Saturday, 12 March 2016

GAVANA AMJIA JUU RAIS MAGUFULI: AKIUKA AGIZO LAKE

Hatimaye gavana wa BoT Prof. Beno Ndulu ametoa majibu kwa rais John Magufuli huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua na kuomba apewe majina pamoja na taarifa za wale watu wanaodhani kuwa ni wafanyakazi wasio na umuhimu BoT.

Hayo yanajiri siku moja baada ya rais John Magufuli kumuagiza gavana huyo kuwaondoa ndani ya utumishi wa BoT wafanyakazi wote wasio na umuhimu pamoja na wale wanaojulikana kuwa ni wafanyakazi hewa.

Jana gavana akiongea na vyombo vya habari pamoja na gazeti la MTANZANIA alisema kuwa kila mfanyakazi wa BoT ana umuhimu wake huku akisisitiza kuwa watu wanaongea wasiyoyajua. Prof. Ndulu pia alisisitiza kuwa yule anayedhani kuwa kuna wafanyakazi wasio na umuhimu BoT basi ampelekee majina yao pamoja na taarifa zao!

Hata hivyo gavana huyo aliweka wazi kuwa rais ametoa agizo hivyo ni muhimu kuzingatia agizo la rais lakini akaweka mkazo kuwa BoT itajiridhisha kwa kina kwanza kabla ya kuchukua hatua yoyote ile! 

My take: Jana nilileta thread humu huku nikisisitiza kuwa huenda rais hajui kile anachokizungumza kuhusu BoT na nikaenda mbali zaidi kuelezea namna utumishi ulivyo pale BoT! Watu mkaja na povu huku mkituma mashambulizi ya kila aina! Haya na leo mjibuni Beno Ndulu! Au mwambieni rais atumbue majipu!

BoT ni taasisi nyeti iliyobeba wafanyakazi ambao kimsingi wanawajibika kwa kina kuhusu nchi! BoT ni taasisi iliyounganishwa kimataifa!


No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...