakuwa umeamua kuyapoteza maisha yako bila kujua. Tambua kusonga mbele liwe ndilo lengo lako la kwanza kama mjasiriamali unayetaka mafanikio makubwa. 

6. Jifunze kila siku
Yafanye maisha yako kila siku yawe shule. Kila unachopitia iwe changamoto au kile kizuri unachokiona kutoka kwa watu wengine kifanye kiwe sehemu ya darasa kwako la kukutoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine. Andika yale mambo ya msingi ambayo unaweza ukawa umejifunza na kisha yafanyie kazi kila siku. Hapo itakusaidia sana kuwa mjasiriamali wa mafanikio. Naamini kwa kujifunza mambo hayo, yatakuwa msaada kwako wewe kama mjasiriamali kuweza kufanikiwa kwa kile unachokifanya katika maisha yako. Kumbuka kuchukua hatua na kufanyia kazi kile ulichojifunza.

Karibu tuendelee kujifunza zaidi
Mmassy Jerome, Arusha Tanzania










MATUMIZI MAZURI YA MSHAHARA WAKO YATAKAYOKULETEA FAIDA




GAWANYA MSHAHARA WAKO KATIKA MAFUNGU/BAHASHA HIZI TANO MUHIMU



Mshahara ni makubaliano ya malipo kati ya mwajiri na mwajira kulingana na kazi anayofanya mwajiriwa kwa muda au kipindi fulani kutokana na mkataba wao waliojiwekea waweza kuwa mwezi.
Wakati mwingine unafanya kazi na kupata mshahara lakini hujui au hufahamu sehemu au makundi unayoweza kuugawa mshahara wako.
Zifuatazo ni bahasha tano ambazo unaweza kuugawa mshahara.



1.SADAKA(Tithe Fund)

Unapopata mshahara wako asilimia kumi ya kipato chako yaani mshahara weka katika bahasha hii au mfuko huu wa sadaka. Kutoa asilimia kumi ya mshahara wako ni mwongozo wa kuufuata lakini siwezi kukulazimisha uamuzi uko mikononi mwako BO SANCHEZ katika kitabu chake cha My Maid Invest in the Stock Market alikuwa akiwaambiwa wafanyakazi wake yani wasaidizi wake hivi ‘’ You will grow in abundance think’’ usemi huu wa BO SANCHEZ una maanisha kuwa kuna faida sana pale unapotoa sadaka kama alivyonena hapo juu, ‘’ utakuwa katika uwezo mkubwa wa kufikiri’

2.MATUMIZI ( Expense Fund)

Haya ni yale matumizi ya kila siku ya mahitaji ya nyumbani (daily needs) ambapo pia unaweza ukatenga fungu lingine la mshahara wako au kipato chako na kuweka katika bahasha hii ya matumizi.Hii itakusaidia sana kutotumia hela vibaya na kuwa na nidhamu ya pesa katika mshahara wako na itakusaidia kujuwa kwa mwezi matumizi yako yanagharimu kiasi gani.


3.MSAADA ( Support Fund)

Katika jamii zetu kusaidiana ni jambo la kawaida msaada huo unaweza ukautoa kwa ndugu,jamaa,marafiki na nk.Pengine ni kumsaidia mtaji wa kuanzisha biashara au kuboresha biashara na mengine mengi kuhusiana na msaada.Hivyo weka sehemu ya mshahara wako katika bahasha hii ya msaada hii itakusidia kutoharibu bajeti zako nyingine.


4. DHARURA (Emergence Fund)

Katika maisha yetu ya kibinadamu huwa tunapatwa na dharura sana,na ubaya wa dharura unakuja pale umepatwa na tatizo halafu huna hela ya haraka ya kutatua jambo hilo lakini kama ukiwa umeweka sehemu ya kipato chako katika bahasha hii wala hutopata shida ya kulitatua. Dharura ni nyingi katika maisha na zinatokea kwa ghafla bila taarifa kama vile ajali, radi au kifo kinavyotokea.ukiwa na hela ya dharura itakusaidia kuwa na amani ya akili (Peace of Mind).


