Tuesday, 14 June 2016

BIASHARA TANO UNAZOWEZA KUANZISHA UKIWA NA MTAJI CHINI YA LAKI MOJA TU. 100,000/=


Mitaji imekuwa kikwazo kikubwa katika kuanza biashara nyingi sana. Sababu nyingine ni kuwa watu wengi wanaofikiria kuanza biashara wanataka kuanza na mitaji mikubwa kama milioni 5 -10 au zaidi. Ukweli ni kwamba hiyo ni ngumu hasa kwa nchi ambazo ni maskini kama Tanzania.

Mwishowe mawazo mengi ya biashara yanakufa kabla ya kuanza.

Wataalamu wa bishara wanaeleza kuwa kuanza ni kugumu na ni kikwazo kikubwa cha mafanikio ya wajasiliamali wengi

Ukweli ni kuwa kuna biashara nyingi tu ambazo hazihitaji mitaji mikubwa kuanza.



1. Kufundisha

Tafuta kitu ambacho unakifahamu na angalia jinsi utawapa watu elimu yako.

Mfano unaweza ukawa ni mtaalamu wa kupika keki tamu. Basi unaweza ukaanda darasa la watu katika maeneo unayoishi na kuandaa mafunzo kwa ada ndogo nyumbani kwako.

Unahitaji kiasi kidogo tu cha fedha ili kutimiza hilo.



Pia unaweza ukafundisha watoto masomo ya ziada kama hesabu au sayansi kama unaufahamu wa masomo hayo au mengineyo.

Vyote hivi havihitaji hela nyingi kuanza kwasababu huhitaji chumba cha biashara wala fanicha.



2. Biashara ya Mtandao

Jiunge na kampuni inayofanya masoko kwa njia ya mtandao. Makampuni haya yatakuhitaji wewe kuafanya matangazo kwa njia ya mdomo kwa mtu hadi mtu kwa kuwaeleza juu ya bidhaa za kampuni husika na wakinunua basi kampuni itakulipa wewe kiasi cha fedha kwa mauzo yaliyofanyika.



Usajili katika biashara hii kunahitaji mtaji mdogo sana hata kwa Sh. 100,000 tu unaweza ukaanza na kuendelea kukuza mtaji.

Baadhi ya biashara za mtandao kuanza
Rifaro: Soma :Fursa ya Rifaro , Namna ya Kukuza Kipato na Fursa ya Biashara ya Rifaro Africa
Trevo: Soma: Biashara Trevo- Kwa Afya na Kipato

3. Kutoa Ushauri wa Kitaalamu


Kama wewe ni mtaalamu katika nyanja fulani kama vile fedha,afya au komputa kwa mfano,unaweza ukaanzisha huduma ya ushauri kwa makampuni madogo au watu binafsi.



Ili kufanya hivyo utahitaji fedha kidogo tu kwaajili ya vitendea kazi kama vile karatasi, kalamu n.k

Utahitaji kujitangaza kwa kupita ofisi hadi ofisi au kwa kutoa matangzao katika radio ,TV au magazeti.

Unaweza kutumia ofisi za wateja kwajili ya kazi hii hivyo kuwa na ofisi. Tumia sehemu unayoishi kama ofisi hivyo ngarama itakuwa ndogo sana.



4. Huduma ya Kutunza Watoto Wadogo


Kutunza watoto wadogo kati ya mwaka 1-5 ni biashara ambayo unaweza ukaianzisha na kuifanya nyumbani na itahitaji fedha kidogo tu.

Wazazi wenye watoto wanahitaji sehemu ambayo watoto wao watapata huduma wao wakiwa kazini.

Kama ukianda mazingira mazuri ampapo watoto wanaweza kucheza na kujifunza,basi utapata wateja wengi.



5. Kukodisha Hema



Huduma ya kukodisha hema kwaajili ya shughuli ni mijawapo ya biashara ambazo hazihitaji mitaji mikubwa.

Utahitaji hema moja au mawili ili kuanza na kisha unaweza ukaongeza kadiri unavyoendelea na kukua.

Uhitaji wa hudum hii ni mkubwa hasa katika shrehe za harusi,siku za kuzaliwa,kipaimara ,komunio,maulidi na bia katika shughuli za misiba.



Biashara zote nilizozitaja hazihitaji fedha nyingi kuanza,kiukweli Shilingi 100,000 tu au pungufu zinatosha.

Hivyo kama unafikiria kuanza bishara na huna mtaji wa kutosha;basi fikiria mojawapo kati ya hizi na ufanikiwe.

Ningependa kusikia biashara nyingine kama hizi. Andika katika kisanduku cha maoni hapa chini nautume.

NJIA SAHIHI ZA KUPATA MAFANIKIO HALALI



MTU anafanikiwa kikweli kwa kupata njia bora kabisa ya maisha ambayo inatokana na kufuata viwango vya Mungu na kuishi kupatana na kusudi la Mungu kwa wanadamu. Biblia inasema kwamba mtu anayeishi maisha ya aina hiyo “atakuwa kama mti uliopandwa kando ya vijito vya maji, ambao hutoa matunda yake katika majira yake na ambao majani yake hayanyauki, na kila jambo analofanya litafanikiwa.”—Zaburi 1:3.

Naam, ingawa sisi si wakamilifu na tunafanya makosa, tunaweza kufanikiwa maishani! Je, hilo linakuvutia? Ikiwa ndivyo, basi kanuni sita zinazofuata za Biblia zinaweza kukusaidia ufikie lengo hilo na hivyo kuthibitisha waziwazi kwamba kwa kweli mafundisho ya Biblia ni hekima inayotoka kwa Mungu.—Yakobo 3:17.

1 Uwe na Maoni Yanayofaa Kuhusu Pesa

“Kupenda pesa ni chanzo cha mambo mabaya ya namna zote, na kwa kujitahidi kufikia upendo huo wengine . . . wamejichoma wenyewe kila mahali kwa maumivu mengi.”(1 Timotheo 6:10) Ona kwamba tatizo si pesa, kwa kuwa sisi sote tunahitaji pesa ili kujitunza na kutunza familia zetu. Tatizo ni kupenda pesa. Kwa kweli, upendo huo hufanya pesa ziwe bwana, au mungu.

Kama tulivyoona katika makala ya kwanza ya mfululizo huu, watu ambao hukimbizana na utajiri ili wapate mafanikio, kwa kweli wanafuatilia upepo. Mbali na kutamaushwa wanapatwa na maumivu mengi. Kwa mfano, katika jitihada zao za kutafuta mali nyingi, mara nyingi watu hupuuza uhusiano wao wa familia na marafiki. Wengine hukosa usingizi, si kwa sababu ya kazi tu, bali pia kwa sababu ya wasiwasi. “Usingizi wa kibarua ni mtamu, awe ameshiba au amekula kidogo tu. Lakini usingizi wa tajiri ni wa wasiwasi daima, maana ziada ya mali yake humsumbua usiku kucha,” inasema Mhubiri 5:12.—Biblia Habari Njema.

Zaidi ya kuwa bwana mkatili, pesa ni bwana mdanganyifu pia. Yesu Kristo alizungumza kuhusu “nguvu za udanganyifu za utajiri.” (Marko 4:19) Hilo linamaanisha kwamba utajiri humwahidi mtu kwamba utampa furaha, lakini haufanyi hivyo. Badala yake unamfanya mtu atamani utajiri zaidi. “Anayependa fedha hatatosheka na fedha,” inasema Mhubiri 5:10.

