Friday, 24 November 2017

JIFUNZE AINA ZA NGIRI NA MATIBABU YAKE


Kuna magonjwa ya hernia ya aina nyingi kama zile ziitwazo kitaalamu inguinal, umbilical, femoral, epigastric, incisional, inguinal hernia na diaphragmatic hernia.
Lakini watu wengi hukumbwa na hernia iitwayo inguinal hernia ambayo hutokeza karibu kabisa na sehemu ya siri ambako hapa kimrija kinachochukua mbegu za kiume kutoka kwenye korodani na kuingia kwenye tumbo na kuingia kwenye kiungo cha kiume.

Hapa panaweza kuwa na uwazi na uwazi huo ukaingia utumbo mdogo na kusababisha hernia hii. Aina hii ya hernia kama nilivyosema hapo juu ndiyo inayosumbua sana watu wengi duniani. Kuna aina nyingine ya hernia inayoweza kutokea kwenye kitovu, sehemu ambayo kunakuwa na mshipa unaopitisha damu yenye chakula na hewasafi ya oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa tumboni.

Sehemu hiyo mtoto anapozaliwa panaweza pasijifunge vizuri, hivyo mtoto huyo kupata hernia hii baadaye kwani utumbo mdogo huingia katika kijinafasi hicho kisichojifunga vizuri, hivyo kusababisha uvimbe wa hernia hii. Lakini tatizo hili ikiwa mtoto amezaliwa na akaishi zaidi ya miaka miwili bila kujitokeza tena, basi atakuwa salama kwa sababu kwa muda huo sehemu hiyo huwa imejifunga kabisa.

TIBA
Ikitokea sehemu hiyo ikaacha kujifunga kwa kipindi hicho cha miaka miwili, basi daktari huamua kumfanyia upasuaji mtoto huyo. Kwa watu wazima hernia kwenye kitovu ambayo kitaalamu huitwa umbilical hernia inaweza ikatokea kwa akina mama wenye mimba au kwa wale ambao ni wanene kupita kiasi kwani presha kwenye tumbo inakuwa kubwa na kufunga sehemu hii ya kitovu ambayo inawezekana awali ilikuwa wazi.

Hernia nyingine huweza kutokea kwenye kiungo cha njia ya kumezea chakula kinapoungana na tumbo. Kama sehemu hii haikufunga vizuri utumbo unaingia kwenye kinafasi hicho na kujitokeza kwenye kimfuko kilichopo kifuani kinachoitwa kitaalamu diaphragm.

Ndiyo maana hernia hii huitwa diaphragm hernia.
Hernia nyingine iitwayo femoral hernia hutokea pale mishipa ya damu iendayo kwenye mguu inapopita kwenye tumbo na ikiwa kwenye maungio pana nafasi basi hernia hii hutokea kwenye paja karibu na kiunoni.

Kuna hernia ingine inayotokea kwenye chembe ya moyo ambapo misuli inaachia na kusababisha kingozi cha tumbo na utumbo kuingia katika sehemu hiyo hivyo kuvimba na kusababisha hernia.

Tiba za uhakika za hernia ni kufanyiwa upasuaji kama tulivyofafanua hapo juu.

======

UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE)
Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji. Ugonjwa huu wa ngiri unawapata wanaume na wanawake wa rika zote. Mshipa wa ngili ni jina linalokusanya magonjwa kama Ngiri kavu (Hernia), Ngiri maji (Hydrocele) na Ngiri nyinginezo kama vile kuvimba kokwa au mfereji unaopitisha manii unaojulikana kitaalamu kama Epididmorchitis.