5.KUSTAAFU (Retirement Fund)

Hii ni njia moja nzuri ya kuweka akiba na kustaafu ukiwa milionea .Weka ,tenga akiba katika bahasha ya kustaafu na iwekeze hela hii katika soko la hisa . Hela hii weka katika bahasha ya kustaafu na usiitumie bali iwekeze katika soko la hisa na mwisho wa siku una staafu ukiwa milionea.
‘’Kila mtu ana matatizo yake ,Hakuna maisha yasiyo kuwa na matatizo ‘’ usemi huu umedhihirishwa katika kitabu cha Tough Times Never Last ,But Tough People Do kilichoandikwa na Robert H.Schuller ‘’Everybody has problem. No life is problem-free’’

Mmassy Jerome,Arusha


Vikwazo Vitano(5) Vinavyoharibu Mahusiano Yetu Na Ndoa Zetu Na Jinsi Ya Kuviepuka.



Habari rafiki na mpenzi msomaji wa Jesam Blog? Karibu katika makala yetu ya leo ili tuweze kujifunza.

Tunapenda kujifunza kila siku ili tuweze kuijua kweli nayo kweli itatuweka huru. Kama hujui ukweli utapata shida kwani jambo usilolijua ni kama usiku wa giza. Katika maisha yetu ya kila siku tunakumbana na vikwazo mbalimbali. Sasa leo naomba tujifunze vikwazo ambavyo vinaweza kuharibu ndoa yako. Siyo tu maisha ya ndoa hata uchumba na maisha yoyote yenye mahusiano.

Binadamu ni mtu mwenye asili ya mahusiano hapa duniani. Kama wewe ni binadamu basi huwezi kukwepa mahusiano mfano mahusiano na wazazi wako, familia yako, ndugu, jamaa na marafiki








Vifuatavyo ni vikwazo katika maisha ya ndoa, mahusiano mengine na jinsi ya kuviepuka.

1. Uchafu; 
Kila mtu anapenda kuona sehemu anayokaa ni safi au mazingira aliyopo ni safi, vyombo tunavyotumia wakati wa kula, sehemu unayolala, nguo unazovaa, usafi wa mwili nakadhalika. Mtu ambaye ni mchafu huwa ni kikwazo kwa watu wengine anaoishi nao iwe ni katika mahusiano ya kifamilia au ndoa.
Kwa wale watu ambao wako katika maisha ya ndoa kitu kinachoitwa usafi ni jambo la msingi sana na la kuzingatia na siyo kitu siku cha moja bali ni kitu cha siku zote. Wanandoa wote wawili wanapaswa kuzingatia usafi katika maisha yao. Swala la usafi ni katika maeneo yote kuanzia mwili, nguo, sehemu unayolala nakadhalika. Wapo watu wengi wanaharibu ndoa zao kwa sababu tu ya uchafu wewe kama ni mke au mme unaweza kumkwaza mwenza wako kama wewe ni mchafu yaani mtu ambaye hupendi usafi. 
Hatua ya kuchukua;
Kama ulikuwa ni mchafu anza sasa kuwa msafi ili ulinde mahusiano yako. Kuwa msafi wa kila kitu usidharau hata kitu kimoja. Kama ulikuwa ni mtu wa kuvaa nguo bila ya kutofautisha nguo hizi ni za kutokea, shamba, kushindia, kulalia anza leo kuvaa kulingana na wakati wa shughuli husika.
Kama wewe ni mchafu wa kinywa basi safisha kinywa chako kila siku ili usiwe kero kwa mwenza wako na hata watu wengine. Uchafu ni hasara katika mahusiano hivyo kuwa msafi wa mwili, akili nk. na usafi ni faida katika mahusiano