Kwa ufupi, mtu anayependa pesa anajiumiza tu. Anavunjika moyo, anakatishwa tamaa, au hata kujihusisha katika uhalifu. (Methali 28:20) Ukarimu, kuwa tayari kusamehe, usafi wa maadili, upendo, na uhusiano mzuri pamoja na Mungu, ni mambo yanayoleta furaha na mafanikio.

2 Sitawisha Roho ya Ukarimu

“Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.” (Matendo 20:35) Ingawa kuwapa watu vitu mara kwa mara kunaweza kumfanya mtu awe na furaha ya muda, roho ya ukarimu inaweza kumfanya awe na furaha ya kudumu. Ni kweli kwamba kuna njia mbalimbali za kuonyesha ukarimu. Mojawapo ya njia bora na inayothaminiwa sana ni kutenga wakati ili kuwa pamoja na watu na kufanya mambo nao.

Baada ya kupitia uchunguzi mwingi kuhusu furaha, afya, na kutokuwa na ubinafsi, mchunguzi Stephen G. Post alisema kwamba kutokuwa na ubinafsi na kuwasaidia wengine kunahusianishwa na maisha marefu, afya nzuri kimwili na kiakili, kutia ndani kupunguza kushuka moyo.

Isitoshe, watu wanaowapa watu vitu kwa ukawaida hawapungukiwi na chochote maishani kwa sababu tu ya kuwa wakarimu. Methali 11:25 inasema hivi: “Mtu mkarimuatafanikishwa, amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa.” (BHN) Kupatana na maneno hayo, watu ambao ni wakarimu kutoka moyoni, ambao hawawapi watu vitu wakitarajia kulipwa, wanathaminiwa na kupendwa na Mungu.—Waebrania 13:16.

3 Samehe kwa Hiari

“Endeleeni . . . kusameheana kwa hiari ikiwa yeyote ana sababu ya kulalamika juu ya mwingine. Kama vile Yehova alivyowasamehe ninyi kwa hiari, nanyi fanyeni vivyo hivyo pia.” (Wakolosai 3:13) Siku hizi, watu hawako tayari kusamehe; wao hulipiza kisasi badala ya kuonyesha rehema. Matokeo ni nini? Wanapotukanwa wanatukana, nao hulipiza jeuri kwa jeuri.

Mambo hayaishii hapo tu. Ripoti moja katika gazeti The Gazette la Montreal, Kanada inasema kwamba “katika uchunguzi uliofanyiwa watu zaidi ya 4,600 wenye umri ya kati ya miaka 18 hadi 30,” wachunguzi “waligundua kwamba uhasama, kukata tamaa, na kutokuwa na fadhili” hufanya mapafu yawe mabovu. Kwa kweli, mambo hayo yanaweza kufanya mapafu ya mtu kuwa mabovu zaidi kuliko ya mvutaji wa sigara! Bila shaka, kusamehe hakufanyi iwe rahisi kushughulika na wengine tu bali pia kunafaidi afya yetu!

Unawezaje kusamehe zaidi? Anza kwa kujichunguza kwa unyoofu. Je, nyakati nyingine huwakasirishi watu? Unafurahi wanapokusamehe? Kwa hiyo, mbona usiwaonyeshe wengine rehema? (Mathayo 18:21-35) Pia ni muhimu kujizuia. “Hesabu moja hadi kumi” au tafuta wakati ili utulize hasira. Tambua kwamba kujizuia si udhaifu. “Asiye mwepesi wa hasira ni bora kuliko mwanamume mwenye nguvu,” inasema Methali 16:32. Maneno “ni bora kuliko mwanamume mwenye nguvu” yanaonyesha mtu amefanikiwa kikweli, sivyo?

4 Ishi Kulingana na Viwango vya Mungu

“Amri ya Yehova ni safi, huyafanya macho yang’ae.” (Zaburi 19:8) Kwa ufupi, viwango vya Mungu vinatufaidi, kimwili, kiakili, na kihisia. Vinatulinda dhidi ya mazoea yenye kudhuru kama vile, kutumia dawa za kulevya, kulewa, ukosefu wa maadili, na kutazama ponografia (picha au habari za ngono). (2 Wakorintho 7:1; Wakolosai 3:5) Huenda mazoea hayo yakatokeza madhara mabaya kama vile uhalifu, umaskini, kutoaminiana, kuvunjika kwa familia, matatizo ya kiakili na kihisia, magonjwa, na kifo cha mapema.

Kwa upande mwingine, wale wanaoishi kulingana na viwango vya Mungu wanakuwa na mahusiano mazuri, pia wanajiheshimu, na kuwa na amani ya akili. Katika Isaya 48:17, 18, Mungu anasema kwamba yeye ndiye “anayekufundisha ili ujifaidi mwenyewe, Yeye anayekufanya uende katika njia unayopaswa kutembea ndani yake.” Kisha anaongeza hivi: “Laiti ungesikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingekuwa kama mto, na uadilifu wako kama mawimbi ya bahari.” Ndiyo, Muumba wetu anatutakia maisha bora zaidi. Anataka ‘tuende katika njia’ ya mafanikio ya kweli.

5 Onyesha Upendo Usio na Ubinafsi

“Upendo hujenga.” (1 Wakorintho 8:1) Je, unaweza kuwazia maisha yasiyo na upendo? Yangekuwa maisha yasiyo na maana kama nini! “Ikiwa . . . sina upendo [kwa wengine], mimi si kitu. . . . Sipati faida hata kidogo,” akaandika Paulo, mtume Mkristo aliyeongozwa na roho ya Mungu.—1 Wakorintho 13:2, 3.

Upendo unaotajwa hapa si ule wa kimahaba ambao una mahali pake panapofaa. Badala yake ni upendo unaodumu ambao unaongozwa na kanuni za Mungu.* (Mathayo 22:37-39) Isitoshe, mtu haonyeshwi tu upendo huo bali anauonyesha kwa matendo. Paulo aliendelea kusema kwamba upendo huo ni wenye subira na pia fadhili. Hauna wivu, haujigambi, au kujivuna. Hutafuta faida za wengine, na hauchokozeki kwa urahisi bali ni wenye kusamehe. Upendo kama huo hujenga. Pia, unatusaidia tuwe na uhusiano mzuri na wengine hasa washiriki wa familia.—1 Wakorintho 13:4-8.

Kwa wazazi, upendo unamaanisha kuwa na hisia nyororo kuwaelekea watoto wao na kuwapa mwongozo ulio wazi unaotegemea Biblia kuhusu maadili na tabia nyingine. Watoto wanaolelewa katika mazingira kama hayo hujihisi salama, wanapendwa, na kuthaminiwa wakiwa sehemu ya familia iliyo imara.—Waefeso 5:33–6:4; Wakolosai 3:20.

Jack, anayeishi Marekani, ni kijana aliyelelewa katika familia iliyofuata kanuni za Biblia. Baada ya kuondoka nyumbani, Jack aliwaandikia wazazi wake barua. Sehemu ya barua hiyo ilisema hivi: “Jambo moja ambalo nimejitahidi kufanya ni kufuata agizo [la Biblia] linalosema: ‘Mheshimu baba yako na mama yako . . . ili mambo yakuendee vema.’ (Kumbukumbu la Torati 5:16) Mambo yameniendea vema. Na sasa ninathamini kwamba imekuwa hivyo kwa sababu mlijitahidi kunilea kwa upendo. Asanteni sana kwa kunitegemeza na kwa jitihada zenu nyingi za kunilea.” Kama wewe ni mzazi, ungehisije kama ungepokea barua kama hiyo? Je, hungejawa na shangwe moyoni?