Ngiri Kavu (Hernia), aina hii ya ngiri huwapata wanawake na wanaume wote kwa ujumla. Ngiri kavu inapompata Mwanamke huitwa Fermoral Hernia, na pindi inapompata mwanaume inaitwa Scrotal hernia. Kwa maana halisi ya ngiri au mshipa wa ngiri ni hali inayotokea katika mwili wa binadamu ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili. Sehemu hiyo inayoathiriwa mara nyingi huwa ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

Pamoja na hivyo mshipa wa ngili hujitokeza sehemu mbalimbali za mwili na hupewa majina tofauti kutokana na sehemu ulipojitokeza, kwa mfano ngiri ya tumbo inajulikana kitaalamu kama Abdominal Hernia, pia watoto wanaozaliwa na vitovu vikubwa inaitwa Umbilical Hernia, na pale ngiri inapojitokeza katika sehemu ya haja kubwa inaitwa Anal Herni. Dalili zake hazitofautiani sana hata hivyo ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote isipokuwa kuna baadhi ya ngili hujitokeza na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza.

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa wa mwili wa kupitiliza au kuongezeka uzito kwa ghafla, pia kua na kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.

Mojawapo ya dalili za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
• Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
• Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.

• Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
• Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.
Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

======

Ugonjwa wa ngiri ya kitovu (Umbilical Hernia)

Hili ni tatizo la kiafya ambalo huathiri ukuta wa tumbo na kitovu. Tatizo hili husababishwa na mambo makubwa matatu; kwanza ni kasoro ya kuzaliwa. Hapa ni kwamba kitovu kinakuwa na kasoro tangu pale mtoto anapokuwa tumboni kabla hajazaliwa.

Tatizo hili kwa watu wazima lipo mara tatu zaidi kwa wanawake ukilinganisha na wanaume ambapo lipo kwa kiasi kidogo sana. Kwa watoto kiwango cha tatizo hili vinalingana kwa wote wa kike na wa kiume na tafiti zinaonesha kwamba, tatizo ni kubwa kwa watoto wa Kiafrika ukilinganisha na mataifa mengine.

Aina ya pili ya tatizo hili ni ngiri ya kitovu. Hii inatokea tu pasipo na kasoro za kuzaliwa nazo. Hili linatokea kutokana na shinikizo la mgandamizo wa hewa na nguvu ndani ya tumbo kunakosababishwa na unene kupita kiasi, kunyanyua mizigo mizito au vitu vizito mara kwa mara, kikohozi cha muda mrefu na ujauzito wa mimba ya mapacha kwa mwanamke.

Aina ya tatu ya ngiri ya kitovu inaitwa ‘Paraumbilical hernia’. Aina hii ya ngiri hutokea zaidi kwa watu wazima na husababishwa na kasoro upande wa juu wa kitovu kuelekea kwa juu kufuata mstari wa kati wa tumbo.

DALILI ZA UGONJWA
Ngiri hutokea katika eneo la kitovu ambacho kwa lugha nyingine huitwa ‘Umbilicus’, ‘navel’ au ‘Belly button’. Kwa watoto wachanga wanapozaliwa kitovu huwa kirefu sana na huungana na kondo la nyuma la mama ili kupeleka lishe na hewa ya oksijeni kwa mtoto anapokuwa tumboni.

Baada tu ya kuzaliwa, mtoto hujitegemea hivyo kitovu hukatwa katika eneo maalum ili kipungue urefu. Baada tu ya kitovu cha mtoto kupona, mtoto anaweza kupatwa na tatizo hili la ngiri ya kitovu tangu anapokuwa mtoto mchanga ambapo akilia kitovu kinatokeza juu na anaponyamaza kinarudi ndani.

Hali hii wakati mwingine humsababisha mtoto apatwe na maumivu makali huku akilia kila wakati.

Aina hii ya ngiri huwa haipasuliwi kwani huisha yenyewe baada ya miaka miwili hadi mitatu, lakini baada ya umri huo kama haikuisha basi mtoto atafanyiwa upasuaji kurekebisha.

Endapo mtoto ngiri hiyo itakuwa inamsumbua kabla ya umri wa miaka mitatu, basi hatapasuliwa bali itafanyiwa utaratibu wa kuirudisha kitaalam ili isiendelee kutokeza na kuleta maumivu. Ngiri inapokuwa kubwa, tundu lake huwa haliongezeki hivyo husababisha matumbo na kila kitu kitachomoza na kubana nje kushindwa kurudi ndani na kusababisha hali iitwayo ‘Strangulation’.