2. Uvivu;
Ashakumu si matusi ndugu msomaji, uvivu ni kama mavi. ‘’mvivu hufanana na jiwe litiwalo mavi, kila mtu atamfyonya katika aibu yake. Mvivu hufanana na uchafu wa jaani, kila augusaye atakung’uta mkono’’ Uvivu ni mbaya sana kama umeweza kufananishwa na kinyesi basi ujue uvivu ni mbaya. Uvivu ni mbaya sana katika maisha ya ndoa na hata maisha mengine kwani uvivu unaleta athari mbaya sana katika maisha yetu ya kila siku. Kama katika maisha ya ndoa wewe ni mvivu basi ni dhahiri kabisa utaweza kuharibu mahusiano ambayo unayo leo hii. 
Mtu mmoja aliwahi kusema unaweza kukwepa wajibu wako lakini huwezi kukwepa matokeo ya majukumu au wajibu wako. 
Hatua ya kuchukua; anza kufanya mambo yako bila kuahirisha, kuwa na ratiba na ukiweka ahadi ya kufanya jambo hakikisha unalitimiza. Dawa ya uvivu ni kuchukua hatua kwa vitendo bila kusubiria. Kila kitu kinawezekana kama ulikuwa ni mvivu wa kuamka mapema asubuhi basi anza zoezi hilo kwa siku 30 na uvivu utaisha wenyewe. Na hapa unahitaji uwe dikteta wa mwili wako hata kama mwili wako haujisikii kufanya jambo kuwa dikteta na wala usiupe demokrasia mwili wako katika kufanya jambo.

3. Ugomvi;
Ugomvi siyo kitu kizuri na siyo alama nzuri katika maisha ya ndoa hata maisha mengine pia, mfano baba na mama kupigana. Ugomvi unaleta athari katika mahusiano mfano kama mama au baba katika familia ni wagomvi wanaleta athari kubwa hata katika malezi ya watoto kwani watoto wanakuwa hawajifunzi somo zuri kupitia wazazi wao.
Ugomvi unaweza kuwa kikwazo kwa wanandoa na kupelekea kuharibu mahusiano yao.
Hatua ya kuchukua;
Ugomvi siyo picha nzuri katika mahusiano. Kama ulikuwa na tabia hii ni vema ukaiacha na kuanza kuishi maisha ambayo yanampendeza mwenzako, familia yako, hata jamii inayokuzunguka.

4. Ulevi ; 
Yule ambaye ni mlevi kati ya wanandoa anakuwa kikwazo kwa mwenza wake. Ulevi wa kupindukia ni athari katika mahusiano ya ndoa na hata watu wengine. Mwenzako anaweza kukerwa na tabia ya ulevi na kupelekea kuharibu mahusiano yenu. 
Ulevi unapelekea watu kusahau majukumu yao katika ndoa zao, familia nk. Ulevi ni utumwa ambao unakufanya kuishi maisha ya ajabu sana.
Hatua ya kuchukua;
Achana na ulevi ili kuokoa mahusiano yako ya ndoa. Anza kusema hapana kubwa kwa ulevi kwani unaharibu mahusiano yako ya kifamilia na hata jamii kiujumla.


5. Ukali;
Ukali ni fedheha mbele ya mwenzako. Kuna watu wanaonyesha ukali kwa mke wake au mme wake mbele ya watu. Ukali unageuka kuwa fedheha endapo unamsema mwenzako mbele ya watu tena kwa sauti kubwa ambayo kila mtu anasikia. Hiki ni kikwazo kwa wanandoa. Pia ukiwa mkali sana ni athari hasi tena kwa malezi ya watoto, watoto wanaweza wakakukimbia nyumbani na kuleta chuki miongoni mwa mzazi na mtoto. Baba kumsema mama kwa ukali mbele ya watoto nayo ni athari mbaya kwani unajenga picha mbaya kwa watoto wanaokuwa na kuhitaji kupata mwongozo kutoka kwa wazazi wao.

Hatua ya kuchukua;
Ukiwa katika hisia kama vile kuwa na hasira usifanye maamuzi yoyote tulia kwanza mpaka hasira zako ziishe. Kama ulikuwa na tabia ya ukali na kumsema mwenzako mbele ya watu siyo tabia nzuri kwani ni fedheha kubwa na hivyo acha kabisa tabia hiyo katika hali ya kawaida ambayo inampendeza mwenzako na familia yako kiujumla. 
Mwisho; katika mahusiano kila mtu ni mteja kwa mwenzako angalia vile vitu ambavyo hupendi kufanyiwa wewe basi usimfanyie mwenzako kwani inakuwa ni kero na kikwazo kwa mwenzako. Kama tulivyoona hivyo vikwazo hapo juu ni tabia ambazo mtu hajazaliwa nazo hivyo ana uwezo wa kuziacha na kuendelea na maisha yanayostahili kuishi.