Pia, upendo unaotegemea kanuni ‘unashangilia pamoja na kweli,’ yaani, kweli kumhusu Mungu inayopatikana katika Biblia. (1 Wakorintho 13:6; Yohana 17:17) Ili kufafanua, fikiria mfano huu: Wenzi walio na matatizo katika ndoa yao wanaamua kusoma pamoja maneno ya Yesu yanayopatikana kwenye Marko 10:9: “Kwa hiyo kile ambacho Mungu ameunganisha [katika ndoa] mtu yeyote asikitenganishe.” Sasa, lazima wajichunguze mioyo yao. Je, kweli ‘wanashangilia pamoja na kweli za Biblia’? Je, wataiona na kuitendea ndoa kama kitu kitakatifu, kama vile Mungu anavyoiona? Je, wako tayari kujitahidi kutatua matatizo yao kwa upendo? Kwa kufanya hivyo wanaweza kufanya ndoa yao ifanikiwe, na wanaweza kushangilia matokeo mazuri ya jitihada zao.

6 Tambua Uhitaji Wako wa Kiroho

“Wenye furaha ni wale wanaotambua uhitaji wao wa kiroho.” (Mathayo 5:3) Tofauti na wanyama, wanadamu wana uwezo wa kuthamini mambo ya kiroho. Kwa sababu hiyo, sisi hujiuliza maswali kama haya, Ni nini kusudi la uhai? Je, kuna Muumba? Ni nini hutupata tunapokufa? Wakati ujao utakuwaje?

Ulimwenguni pote, mamilioni ya watu wanyoofu wametambua kwamba Biblia inajibu maswali hayo. Kwa mfano, swali la mwisho linahusiana na kusudi la Mungu kwa wanadamu. Kusudi hilo ni nini? Ni kwamba dunia iwe paradiso inayokaliwa na watu wanaompenda Mungu na viwango vyake. Zaburi 37:29 inasema: “Waadilifu wenyewe wataimiliki dunia, nao watakaa milele juu yake.”

Ni wazi kwamba Muumba wetu anataka tufanikiwe kwa muda mrefu zaidi kuliko miaka 70 au 80 tu. Anataka tufanikiwe milele! Kwa hiyo, sasa ndio wakati wako wa kujifunza kuhusu Muumba wako. Yesu alisema: “Uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na juu ya yule uliyemtuma, Yesu Kristo.” (Yohana 17:3) Unapoendelea kupata ujuzi huo na kuutumia maishani, utagundua kwamba “baraka ya Yehova . . . ndiyo hutajirisha, naye haongezi maumivu pamoja nayo.”—Methali 10:22.

Ahsante na karibu tena 

Jerome Mmassy-Arusha Tanzania

Monday, 13 June 2016

MAMBO MAGUMU KWA MAGUFULI NDANI YA CCM

Magufuli atikiswa.
[​IMG]

Hii habari ni kutoka katika gazeti la Raia Mwema, toleo la 461 la tarehe 8 Juni 2016

Vigogo wapanga kumpindua

SASA ni rasmi kwamba kuna vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanajipanga kuzuia Rais John Magufuli asiwe Mwenyekiti wa chama hicho baadaye mwaka huu kama inavyotarajiwa na wengi, Raia Mwema limeambiwa.

Gazeti hili limeambiwa kwamba mkakati huo unapangwa kwa siri kubwa na kwamba utatekelezwa wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao.

Vyanzo vya kuaminika vya gazeti hili vimeeleza kuwa kuna wajumbe ambao watasimama na kutoa hoja kwamba si lazima kwa Mwenyekiti wa CCM kuwa pia Rais kutokana na sababu mbalimbali.

“Kuna sababu kadhaa ambazo zitatumika. Kwa mfano, kuna watakaosema kwamba dunia nzima hivi sasa mfumo huo hautumiki. Nchi zinazotajwa kutotumia mfano huo ni Kenya, Afrika Kusini na hata Marekani.

“Hoja itakuja kwamba kazi za chama ni za chama na za serikali ni za serikali. Wataeleza kuwa Jacob Zuma (Rais wa Afrika Kusini) si Rais wa chama tawala (ANC). Rais wake anaitwa Baleka Mbeke.

“ Kuna wengine watatoa hoja kwamba katika hali ya sasa, kama Rais akichukiwa, basi na chama kitachukiwa pia kama mtu mmoja atashika nafasi hizo mbili.

Ni muhimu chama kiokoe serikali au serikali iokoe chama na si wote wazame kwa pamoja,” kilieleza chanzo hicho ambacho ni mmoja wa wanachama waandamizi wa CCM waliowahi kushika nyadhifa za juu serikalini.

Hata hivyo, mtoa habari wetu huyu ambaye aliomba kutotajwa jina kwa maelezo kuwa wahusika ni watu anaofahamiana nao vizuri; alisema kwamba ni wazi Rais Magufuli ana taarifa hizo na kwa vyovyote atajiandaa kupambana na hali hiyo.

Mmoja wa vigogo wanaotajwa kuhusika na mpango huu aliliambia gazeti hili kwenye mahojiano naye yaliyofanyika Dar es Salaam kuwa haoni kama ni tatizo kama kuna wana CCM wanaoamini kuwa utaratibu wa Mwenyekiti wa chama kuwa pia Rais wa nchi umepitwa na wakati.

“ Sikiliza, mimi sitaki unitaje jina kwenye gazeti lako kwa sababu ukifanya hivyo utakuwa tayari umenihukumu kwamba nimo kwenye huo mpango. Mimi sijui chochote.

“Hata hivyo, sidhani kama wanaofikiri tofauti wanakosea. Kama wataibua hoja hiyo, itapewa majibu na huo ndiyo utaratibu wetu ndani ya CCM.

“Kama watu wanaona kwamba kitu kimepitwa na wakati watasema tu. Tulikuwa na Azimio la Arusha baadaye likabadilishwa. Tulikuwa tumekataza wafanyabiashara kwenye siasa lakini baadaye tukawarudisha na sasa tunafikiria kuwatenganisha na siasa. Hayo yote ni mawazo”, alisema kigogo huyo ambaye ni mwanasiasa maarufu wa CCM ambaye aliwania urais na Magufuli katika mchakato wa ndani wa CCM mwaka jana.

Katika miaka ya 1990, aliyewahi kuwa Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kuwaambia wanachama wa chama hicho kuwa ni muhimu kwa mtu mmoja kushika nyadhifa zote hizo kwa sababu ya umoja na utengamano ndani ya chama.

“ Mnaweza kuamua kuwa na Rais mtu mwingine na Mwenyekiti wa chama. Lakini omba Mungu wapatane maana wasipopatana itakuwa vurugu tupu,” Mwalimu alinukuliwa kusema wakati huo.
Katika historia ya CCM, ni Mwalimu pekee aliyepata bahati ya kuwa Mwenyekiti wa chama wakati Rais wa Tanzania akiwa Ali Hassan Mwinyi, lakini wanasiasa wakongwe kama Pius Msekwa wanaamini kuwa isingekuwa rahisi kwa Nyerere kuondoka ghafla madarakani kwa kuacha nyadhifa zake zote.

Katika mahojiano yake aliyowahi kufanya na gazeti hili nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Msekwa alisema kwamba anaamini Mwenyekiti wa sasa wa CCM, Jakaya Kikwete, atamuachia Magufuli wadhifa huo mapema.