Kama hali hii haitatibiwa mapema basi italazimika upasuaji wa dharura na ikichelewa huweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa. Tatizo hili hutokea hata kwa ngiri nyingine ambazo tutakuja kuziona katika matoleo mengine.

UCHUNGUZI
Ngiri ya kitovu huonekana kwa macho pale inapochomoza ambapo dhahiri itaonesha imechomoza, wakati mwingine mgonjwa atalalamika maumivu na kama ni mtoto atakuwa analia mara kwa mara.

Vipimo vingine vitategemea na daktari kadiri atakavyoona inafaa.

MATIBABU
Matibabu ya ngiri ni kupasuliwa, haishauriwi kufungia sarafu kwani inaweza kukosewa na kusababisha sehemu ya utumbo kubanwa au kuleta maambukizi ya ngozi kwenye kitovu. Kwa mtoto huisha yenyewe taratibu na ikibidi hupasuliwa baada ya umri wa miaka mitatu.

Wakubwa ni lazima ipasuliwe kama inaleta shida. Wahi hospitali ya mkoa kwa uchunguzi na tiba

======

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji (operesheni).


Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni: Kuwa na uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia kuharisha au kuvimbiwa (Constipation). Vitu hivyo pamoja na mtu kuwa na misuli au tishu zilizopoteza uimara au uwazi (opening or hole) humfanya mtu apate ngiri (hernia).

Ngiri hutambuliwa kwa kutokea kitu kama uvimbe au kujaa katika eneo husika (baadhi ya maeneo yametajwa hapo juu) na pia kwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari huwezesha kugundua tatizo hili.

Njia inayoweza kutatua tatizo hili ni kwa mtu mwenye ngiri kufanyiwa upasuaji ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea. Pia kutegemeana na kihatarishi cha tatizo hili, mtu unaweza kuwa unafanya mazoezi ili kupunguza uzito wako na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga mboga au matunda yenye nyuzi nyuzi (fibers), hii itasaidia pia mmeng’enyo (digestion) wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa. Matunda (Vitamin C) husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na pia husaidia kupona haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji (operesheni). 

Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vyema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Thursday, 23 November 2017

HERNIA NI NINI? CHANZO NA TIBA YA HERNIA.




Hernia ni uvimbe (eneo lililotuna) kutokana na viungo vya ndani ya mwili kusukuma kuta za misuli inayozunguka au kushikilia viungo hivyo. Hernia hutokea wakati kuna udhaifu au kuna tundu kwenye kuta za misuli inayoshikilia na kuviweka viungo vya tumbo kwenye sehemu yake (peritoneum). Udhaifu huo unaweza kuviruhusu viungo vya ndani kusukuma na kupenyeza, na kujenga eneo lililotuna. Unaweza kuwa na hernia ikiwa unaweza kuhisi namna ya eneo laini lililotuna kwenye maeneo ya tumbo au kinena au kwenye kovu ambalo lilitokana na upasuaji. Eneo hili lililotuna linaweza likapotea ukiminya sehemu hiyo au ukijilaza. Unaweza kupata maumivu kwenye eneo hilo hasa ukikohoa, ukiinama au ikinyanyua kitu kizito.






Hernia ni tatizo linalowasumbua watu wengi katika nchi nyingi duniani. Hernia mara nyingi hutokea kwenye maeneo ya tumbo, lakini huweza pia kutokea kwenye sehemu ya juu ya mapaja, kwenye kitovu, na kwenye maeneo ya kinena. Hernia haihatarishi maisha mara moja, lakini haiwezi kuondoka yenyewe na inaweza kuhitaji kufanyika kwa upasuaji.