Hizi Ndizo Lugha Tano (5) Muhimu Za Kuonesha Upendo Kwenye Mahusiano Yetu.


Habari rafiki na mpenzi msomaji wa Blog yetu Natumaini unaendelea vizuri na shughuli zako za kimaendeleo. Karibu tena katika safu hii, leo tutajifunza kuhusu lugha tano muhimu katika mahusiano yetu. Kama tunavyojua siku zote Upendo huanzia nyumbani. Upendo mlionao wakati wa uchumba ndio huohuo mnatakiwa kuuendeleza baada ya ndoa na kupata watoto.
Pia kuna watoto wanaokuzwa kwa upendo, wanaohitajiwa na wanaothaminiwa. Pia kuna watoto wanaokuzwa kwa kutokupendwa, kutokuhitajiwa na kutokuthaminiwa. Watoto wanaopendwa na wazazi wao na jumuiya zao watakuwa na hisia za upendo kutegemea saikolojia zao na upendo waliooneshwa na wazazi wao. Watoto ambao hawajakuzwa kwa upendo hawawezi kuwa na upendo kutegemea na saikolojia zao za kukosa upendo toka kwa wazazi wao na jamii inayowazunguka. Wazungu wanasema ‘’Love makes the world go round’’ (Mapenzi yanaifanya dunia izunguke). Kwa hiyo hatuna budi kuishi kwa upendo ili kuwa na maisha yenye furaha na amani. Zifuatazo ni lugha tano za upendo ;











1. Maneno Yenye Kufariji Na Kutia Hamasa (Words of affirmation/ Verbal Compliments). Unapoongea na mpenzi wa moyo wako mpe maneno yenye kufariji ili umpe furaha. Jaribu kuongea naye kwa upole, maana utamfanya ajisikie raha na kupendwa. Usipende kumkaripia. Pale mpenzi wako anapofanya vizuri mpongeze mfano kama amevaa nguo amependeza jaribu kumsifia kwani unaongeza upendo na kujiamini kwake. Pia akiwaletea zawadi nyumbani mpe maneno mazuri mwambie hata asante kwa zawadi nzuri na usianze tu kuzikosoa hata kama hujazipenda. Usihesabu mabaya maana upendo hauhesabu yaliyo mabaya (Love doesn’t keep a score of wrongs). Pia upendo hauhesabu makosa ya zamani, hakuna mtu miongoni mwetu ambae ni mkamilifu. Upendo unaombwa na sio kulazimisha na kutoa amri. Ukilazimisha na kumuamrisha mpenzi wako unakuwa mzazi na yeye unamgeuza kuwa mtoto. 
Kama tunataka kujenga uhusiano ulio bora lazima tujue kila mtu anapendelea nini. Kama tunataka kupendana lazima tujue nini mwenzako anataka. Kitu ambacho tunaweza kufanya na matatizo yaliyokwisha kutokea ni kuyaacha yawe historia, ndio yalitokea, inauma lakini mpenzi wako amekubali kosa na kukuomba msamaha wako. Kwa hiyo msamaha sio mpaka ujisikie bali ni kujizatiti au kujitoa (forgiveness is not a feeling, it is a commitment). Msamaha ni matendo ya huruma na sio kushikilia kosa la yule aliyekosea. Msamaha unaonesha upendo. Mwanasaikolojia William James alisema kwamba ‘‘Hitaji kubwa la binadamu ni kujisikia anathaminiwa’’ kwa hiyo maneno yenye kufariji na kutia moyo ndio yanaweza kujaza upendo kwa watu wengi katika mahusiano yetu.