“Katika historia ya Tanzania, ni Nyerere pekee ndiye aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM kwa muda mrefu huku mzee Mwinyi akiwa Rais. Lakini kulikuwa na sababu wakati huo kwamba Watanzania walikuwa wakimpenda sana Mwalimu na nchi ingetikisika kama angeachia nyadhifa zote mbili,” alisema Msekwa mapema mwaka huu.

Wakati gazeti hili likiwa na taarifa kwamba baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu huo tayari wameanza kutumiwa mialiko ya kwenda kuhudhuria mkutano huo, kuna wajumbe wameanza kudai kwamba mkutano huo ‘hautanoga’ kufanyika wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ulioanza wiki hii.

Raia Mwema limeambiwa kwamba sababu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mojawapo ya zile zinazoanza kuibuka sasa kutaka Mkutano Mkuu wa CCM usogezwe mbele, baada ya ile ya zamani ya ukosefu wa fedha kuonekana haina nguvu.

Gazeti hili limeambiwa kwamba baada ya viongozi wa CCM sasa kudai kwamba kuna matatizo ya kifedha, Magufuli mwenyewe ameamua kubeba mzigo wa kuhakikisha fedha zinapatikana kufanikisha hilo.

Mkutano huo unaweza kufanyika baada ya Bunge la Bajeti kumaliza mkutano wake mjini Dodoma mwishoni mwa mwezi huu ili kuwezesha wale watakaokuwa Dodoma kutohangaishwa kurejea makwao na kisha Dodoma tena kwenye mkutano huo.

Alipoulizwa na Raia Mwema kuhusu kama Magufuli amekubali kubeba mzigo wa kutafuta fedha za Mkutano Mkuu huo wa CCM na mambo mengine yanayohusu Uenyekiti wa CCM, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa, alisema hana mamlaka ya kuzungumzia mambo ya chama.

“ Mambo ya CCM mimi yako nje ya uwezo wangu. Siwezi kukujibu ndugu yangu naomba tu uwaulize wenyewe kwa vile mimi niko serikalini na kwenye chama wana watu wao”, alisema.
Juhudi za kumpata Msemaji wa CCM, Christopher ole Sendeka, kuzungumza kuhusu suala hili hazikufanikiwa hadi tunakwenda mitamboni kwa vile ofisini kwake alielezwa kuwa yuko safarini kwenye mikoa ya Kusini na simu yake ilikuwa haipatikani.

LIPUMBA AMWOMBA MAALIM SEIF AREJEE CUF




Mwenyekiti wa zamani wa CUF,Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa amemwandikia Katibu Mkuu wa chama hicho barua ya kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu Uenyekiti wa CUF.

Sasa anasubiri majibu toka kwa Katibu Mkuu, Maalim Seif baada ya ombi lake kujadiliwa na ngazi za juu za kichama.

Pia amesema Bajeti ya mwaka wa Fedha 2016/17 yenye thamani ya zaidi ya Trilioni 29.5 haiendani na uhalisia

UMEMPATA “SUGAR DADDY” ANAKULIPIA KODI? HIZI NI SHERIA LAZIMA UZIFUATE!!




Kumekuwa na mikasa kwa Wanaume ambao wanalipiwa kodi na Wapenzi wao wakike kwamba ni mabwege au watoto wa mama kama wengi walivyozoea kuwaita. Lakini kwa upande mwingine kuna wale Wanawake ambao japo sio kwamba hawana kipato kabisa ila wanaamini kuwa wakimpata “Sugar Dady au Sponsor” wa kuwalipia kodi basi fedha yao kidogo waliyonayo wanaweza kuitumia kwenye masuala yao ya Urembo.

Kitu ambacho wanawake hawa wanapaswa kujua ni kuwa, mwanaume anapokulipia kodi kuna sheria au taratibu ambazo aidha kwa kujua au kuto kujua lazima uzifuate. Sheria au taratibu hizo ni hizi;-

Moja, tayari una mahusiano na huyo anayekulipia kodi. Haiwezekani mwanaume akulipie wewe kodi alafu kila siku wewe upo na wanaume wengine labda kama huyo mwanaume ni baba yako mzazi

Pili, mwanaume akikulipia kodi anakuwa na kauli/maamuzi ndani ya nyumba. Akija ataweza anza na kuulizia chakula, yani kama hamna anamaanisha ukapike. Na kwavile wewe ndio unamtegemea basi utakuwa huna namna bali kutimiza anachotaka.

Tatu ni kwamba kiuhalisia hiyo nyumba ni yakwake, sababu anamiliki funguo pia. Na kitendo cha yeye kuwa na funguo inamaanisha kuwa hana haja ya kukupigia simu kuwa anakuja sababu ni kwake. Mtu hana haja ya kupiga simu kwamba anaenda kwake. Anaweza kuja muda wowote atakao. Unaweza ukabadilisha baadhi ya vitu ndani kama vile rangi ya mapazia, ukaweka kapeti jipya ila ni kwake pia.


Nne, kutakuwa na sehemu au kiti maalum ambacho atakuwa anakaa kila mara awapo nyumbani. Na watu wengine walioko nyumbani hawatakuwa wakikaa hilo eneo. Sio kwamba eneo hilo limeandikwa jina hapana, na hiyo ni ishara ya power ndani ya familia. Hii hata zamani ilikuwapo.

Tano hutaweza kuwa kila ukikaa nae basi unaanza kuzungumzia marafiki zako wa kiume, mara ooh mimi na John tumekuwa marafiki kwa muda, Oh John kafanya hiki kafanya kile,hakuna mwanaume anakulipia kodi wewe uje uwafurahishe rafiki zako kwenye nyumba. Tena ukitaka kutoka out na marafiki lazima uombe ruhusa. Kama unaona masharti huwezi get up and pay your rent vinginevyo sharti ndio hilo.

Sita ni kuwa hakuna mwanaume anakulipia kodi kama anajitolea au msaada, kila mtu kuna anategemea faida mwisho wa siku na faida ni kama kufanya mapenzi na mengine. Hapo hana tofauti na mtu ambaye amaewekeza kwenye mradi wake anakaa kusubiria mrejesho. Ukweli ni kuwa ukilipiwa kodi unauza uhuru wako, kinyume chake ni kuwa kama unataka uhuru wako basi lipa kodi yako.

Ila ukweli ni kuwa katika zoezi zima hili la kutegemeana mwisho wa siku kila mmoja anafanikiwa lengo lake. Mwanaume anapata mrejesho wa uwekezaji wake na mwanamke anaweza kununu wigi jipya.

OSAMA BIN LADEN YUPO HAI NA ANAISHI MAISHA YA KIFAHARI- SNOWDEN,ANALIPWA MILLIONI MIA MBILI ISHIRINI ZA TANZANIA





Mmoja wa wapuliza filimbi katika taasisi ya ulinzi wa taifa la Moscow Edward Snowden, ameeleza kuwa anamilki nyaraka za siri zinazoonyesha kuwa Osama Bin Laden yupo hai.

Snowden, ambaye anaishi kama mkimbizi nchini Russia ameeleza taarifa hizo ambazo hazijaweza kuthibitishwa kuhusu gaidi Osama Bin Laden alipokuwa akifanya mahonjiano na jarida la Moscow.

Edward Snowden anayeelza kuwa ana nyaraka zinazoonyesha kuwa Osama Bin Laden yupo hai.