Hernia mara nyingi hupewa majina kutokana na sehemu ya mwili inapojitokeza, ingawa mara nyingine majina huweza kutolewa kutokana na sababu nyingine za kuitambulisha. Kila hernia hutibiwa tofauti na nyingine kutokana na sehemu iliyopo na sababu nyingine za kitaalamu. Kuwa na elimu ya kutosha ya kila aina ya hernia itakusaidia kujua namna ya kutoa maamuzi sahihi ya tiba yake.


Aina Za Hernia

1. Inguinal (groin hernia)

Inguinal hernias au groin hernias hutokea pale utumbo au mafuta yanaposukuma na kupenya kwenye misuli ya eneo la kinena. Hii ndiyo aina ya hernia inayowasumbua watu wengi zaidi. Inguinal hernia inaweza kuonekana kwa wanaume na wanawake lakini huwapata zaidi wanaume kwa sababu tayari wana kijitundu kidogo kwenye misuli ya kinena kwa ajili ya kupitisha arteri, veni na mrija wa mbegu vinavyoelekea kwenye korodani. Asilimia 97 ya aina hii ya hernia huonekana kwa wanaume.






Hernia inaweza kuwa juu ya misuli ya tumbo (direct inguinal hernia) au inaweza ikafuata njia ya mrija wa shahawa pale unapoacha eneo la tumbo na kuelekea kwenye korodani (indirect inguinal hernia). Inguianal hernia huanza kama uvimbe mdogo ambao huongezeka na muda. Uvimbe unaoonekana ni utumbo au mafuta yanayosukuma misuli.






Uvimbe huweza kupotea kwa kulala na kurudi mwili ukianza shughuli. Uvimbe huu ukiwa mkubwa sana, huenea kutoka kwenye kinena hadi kwenye korodani zenyewe. Hernia ikiwa kubwa sana huleta matatizo kuiondoa.

2. Umbilical (belly button hernia)

Belly button hernia au umbilical hernia kama inavyoitwa mara nyingine, ni pale utumbo au mafuta yanapopenya kupitia sehemu dhaifu ya misuli iliyopo katikati ya tumbo chini ya kitovu. Sehemu hii ndiyo inayopata udhaifu mara nyingi kwa sababu ndiyo sehemu inayopata minyumbuko zaidi wakati tukifanya shughuli yo yote ya mwili.

Umbilical hernia inaweza kuwa moja kwa moja chini ya kitovu, lakini wakati mwingine inaweza kuwa juu kidogo au chini kidogo ya kitovu. Inaweza kuonekana kama kijikokoto kidogo chini ya ngozi, au ikikua inaweza kuonekana kama kijimpira cha gofu au hata kufikia kimpira cha tenisi kama kikiachwa bila tiba.



Kwa watoto wa kufikia hadi miaka 5, hernia hii kwa kawaida huondoka yenyewe. lakini kwa watu wazima hernia hii haipungui na huwa inazidi kuwa kubwa kila wakati. Wanawake kwa kawaida hupata umbilical hernia wakati wa ujauzito, na hupotea yenyewe baada ya kujifungua. Kwa baadhi ya wanawake, kijishimo hiki katika musuli hubakia baada ya kujifungua. Inashauriwa kuwa wanawake wasubiri kwa miezi 3-6 kuona kama hernia hii itafunga yenyewe.

Kama ilivyo kwa hernia nyingine, dalili za kawaida ni maumivu kwenye kitovu. Kutokana na mafuta au misuli kupita kwenye hernia hii, uvimbe utaonekana chini ya ngozi kwenye eneo hilo. Baada ya muda, kama hernia itakuwa kubwa sana, utumbo unaweza kunaswa kwenye hernia hiyo na kuleta madhara kwenye utumbo, vikiambatana na kichefuchefu, kutapika, na kufunga choo.