2. Kuwa na Muda mzuri (Quality Time). Unatakiwa uwe na muda mzuri na mpenzi wako, tenga muda wa kukaa na mpenzi wako, msikilize anasema nini na anapenda nini. Sio unakaa na mpenzi wako mnaangalia televisheni halafu unajisemea umempa muda mpenzi wako. Unapokuwa umekaa na mpenzi wako hutakiwi ufanye kitu kingine zaidi ya kuwa naye, hakikisha unamwangalia machoni mpenzi wako wakati anaongea. Usimsikilize mpenzi wako huku unafanya kitu kingine kwa wakati huohuo, sikiliza kwa hisia, pia jaribu kuangalia lugha za mwili ili uweze kuelewa kile mpenzi wako anakueleza mfano kukonyeza, kukuminya mguu au hata kufumba macho. Vilevile Usipende kuingilia wakati mpenzi wako anaongea, mwache aongee mpaka amalize ndipo na wewe uongee. Unapaswa kujaza tanki la mapenzi kwa mwenzako kulingana na hisia zake pamoja na mawazo kulingana na muda. 
Pia mnapaswa kufanya shughuli mbalimbali pamoja mfano, kusikiliza mziki, chukueni muda wa kucheza, kuongea kufanya mazoezi ya mwili kusoma vitabu na kushirikishana yale mliojifunza, kaeni muongee kama vile mnatongozana, kuleni pamoja, ulizaneni maswali ya hapo zamani mfano wakati unasoma elimu ya msingi ulikuwa unapendelea somo gani? Kwa kufanya hivyo, utakuwa umejaza tanki la upendo kwa mwenza wako ambaye anajisikia kupendwa pale unapompa muda.

3. Kupokea Zawadi (Receiving Gifts). Kuna wapenzi wengine wanajisikia upendo pale wanapoletewa zawadi na wenza wao. Kwa mfano, pete ni kitu kinachoonekana na ni ishara ya upendo na muunganiko wa nafsi mbili katika upendo ambao hauna ukomo. Zawadi ni alama zinazoonesha upendo. Mpe mpenzi wako zawadi na kama akikuuliza mjibu ‘najaribu kujaza tanki lako la upendo, unapompa mpenzi wako zawadi anajisikia upendo na sio lazima umnunulie vitu vya bei kubwa. Unaweza hata ukachuma ua la rose na kumpa mpenzi wako wakati unatoka kazini kwako, huwezi jua kiasi gani utakuwa umemfurahisha ila ni yeye mwenyewe ndio ataona kiasi gani umeonesha kumjali na kumthamini. Unaweza ukamtengenezea mpenzi wako kadi kwa kutumia mkasi na karatasi, kata karatasi hilo hata umbo la mduara au kopa na andika maneno I loveYou.
Kwa kufanya hivyo utakuwa umefanya jambo la maana na la msingi sana. Utazidi kumfanya mpenzi wako ajisikie raha na kuona hakuna kama yeye katika dunia hii. Kuonesha upendo kwa njia ya zawadi sio lazima uwe na fedha nyingi ili uweze kununua zawadi kubwa kubwa kama gari au nguo bali unaweza hata kununua pipi ya shilingi mia moja au chokoleti kama mpenzi wako anapenda vitu hivyo. Usikae chini usubiri mpaka upate hela ili labda umnunulie mpenzi wako zawadi ya nguo, anza sasa kwa vitu vidogo vidogo visivyohitaji pesa nyingi. Pia kuna watoto wengine wanapenda sana zawadi hivyo basi unapotoka kazini usiache kumletea mwanao zawadi mfano, ua, box la kuchezea, jani au kitu chochote ili ajisikie kupendwa na wewe mzazi ujaze tenki la upendo kwa mwanao.

4. Kusaidiana Katika Mambo Mbalimbali (Acts of Service). Kama wapenzi mnatakiwa kusaidiana kufanya shughuli mbalimbali. Saidianeni kwa upendo (Serve one another in love), Kama wapenzi mnatakiwa kusaidiana kufanya mambo mbalimbali mfano mama akiwa jikoni anapika baba anaweza akatoka nje na kukata majani yaliyopo kwenye uwanja wenu wa nyumba. Au mama akiwa anafua nguo za watoto baba anaweza kukaa na mtoto au watoto na hata kuwabadilisha nepi au pampasi. Kwa kufanya hivyo upendo unazidi kuimarika na tenki la upendo la mwenza wako ambae anapenda kusaidiwa kazi litakuwa limejaa na hata kuweza kufurika (full tank and overflowing).