Amesema kwamba, sio kwamba Osama yupo hai tu, bali anaishi maisha ya kifahari Bahamas. “Nina nyaraka zinazoonyesha kuwa Bin Laden bado yupo kwenye mfumo wa malipo wa CIA. Osama anapokea zaidi ya dola 100,000 kwa mwezi, ambazo zimekuwa zikisafirishwa na wafanyabiashara wakubwa na mashirika moja kwa moja kwenda kwenye akaunti yake ya benki ya Nassau.”

Snowden aeleza kuwa shirika la kijasusi la Marekani (CIA) lilidanyanga kuhusu kifo cha kiongozi wa zamani wa Al Qaeda, wakati ukweli ni kuwa alisafirishwa kwa siri katika eneo ambalo halikutajwa Bahamas.

“CIA kwa kushirikiana na usalama wa taifa wa Pakistani waliidanganya dunia kuhusu kifo cha Osama. Kwa vile kila mtu aliamini kuwa amekufa, hakuna aliyehangaika kumtafuta, hivyo ilikuwa rahisi kwake kujificha. Bila ndevu (mzuzu) na koti la kijeshi, hakuna mtu anaweza kumfahamu” alieleza Snowden.

Osama Bin Laden ambaye alisemekana kuuawa na Jeshi la Majini la Marekani mnamp 2 Mei 2011 imeelezwa kuwa yupo hai na anaishi maisha ya kufahari.

Alieleza kuwa, nyaraka zinazoonyesha kuwa Osama yuko hai, ataziweka wazi katika kitabu chake kipya kinachotarajiwa kutoka mwezi wa tisa mwaka huu.

Edward Snowden alikuwa muajiriwa wa NSA mwaka 2013 baada ya kuwa alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Dell na CIA. Mwezi wa sita mwaka huo alitoa nyaraka za siri za NSA kwa waandishi wa habari. Serikali ya Marekani ilimfunguliwa mashtaka baada ya kitendo hicho. Sasa amepewa hifadhi (asylum) nchni Moscow baada ya kutoroka Marekani kwa kosa la kuvujisha siri.

HUJAFA HUJAUMBIKA, NA USITUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO:BARUA YA WAZI KWA RAFIKI YAKO WEWE RAFIKI YANGU



Mwanzoni nilidhani ni utani, ila mpaka nilipokuja kuiona picha ukiwa ndani ya shela na tabasamu kubwa lisilo hata na tone la huzuni moyo wangu uliumia sana. Nikaanza kutafakari toka mbali kwa niliyoyaona na kuyajua mwenyewe achana na yale ambayo nilikuja kusimuliwa, kwa sababu safari ya urafiki wenu imetoka mbali sana ni zaidi ya miaka 11 hivi tangu mlipofahamiana. Nakumbuka mara ya kwanza nakutana na rafiki yako mpenzi, alinisimulia mambo mengi mazuri na yenye kutia moyo.

Ambayo kwa kiasi kikubwa yalinishawishi hata mimi kuitwa mume. Nakumbuka tulisheherekea vizuri sana siku ile ya harusi yangu kwa furaha kubwa na uhakika usiokuwa na chembe ya kwamba hichi ninachokiona kitakuja kutokea. Nikawakabidhi kijiti mlikuwa wawili wewe na rafiki yako wa siku nyingi na pia alikuwepo rafiki yangu mwingine kupitia mke wangu ambao wao kwa heshima kubwa walitimiza ahadi waliyokuwa wameniahidi siku ile ya ndoa yangu. Ila wewe sijui ni nini kilitokea mpaka yakatokea haya. 

Katika hili lililotokea kwako naungana na ule msemo unaosema historia haidanganyi, ni kweli historia haidanganyi. Waliokutangulia ndani ya ukoo wenu walishayafanya haya uliyoyafanya wewe. Aliyekutangulia aliacha mume bora, akaolewa na bora mume mwingine kwa sababu ya land Rover ya enzi za mwalimu. Baada ya miaka kadhaa nadhani wewe ni shaidi hivi ile land Rover bado ipo? Vipi kuhusu yule kaka ambae ukoo mlimuona kajamba nani leo je mafanikio aliyoyapata yanalingana na unabii wenu, wa kibinadamu unaoona leo wala hauyajui ya kesho? 

Nayasema haya yote mpaka kurejea mifano hai kutokana na sababu ambayo familia waliitoa kumuhusu rafiki yako mpenzi. Aliyejitoa kwa kila kitu kwa ajili yako kuhakikisha tu unapata yote uliyohitaji, yeye akiamini kuwa hakuna hasara yeyote kumsaidia mke wake mtarajiwa. Kumbe rafiki yako huyu alikuwa anajipatia matumaini hewa ambayo hayapo. Nilijaribu sana kukushauri nini ufanye pale uliponiletea malalamiko kuhusu changamoto uliyokuwa unapitia nikiamini kuwa ulikuwa ni mwanamke shupavu unaeweza kusimama kutetea haki yako. 

Masikini mimi nilishindwa kutambua kuwa kumbe tayari ulishakutana na mwajiriwa wa serikali. Mwalimu wa sekondari ambae wazazi wako walikuwa wanamtaka kisa tu ana ajira ya serikari. Walimkataa rafiki yako wa siku nyingi eti kisa yeye si mwajiriwa wa serikari, ni mwajiriwa wa secta binafsi, hivyo muda wowote anaweza kufukuzwa kazi hivyo akageuka kuwa tegemezi kwako. 

Inasikitisha sana hii binadamu kugeuka kuwa ni watabiri wa maisha ya watu. Kinachonisikisha zaidi ni kuwa umeolewa na mtu usiyempenda kwa shinikizo la wazazi ila si kwa mtakwa yako. Hili maana yake nini? Maana yake ni kuwa hautakuwa na furaha na huyo mume. Kwa kuwa nafahamu hilo na wewe pia unalijua hilo, na hii dhuruma kubwa uliyomtendea rafiki yako wa siku nyingi itakuandama na kukutafuna maisha yako yote. Ipo siku utakuja kuwalaani wote waliosababisha ukaingia kwenye mkataba ambao haukuridhia kutoka moyoni. Waliokushawishi wao kwa sasa ni furaha tupu kwasababu masilahi yao wanayotegemea kuyapata na ambayo kiuharisia hawatayapata wamefanikiwa kuyalinda. Huyu rafiki yako wa siku nyingi yeye kwa sasa Ninachomshauri ni kuwa, akuchukulie kama amekupoteza katika ajari mbaya iliyowakumba, na wewe ukapoteza maisha. Hivyo hana budi kukusahau na kuzoea na hata wewe nakushauri pia umchukulie hivyo hivyo. Ingawa najua huwezi kumchukulia hivyo kwa kuwa umemtenda yasiyostahili. Mwenzako amekutendea mema wewe umemlipa mabaya. Ninayo mengi sana ya kukwambia kuhusu uchungu na masikitiko yangu. Ila najisikia nimechoka kuandika ngoja nipumzike. Ili nisiendelee kukuchosha kwa upuuzi wa masikitiko yangu nakutakia honey moon njema nitakutumia kumbukumbu zetu enzi zile za furaha yenu na yetu pia tulipokuwa na matumaini hewa juu yako.