Kwa sababu hakuna hernia inayopona yenyewe, upasuaji unahitajika. Njia inayopendekezwa hapa ni open surgery kwa sababu tundu ni dogo.
3. Femoral (below the groin)
4. Epigastric (just below the breast bone)
5. Ventral (above the umbilicus)
6. Incisional (through a prior surgery site)
7. Sports


Namna nyingine za kuelezea Hernia:

1. Recurrent (after a prior hernia repair)
2. Unilateral (one side of the body)
3. Bilateral (both sides of the body)


Sababu Za Hernia

Ukiondoa hernia inayotokana na upasuaji wa awali, mara nyingi hakuna sababu inayoeleweka ya kusababisha hernia. Watu walio kwenye hatari zaidi ya kupata hernia ni wenye umri mkubwa, na wanaume wapo kwenye hatari zaidi kuliko wanawake.

Hernia inaweza kujitokeza mtoto anapozaliwa au kwa watoto waliozaliwa na dosari kwenye kuta za matumbo yao.

Shughuli au madawa yanayosababisha mgandamizo kwenye kuta za tumbo vinaweza kusababisha hernia. Vitu hivi ni pamoja na:

. Kujikamau kwa nguvu wakati wa haja kubwa kutokana na choo kuwa kigumu
. Kikozi cha mara kwa mara
. Kuwa na tatizo la cystic fibrosis
. Kuvimba kwa tezi dume
. Unene wa kupindukia
. Kukojoa kwa shida
. Kunyanyua vitu vizito
. Maji tumboni
. Lishe duni
. uvutaji wa tumbaku
. Korodani zisizoshuka
. Uchovu wa mwili


Dalili Za Hernia

Mara nyingi, hernia ni uvimbe unaoonekana usio na mauvimu na usiohitaji tiba ya haraka. Lakini wakati mwingine, inaweza kukukosesha raha na kuwa na maumivu, dalili zikiongezeka wakati umesimama au wakati unanyanyua vitu vizito. Watu wengi huona uvimbe ukizidi na hatimaye humwona daktari.

Kuna wakati ambapo hernia inahitaji huduma ya haraka ya upasuaji, kwa mfano, pale sehemu ya utumbo inapokuwa imezibwa na hernia ya tumbo (inguinal hernia).

Hatua za haraka za uchunguzi zinatakiwa zichukuliwe wakati inguinal hernia inapoanza kuonyeza dalili kali za:

. Maumivu
. Kusikia kichefuchefu
. Kutapika

Uvimbe wa hernia yenye dalili hizi mara nyingi ni mgumu na huleta maumivu na hauwezi kusukumwa urudi ndai ya tumbo.

Hiatal hernia inaweza kuleta dalili za acid refluc kama kiungulia, kinachotokana na tindikali za tumboni kupanda kwenye koromeo.


Tiba Ya Hernia

Hernia isipokuwa na dalili mbaya, njia bora ni kuiacha na kusubiri, ingawa hii inaweza kuwa njia sahihi kwa hernia za ina fulani, kama femoral hernia.

Madaktari bado hawajafikia kukubaliana wote kuhusu faida za kufanya upasuaji kwa inguinal hernia ambayo haijaanza kuleta usumbufu ambayo inaweza kusukumwa ndani ya tumbo. Madaktari wengi wa nchi ya Marekani wanashauri kusubiri badala ya kufanya upasuaji. Wengine wanashauri kufanya upasuaji ili kuiwahi kabla haijaweza kuziba sehemu za utumbo.

Uamuzi wa kufanya upasuaji unategemea hali iliyopo, pamoja na sehemu hernia ilipo, ambapo kuna upasuaji wa aina mbili unaoweza kufanyika:

. Open surgery
. Laparoscopic operation (keyhole operation).

Open surgery huziba hernia kwa kutumia nyuzi (sutures), mesh au vyote na kidonda juu ya ngozi kuzibwa kwa nyuzi, staples au surgical glue.






Laparoscopic repair hutumika kwa upasuaji wa kujirudia ili kukwepa makovu, igawa ni ghali zaidi, inapunguza uwezekano wa kuleta madhara hasa ya maambukizi ya vijidudu.