5. Kuguswa Kimwili (Physical Touch). Risechi nyingi zimehitimisha kuwa watoto wanaokumbatiwa, kupakatwa na kubusiwa wanakuwa na afya nzuri ya kihisia kuliko wale ambao wanaachwa kwa muda mrefu bila kuwa na mguso wa kimwili. Kujamiiana ndio lahaja pekee katika mapenzi. Kama mume wako anapenda kukutana kimwili usimkatalie mpe ili ujaze tanki lake la upendo mpaka lifurike. Mume anaweza akawa hapendi kula vyakula mbalimbali na kitu chake kikubwa anachopenda ni tendo la ndoa hivyo basi wewe kama mke usihangaike kupika vyakula vya kila aina ukafikiri mume wako ndio atajisikia kupendwa. Kama lugha ya upendo ni kuguswa kimwili basi jitahidi kumpa mume wako muda mwingi huko kulikoni kitu kingine na vivyo hivyo na atendewe mke. Sio mke anataka mguso wa kimwili na mume wake halafu mume yuko bize na kompyuta au simu. Kufanya hivyo utakuwa umemuumiza mwenza wako na utamfanya ajisikie kukosa upendo.
Mguso wa kimwili unaweza kujenga au kubomoa uhusiano. Kugusa mwili wa mpenzi wako ni kumgusa yeye na kutomgusa mwili mpenzi wako ni kujiweka naye mbali kihisia. Hivyo basi ili mahusiano yadumu mguso wa mwili ndio kitu kikubwa na chenye umuhimu hivyo wanandoa au wapenzi hawana budi kugusana miili yao ili kuimarisha upendo. Kama unaweza kumkumbatia au kumbusu mpenzi wako mfanyie wala hauhitaji ruhusa wala mtaji katika hili.
Kwa kuhitimisha, upendo ni chaguo na upendo hauchagui, wapende hata maadui zako na wale wasiopendwa. Unapaswa ujue lugha yako ya upendo na hata ile ya mwenza wako ili muweze kujaza matenki yenu ya upendo mpaka yamwagikie na kufurika (overflowing love) na pia muweze kuishi kwa upendo ulio mkuu. Kama bado hujajua lugha ya upendo ya mpenzi wako mfano kupokea zawadi, kuguswa kimwili au hata kuwa na muda mzuri na mpenzi wako anza sasa kuijua ili uweze kumtimizia vile vitu anavyopenda na usije ukawa unapoteza muda kwenye kitu ambacho hakipendi. Hivyo ni muhimu kujua lugha ya upendo ya mwenzako ili kila mmoja awe na uelewa unaoshabihiana yaani mutual understanding.




Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy wa AMKA TANZANIA

KWA WALE WANAOHITAJI KUSOMA NJE YA NCHI,WATAFUTE HAWA JAMAA CHAP

Looking for an opportunity (yourself or your family members) to study abroad or online? Come and visit us at SABRAHM CONSULTING LTD in Corridor Springs Hotel, phone: +255 688 763 923 & +255762 875 209 (English) or +255788 501 475 (Swahili).  We can help you!

SABRAHM is an Agent of KAPLAN INTERNATIONAL COLLEGES in the UK.




Dr. Leontine Mabika
Managing Director of SABRAHM Consulting LTD
Conference Coordinator and Conference Interpreter
Member of AIIC ( International Association of Conference Interpreters)
P.O. Box 16200, Arusha, Tanzania.
-- 



Mzizi Mkavu : SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI, INASABABISHWA NA NGO...

Mzizi Mkavu : SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI, INASABABISHWA NA NGO...: UTAFITI mpya wa kitabibu umebaini kuwa saratani ya shingo ya kizazi, inasababishwa pamoja na mambo mengine na ngono kama ilivyo k...

Mzizi Mkavu : MUHIMU KUJUWA WAKATI UNA MIMBA

 MUHIMU KUJUWA WAKATI UNA MIMBA: Wanawake wengi hujua wameshika mimba aghalabu wiki 3 baada kushika mimba. Mwili wenyewe utakuonyesha/utakutabiria kama: Hedhi yako itakoma...

Mzizi Mkavu : KUUMWA TUMBO WAKATI WA HEDHI

Mzizi Mkavu : KUUMWA TUMBO WAKATI WA HEDHI: KARIBU sana katika makala yetu inayohusu afya.Kutokana na simu nyingi ninazozipata nikiulizwa maswali juu ya maumivu yanayowapata akina...