JE! MAFANIKIO YAKO KIFEDHA YANA MATATIZO?SOMA HAPA


Mwaka 1997 tulipokea barua na simu nyingi toka kwa watu wa Mungu mbalimbali wakihitaji maombi kwa ajili ya matatizo yaliyokuwa yanawasumbua katika maeneo ya kifedha. Wengine biashara na kazi zao vilikuwa haviendi vizuri - nakadhalika.
Tulikaa na jambo hili katika maombi. Tarehe 24 Septemba 1997 saa kumi na nusu asubuhi tukiwa katika maombi Bwana Yesu alisema nasi katika mioyo yetu ujumbe ufuatao ambao tunaamini utakusaidia hata wewe. Bwana Yesu alituambia hivi:


roho ya mpinga Kristo ndiyo iliyoshambulia mafanikio ya kifedha katika watu wangu,

Imeelekeza mashambulizi katika mafanikio ya roho zao (na nafsi zao) maana nimesema mtafanikiwa katika mambo yote kwa kadri roho zenu zifanikiwavyo,

Kufanikikiwa kwa roho zenu kunategemea kufanikiwa kwa nafsi zenu. Mtafanikiwa katika roho zenu kwa kadri nafsi zenu zifanikiwavyo, na matokeo yataonekana katika mambo yote

Nafsi zenu zifanikiwavyo zinategemea utendaji wenu wa Neno langu. Ikiwa utendaji wenu wa Neno ukiwa hafifu, na kufanikiwa kwa nafsi zenu kunakuwa hafifu. Kufanikiwa kwa nafsi zenu kukuwa hafifu na kufanikiwa kwa roho zenu kunakuwa hafifu, kwa hiyo kufanikiwa katika mambo yote kunakuwa hafifu pia.

Ndiyo maana nasema roho ya mpinga Kristo imeelekeza mashambulizi yake katika kupinga, kuzuia, na kuchelewesha mafanikio yenu katika roho na nafsi zenu.

Lakini mnaweza kushinda kwa kusimama katika Neno langu ambalo ni upanga wa Roho mikononi mwenu.

Nimesema katika Yoshua 1:8 ya kuwa mtafanikiwa ikiwa mambo matatu yatafanyika juu ya Neno langu:
(a) Lisiondoke kinywani mwenu 
(b) Mlitafakari wakati wote
(c) Na kudumu kulitenda

Sasa angalia mmesimamaje katika maeneo hayo matatu. Maana hizo ni mbinu za kulitumia Neno langu kama silaha ya kumshinda adui

Mkisimama katika Neno langu ninavyotaka mtavuna mafanikio sana kwa wakati wangu msipozimia na kukata tamaa katika mioyo yenu.

roho ya mpinga Kristo inawakatisha tamaa kwa kuwaangaliza matokeo ya upungufu mlionao badala ya kuangalia ahadi zangu na matokeo yake.

Kwa kadri mnavyoangalia matokeo ya upungufu mlionao, ndivyo mnavyozidi kutafakari juu ya upungufu mlionao. Kwa kadri mnavyozidi kutafakari juu ya upungufu mlionao, ndivyo mnavyozidi kukiri na kushuhudia upungufu mlionao na matokeo yake.

Kumbuka mnayafunga mafanikio yenu kwa maneno ya vinywa vyenu yanayotoka katika nafsi zisizotafakari ahadi zangu na matokeo yake.

Mimi si mtu hata niseme uongo. Nililolisema katika Neno langu nimesema nitalitimiliza. Napenda kufanikiwa kwenu kuliko nyinyi mnavyopenda kufanikiwa kwa watoto wenu. Msikubali adui ayumbishe macho yenu na mioyo yenu isione uaminifu wangu.

Mkisimama katika neno langu na kupigana hivyo vita vizuri vya imani mlivyo navyo;
- mtashangilia ushindi wakati kuta hazijaanguka bado,
- mtatangaza ushindi wakati bado upinzani wa adui umesimama,
- mtaona mafanikio wakati bado mmezungukwa na upungufu,

Kumbuka neno langu linatangaza ushindi katika roho kwanza kabla ya haujaonekana kwa nje. Ndicho kilimchomsaidia Ibrahimu wakati anasubiri mtoto wake. Na ndicho kilichonisaidia na mimi pale masalabani - nilishangilia ushindi dhidi ya adui hata kabla sijafufuka. Daudi naye aliuona ushindi wakati bado Goliati amesimama mbele yake.

Kila mtu atakuja kwangu na kuuliza nimpe Neno la kusimamia katika vita alivyo nayo. Hamuwezi kushinda pasipo Neno.

Haya ndiyo machache tuliyoyapokea kutoka kwa Bwana Yesu tulipofanya maombi ya kuuliza kwa nini watu wengi wa Mungu wamekuwa hawafanikiwi vizuri katika eneo la fedha. Ingawa Bwana alisema nasi mwaka 1997 tunaamini bado ujumbe una nguvu ndani yake ya kukusaidia. Tafakari maneno ya ujumbe huu, weka katika matendo yaliyomo - na Mungu atakusaidia!

Ahsante,
Mwl. Christopher Mwakasege

Sunday, 12 June 2016

MAMBO YA KUTAFAKARI KABLA YA KUFANYAUAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA



Jambo la kwanza: Kuoa au kuolewa kunabadilisha uhusianowako na wazazi wako.
Mwanzo.2:24 anasema, “Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili moja”. Ukiangalia (Zaburi.45:10-11) anasema, “Sikia binti utazame (maana yake anazungumza na msichana) utege sikio lako. Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako na mfalme atautamani uzuri wako, maana ndiye bwana wako naye umsujudie”.
Najua watu wengi sana wanataka waingie kwenye ndoa, waoe au waolewe, lakini uhusiano wao na wazazi wao usibadilike, haiwezekani. Biblia imeweka wazi kabisa, unataka kuoa, mwanamume lazima kwanza aachane na baba yake na mama yake, maana yake kuna mabadiliko. Kuna mabadiliko mahali pakuishi, kuna mabadiliko juu ya mtazamo wako wa kwanza wa maisha yako. Mke wako hawezi kuwa mama yako, na mume wako hawezi kuwa baba yako. Mke wako anakuwa mke wako na si mama yako. Mume wako anakuwa mume wako na si baba yako.
Na kabla hujafikia maamuzi ya namna hiyo - ukiingia kwenye ndoa, ndoa yako itakuwa ngumu. Maana inawezekana unaishi vizuri na wazazi wako, kiasi ambacho maamuzi yako yoyote unayofanya lazima ushirikiane nao, na hiyo ni hatua nzuri kabisa. Lakini ukiishaingia kwenye ndoa, mtu wa kwanza wakushirikiana naye ni mke wako kama umeoa, na ni mume wako kama umeolewa lakini, sio baba yako, sio mama yako.
Na wazazi wengine wasingetaka kuona kwamba unakuwa mbali nao kwa jinsi hii, wanataka waendeleze maamuzi yao na utawala wao waliokuwa nao juu yako mpaka kwenye ndoa yako, haiwezekani. Biblia inakataa. Sasa ukisoma ile Mwanzo unaweza ukafikiri ni wanaume tu wakioa ndio wanatakiwa watoke, waachane na wazazi wao, lakini Zaburi 45:10,11 inatuambia wazi kabisa, inasema, “Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako. Naye Mfalme atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie”.
Sasa haimaanishi usiwasalimie, haimanishi usiwasaidie, lakini ningekuwa nazungumza kwa kiingereza ningekuambia, “your priorities must change” lazima ubadilike jinsi ambavyo unaweka kipaumbele katika watu ulio nao.
Unapoamua kuolewa, wa kwanza sio baba yako wala sio mama yako, wa kwanza ni mume wako baada ya Yesu. Katika mahusiano ya kibinadamu anayekuja pale wa kwanza baada ya Yesu moyoni mwako ni mume wako. Ikiwa hujafikia maamuzi ya namna hii moyoni mwako basi bado hujafikia utayari wa kuolewa. Na ina madhara yake magumu. Maana biblia inasema, kabla hujawasahau watu wako na watu wa nyumba ya baba yako, mume wako hawezi kuutamani uzuri wako, ukitaka autamani uzuri wako lazima uwasahau kwanza watu wa nyumbani kwa wazazi wako.
Sasa kuna tofauti ya kupenda na kutamani. Kabla hujaolewa au kabla hujaoa huruhusiwi kutamani. Lakini ukiisha oa unaruhusiwa kutamani lakini mke wako tu. Ukiishaoa kutamani mke wako ruksa, na biblia imeweka vizuri kabisa, na ukiishaolewa kutamani mume wako ni ruksa. Lakini biblia imeweka utaratibu wa ajabu sana kwamba, ili mume amtamani mke wake, lazima mke wake awasahau kwanza watu wa nyumbani mwa wazazi wake. Hiki ni kigezo kigumu sana.
Ndio maana unaweza ukakuta mtu ana mke mzuri sana lakini hamtamani. Unaweza ukafikiri labda ni kwa kuwa hajajipamba vizuri; lakini hata kama atajipamba, atajikwatua kuanzia asubuhi mpaka jioni, - anaweza hata akatumia muda mwingi kwenye kioo kuliko kwenye maombi akijitengeneza, lakini bado mume wake asimtamani; kwa nini? Kwa sababu ndani yake hajaachia watu wa nyumba ya wazazi wake. Au watu wa nyumba ya baba yake wana nafasi kubwa moyoni kuliko mume wake.
Ni mabadiliko ambayo lazima uyatarajie, watu wengi sana huwa hawafikirii hayo, wanafikiri ni kitu rahisi. Unaweza sasa ukaelewa kwa nini watu wengine ikifika siku ile ya “send off”, yaani ya kum’send’ msichana ‘off’ asikae tena nyumbani kwa baba yake, hiyo siku ni ngumu sana kwa wazazi. Kwa sababu wanajua, wanaagana na msichana wao, mahusiano yao waliokuwa nayo toka mwanzoni, tangu alipozaliwa, alipokuwa tumboni mpaka wakati huo yanabadilishwa, yanajengwa mengine, sasa anakwenda kuwa mke wa mtu, hawawezi tena kuingilia maamuzi juu yake, amefunga agano mahali pengine.
Unakuta siku hiyo wazazi wengine wanalia, unakuta vijana wengine wanalia, wasichana wengine wanalia. Usije ukafikiri ni kitu rahisi. Ndani ya nafsi kuna vitu vinaachana, kati ya wazazi na wale watoto wanaoana.

Mwl.Mwakasege

JIHADHARI NA MATARJIO POTOFU KUHUSU NDOA

Leo tutazungumzia kipengele muhimu cha Kujihadhari na matarajio potofu kuhusu Ndoa, au yaliyojengwa kuhusu Ndoa.

Matarajio potofu ni ile hali ya kuamini kwamba kuna vitu fulani vitatokea au vitakuwa hivi halafu wala havitatokea na wala haviko hivyo unavyotarajia.

Matarajio potofu kuhusu ndoa yako sana katika jamii zetu sio za Kiafrika tu hata mabara ya Ulaya, yako katika jamii za dini mbalimbali, kabila na mila mbalimbali

Najua hata wewe kuna matarajio potofu kuhusu Ndoa ambayo utakuwa umeyaamini kwasababu ulizaliwa katika jamii ambayo yaligeuka kuwa sehemu ya hiyo jamii. 

Katika jamii zetu na mazingira yanayotuzunguka matarajio potofu yanaweza kuwa na sehemu kubwa inayofanya Ndoa nyingi ziwe katika shida ambazo zimekuwa nazo leo.

Kitu kibaya ni kwamba hata sisi Wakristo tumeyaamini na tunayakiri maratajio hayo matarijio potofu, ndio maana leo nimekuja kukuambia kwamba hayo ni potofu labda ulikuwa hujui.

Tuangalie Aina Tano za Matarajio Potofu kuhusu Ndoa;

1. Ndoa Ndoano au Ndoa si Lelemama

Mara nyingi kwenye sherehe mbalimbali za Harusi utakuta pande mbili ya Bibi Harusi na Bwana Harusi wanapewa nafasi ya kutoa nasaha sasa hapo ndio utasikia haya maneno yakisemwa katika nasaha na tena cha kushangaza utakuta watu ukumbini wananapiga makofi.
Sasa wewe mzazi au mlezi mwenzangu unaposubiri ile sherehe pale ndio uje kumwambia mtoto Ndoa si Lelemama au Ndoa ni Ndoano kwanini umechelewa si ungemkataza au ungekataa mahari jamani, Ili basi kumuepusha na hiyo lelemama unafikiri ipo.

Maana kwa kusema pale ina maana unakiri kabisa kwa mdomo wako Mwanangu Ndoa Ndoano au si Lelemama kwahiyo ukavumilie, pale unamfanya huyo mratajiwa awe na hofu kubwa kwahiyo atakaa kimtegomtego ili tu akiona tu kaugomvi kidogo anakumbukaa anhaa hii ndio ileee lelemama niliambiwa na baba au mama siku ile pale Kibada Skyline Hall…Ohh mwisho wa siku anaanza tu kuhesabu makosa siku anakurudia na mizigo ooh Baba na Mama ile Lelemama yangu anhaa hukuwahi kuiona imekuwa lelemama kwelikweli Nimeshindwa na Nimerudi, Utajibu nini mzazi mwenzangu au mlezi mwenzangu.

Haimaanishi kwamba kama wewe mzazi au mlezi ulipata shida katika Ndoa yako na mtoto wako lazima apitie ulichopita, hata kidogo , na jaribu ulilopitia je umetafuta Kusudi maana nimejifunza kila Jaribu ulilopitia katika maisha lina kusudi sasa kwasababu tunashikilia sana Uchungu inakuwa Ngumu kuliona Lile Kusudi ambalo ndilo hasa Mungu anataka tulifanye, Haleluyaaaaaaaaa

Sasa na wewe kijana au binti haya na wewe hata hujaolewa unaanza kukaa barazani ooh unajua Bwana wanaume siku hizi wasanii tuu Ndoa hamna, hakuna zote Ndoa Ndoano, unajua kinachotokea katika Ulimwengu wa Roho, tusome pamoja Mithali 18: 21 “Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.”

Haya kijana na Binti yangu umeona Maneno ya Mungu yanavyosema,kuwa makini unaongea nini wewe ni mtoto wa Mfalme wa Wafalme usiishi kama watu wa mataifa ambao hawana Tumaini,badili Maneno ya Kinywa chako leo, Sema mimi ndoa yangu itakuwa nzuri itabariki watu, itasimama kama Ushuhuda na utapata hicho unachokisema.






2. Ndoa ni 50/50

Hapa wanamaanisha usijitoe mzima mzima kwenye Ndoa, mwenzako asije akakujua sanaa. Hayo ni maneno tena hata wazazi wanafundisha watoto wao hivyo.

Unajua Mungu anataka moyo safi,Ndoa ili iwe Ndoa nakwambia ni kujitoa 100/100 asilimia katika maeneo ya kifikira, kimwili na kiakili nakadhalika.