THIS IS THE POSITIVE MOBILITY AS TANZANIA OUTS KENYA'S POWER HOUSE

Less than a year after President Magufuli took office, Tanzania is already gaining influence among its neighbors and moving away from its reputation as a lone ranger in the region. So what does this mean for Kenya?

Tansania Präsident John Magufuli
Despite having the largest population in East Africa, Tanzania has often been sidelined in regional politics. While Kenya's influence surged, Tanzania was accused of being too slow and cautious when it came to plans for regional integration and infrastructure.

But since John Magufuli's surprise election win last October, it seems Kenya could be losing its grip on East African politics as Tanzania increasingly presents itself as a viable alternative for regional cooperation.



Just last week, the Ugandan government announced it would route the country's valuable oil exports through Tanzania rather than Kenya, opting for a pipeline to the Tanzanian port city of Tanga.

A report commissioned by the Ugandan government in March found that the pipeline route through Tanzania was cheaper and would be in operation more quickly than the Kenyan option. The decision was a blow for Kenya, which will now have to go through with its own ambitious oil pipeline project alone, or find new partners.

An international railway project, championed by Kenya, has also come up against difficulties as regional players consider their options. Widespread media reports claimed that Rwanda was pulling out of plans to develop rail links to Indian Ocean ports through Kenya in favour of routes through Tanzania. But the Rwandan government has now said it plans to continue with both routes.

Magufuli's new approach

The readiness of Uganda and Rwanda to embark on projects and agreements with Tanzania, particularly when it means breaking off deals with Kenya, is a mark of the shift of influence within the region. Kenyan political analyst and commentator Martin Oloo told DW that President Magufuli's pragmatic, hands-on approach is making this possible. "It is changing the way business can be done: in a more efficient and effective way," he said.

Rwandan President Paul Kagame shakes hands with President Magufuli 
President Magufuli visited his Rwandan counterpart Paul Kagame last month
One of Magufuli's key policies is cracking down on corruption. "What is endearing him to his own people and perhaps what is making sense economically for the region is that business can be done in cheaper ways, business can be done by minimizing corruption," Oloo said. "And corruption is expensive, so countries where there is runaway corruption, like in Kenya. That's impeding its competitiveness, its impeding its relevance within the region," he added.

Stability and growth

But Tanzania's recent political gains are not only down to Magufuli's leadership style. The country has enjoyed a steady growth rate of 6 - 7 percent over the past decade and is already starting to overtake Kenya economically. "Magufuli's performance will only be helping that to happen faster," Oloo said.

Despite widespread poverty, long term political stability has provided a solid foundation for growth and development. "You can decide to look at Kenya as a powerhouse maybe on the economic side, but you've got to accept that Tanzania is a powerhouse in terms of stabilizing these countries," said Richard Shaba, Program Coordinator at the Konrad Adenauer Foundation in Tanzania, a German political foundation. "We take most of the refugees. We do most of the reconciliation whenever these countries have a problem," Shaba told DW.

When it comes to stability, Kenya is struggling. Security has become a growing fear, not only for Kenyans but also investors. The country's border with Somalia makes it vulnerable to attacks from Somali terrorist group al-Shabab, making Tanzania an attractive alternative.

Kenyan police carry the body of a man killed in an al-Shabab attack 
Kenyan police deal with casualties following an al-Shabab attack on a village on Kenya's border with Somalia last year
What's next for East Africa?

In the face of these difficulties, Kenya will now have to up its game if it wants to retain its regional strength. "What should be worrying Kenyans is that we need to take on runaway corruption, we need to improve efficiency, we need to make ourselves competitive within the region," said analyst Oloo. "And unless we do that, then our neighbors like Tanzania and Rwanda are actually going to run away with the opportunities."

If the latest developments in terms of regional cooperation are anything to go by, that is already happening. But according to Richard Shaba, even Magufuli's unconventional approach won't completely change Tanzania's traditionally guarded politics when it comes to cooperation and integration in East Africa.

"I think Tanzania will pursue more or less the same regional politics - being a bit cautious - because when the East African Community collapsed in 1977 we got our fingers burned very badly," he told DW. "Willingness is always there, but the approach will be cautious."

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...