Ukikaa nusu nusu na ndoa yetu ya Kikriso ni ya milele yaani kifo tu ndio kinatenganisha si utaumia sana mpendwa wangu maana utaishi maisha fake maisha yako yote.

Mungu ndio alianzisha Ndoa na kama Mungu ndio mwanzilishi alijua tu kwamba itakuwa nzuri ila tufuate kanuni zake, kila siku kujikana na kuhakikisha uko katika mstari Mungu anaotaka



3. Ndoa ni sehemu ya kupunguzia matatizo

Wengine wameoa au wameolewa ili kupunguza matatizo waliokuwa nayo kabla, labda mmoja ana kipato kidogo sasa anajua akiolewa na mwenye kipato kikubwa atakuwa amepata suluhisho,

Nakwambia ni kosa kubwa kuolewa na mtazamo huo, kwasababu kama ni hivyo matatizo yako yatazidi mara mia maana sasa unaweza kukuta mwenzako labda ana vitu vingine anavipa kipaumbele na sio kutapanya hela kama ulivyofikiri, maana mwingine anaolewa au kuoa anafikiri kila wiki atakuwa anapelekwa Sychells au Dubai kumbe mwenzako ana malengo mengine ya maendeleo, sasa hapo unajikuta unakuwa frustrated ooh hanipendi , kumbe wewe ndio unatakiwa kujua ndoa si sehemu ya kusolve matatizo yako ila inabidi ubadilike ili uweze kuishi vizuri na mwenzako, Halleluyaaa, Bado mnanipenda kweli jamani……..



4. Mwanamke aliyesoma sana hafai kuwa mke

Nimekutana na hili swali mara nyingi jamani mama mimi nina Masters au PHD nitaolewa kweli, ni kutokana na jamii ambavyo imetufanya tuone kwamba sio sahihi.

Wengine wanasema ukitaka kuoa Bwana nenda zako kijijini wakutafutie mchumba mwenye elimu ya chini sana au hana kabisa ili niweze kumtawala hawa wasomi wana maswali sana sitawaweza,nani kakuambia Ndugu yangu wewe unafuata kanuni gani ya Ndoa ya Dunia inavyosema au Mungu. Je hujui kama unaweza kumchukua wa kijijini akitakata tuu anakuwa tatizo mpaka unajuta, achana na hilo tarajio potofu kama Mungu amekukutanisha na mdada ana PHD au Masters yeye Mungu huyohuyo atampa huyo dada hekima ya kuishi na wewe na wewe hivyohivyo.

Ukimuamini Mungu kwamba yeye ndio anakupa wa kufanana nae na ukaamini kabisa kwamba huyu amefanana nami chochote alicho nacho hakimkoseshi sifa za kuwa mke, huo mtazamo utafanya uwe na Ndoa yenye Amani sana.

5. Kuishi pamoja, kinyumba kwanza ili kuona kama tunaendana

Eti kuna mtu ameniambia kwamba siku hizi kuna mtindo umeibuka Bwana, watu kwasababu wanajua Ndoa ni Lelemama ni Ndoano basi wamevumbua njia zao wenyewe kwamba sasa ili kumsoma mwenzangu kama anafaa kunioa au kumuoa nitest kuishi naye, yaani hiyo ni ajabu na kweli.
Hiyo si sawa kabisa maana nikipekua Biblia yangu sioni popote kinyumba kimeruhusiwa na Mungu, lazima tufuate manual ya aliyetuumba ili tuwe salama.
Ndoa ni mpango Kamili wa Mungu ukiingia ujue uko katika mpango wake uache hofu na Mashaka, uwe na Imani kwasababu maisha yetu ya Ukiristo ni maisha ya Imani.

Amini kwamba ukiingia katika Ndoa utashinda majaribu yooote maana kwakweli lazima yaje, wala siko mahali hapa kukuambia kwamba Majaribu hayatakuja yatakuja mpendwa wangu ila kama Neno linavyosema katika Warumi 8 : 37 ”Lakini katika mambo yote haya sisi ni washi ndi, naam, na zaidi ya washindi, tukiwa ndani yake yeye aliyetu penda.”TUJUE UTASHINDA NA UTAKUWA NA NDOA YENYE USHUHUDA.

Na Dr.Mosses Kulola


SOMO KUU SIKU YA LEO; USIYAONE MATATIZO YA KIUCHUMI KAMA KIKWAZO KWAKO



Shalom,

Tunajua unataka uwe na uchumi mzuri. Hii ni kwa mwanadamu yeyote bila kujali mahali alipo,awe anafanya kazi au hata kama hafanyi kazi.
Kuanzia leo na siku kadhaa zitakazofuata,tutajitahidi kukushirikisha misingi kadhaa iliyomo katika biblia,ambayo tunaamini itakusaidia uwe na uchumi mzuri. Msingi wa kwanza ni huu:Badilika unavyoamini juu ya uchumi,utabadilika unvyosema juu ya uchumi,na hali yako ya uchumi itabadilika vivyo hivyo.
Tunaamini ya kuwa; mtu akibadilika anavyoamini atabadilika pia anavyosema;na hali yake ya maisha itabadilika vivyo hivyo.
Jambo hili tunalipata tunaposoma kitabu cha Mithali 23:7 ya kuwa; “Maana aonavyo nafsini mwake,ndivyo alivyo.”
Tafsiri nyingine ya mstari huu inasema;”maana awazavyo nafsini mwake ndivyo alivyo.” Tasfiri nyingine ya mstari huu inasema;”maana aaminivyo nafsini mwake,ndivyo alivyo.” Mstari huu unataka tujue ya kuwa maisha ya mtu alivyo ni matokeo ya awazavyo au aaminivyo au afikirivyo(mindset), nafsini mwake.
Ulivyo kimaisha kwa nje ni matokeo ya msimamo wako wa kimawazo ndani yako. Kwa ulivyo kiuchumi,ni matokeo ya msimamo wako kimawazo(mindset),ulionao ndani yako juu ya uchumi.
Wapelelezi 10 walileta habari mbaya walipotoka kuipeleleza Kaanani,kwa vile waliamini mioyoni mwao ya kuwa “majitu” waliyoyakuta Kaanani yalikuwa kikwazo na pingamizi kwao.Wapelelezi wawili (Yoshua na Kalebu),waliona hayo “majitu” pia lakini mioyoni mwao waliamini tofauti. hawakuyaona majitu kama kikwazo bali waliyaona kama fursa kwao ya kutatua tatizo hilo ili waweze kula.
Soma habari hii katika kitabu cha hesabu 13:32,33 na Hesabu 14:9,28
Matokeo ya tofauti hizo kuwaza na kuamini,kuliamua hatma ya baadaye ya uchumi na maisha yao.Wapelelezi 10 waliishia kulalamika na kushindwa kwenda Kaanani. Na wale wawili (Yoshua na Kalebu) waliweza kwenda Kaanani na wakawa na maisha mazuri.
Wazo tunalokufikirisha siku hii ya leo ni kwamba;Usiyaone matatizo ya kiuchumi yanayokuzunguka kama kikwazo,bali yaone fursa ya kuyatatua ili iwe njia mojawapo ya kuongeza kipato chako. Kumbuka wanaolalamika wanapoona matatizo,wanajipofusha fikra szao wasiona fursa za kimaendeleo katika matatizo hayo.
Mungu awabariki.
Mwl.Christopher Mwakasege

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...