Kwa kulinganisha upasuaji huu wa aina hizi mbili, asilimia za uwezekano wa hernia kujirudia zinalingana, ingawa open surgery inaweza kusababisha madhara zaidi, kama maambukizi ya vijidudu

MATATIZO YA TEZI KIBOFU (TEZI DUME)



Tezi Kibofu Ni Nini?

Tezi kibofu au tezi dume kama ilivyozoeleka kutamka, ni kiungo ambacho ni sehemu ya mfumo wa uzazi vya mwanamme kinachouzunguka mrija wa mkojo. Tezi dume ipo katikati ya kibofu cha mkojo na dhakari na ipo mbele kidogo tu ya rektamu. Mrija wa mkojo unapita katikati ya tezi dume ukitokea kwenye kibofu na kuelekea kwenye uume, na kutoa mkojo nje ya mwili.

Tezi dume hutoa majimaji yenye kazi ya kurutubisha na kulinda shahawa. Mwanamme anapofikia kileleni, tezi dume hukamulia maji haya ndani ya mrija wa mkojo na kutolewa pamoja na mbegu kama manii (semen).
Mirija ya vasa diferentia hutoa mbegu kutoka kwenye korodani hadi kwenye seminal vesicles. Seminal vesicles huchangia majimaji kwenye manii wakati mwanamme anapofikia kumwaga manii.

Kwa vile nimetaja kuwa tezi dume ni sehemu ya mfumo wa uzazi wa mwanamme, swali linaweza kuja; Jee, wanawake hawana tezi dume?

Wanawake wana viungo vidogo viwili vinavyoitwa Skene’s glands vilivyopo eneo la chini la mwisho wa mrija wa mkojo, karibu na eneo ambalo linasadikika kuwepo kwa G-spot. Viungo hivi hutoa majimaji yanayosaidia kulainisha tundu la mrija wa mkojo. Viungo hivi ni vidogo ukilinganisha na tezi dume ya mwanamme. Bado kuna mjadala kuhusu kazi za skene’s glands katika mwili wa mwanamke na kuhusika kwake katika tendo la ndoa. Baadhi ya watafiti wanaamini kuwa viungo hivi ndivyo vinavyotoa majimaji (“female ejaculate”), mwanamke anapofika kileleni.


Magonjwa Ya Tezi Dume 

Wanaume wote wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya tezi dume na hasa wanapofikia umri wa miaka 50. Hapa chini tutapitia baadhi ya matatizo yanayowasumbua zaidi wanaume:

Benign Prostatic Hyperplasia (BPH) au Prostate Enlargement


Hii ni hali ambapo tezi dume huongezeka ukubwa. Zaidi ya theluthi ya wanaume wote walio juu ya miaka 50 wana dalili za kuvimba kwa tezi dume. Haijajulikana kwa uhakika ni kwa nini tezi dume huwa kubwa zaidi kadri umri unavyoongezeka, lakini kukua huku si dalili ya kansa na wala hakuongezi uwezekano wa kupata kansa. Hili si tatizo kubwa sana la kiafya.






Tezi dume iliyoongezeka ukubwa huleta msukumo juu ya mrija wa mkojo na kibofu cha mkojo hali ambayo inaweza kuathiri namna mkojo utakavyotoka.

Dalili ya tezi dume iliyovimba ni:

. Shida katika kuanza kukojoa au kuubana mkojo
. Mtiririko dahifu wa mkojo
. Kukojoa kwa shida
. Kujisikia kuwa hujamaliza mkojo
. Mkojo kuendelea kudondoka kwa muda mrefu baada ya kumaliza
. Hali ya kujisikia kukojoa mara kwa mara au ghafla
. Kuamka mara nyingi zaidi usiku kwa ajili ya kwenda haja ndogo

Kwa baadhi ya wanaume, dalili zinaweza kuwa ndogo ambazo hazihitaji tiba. Kwa wengine, zinaweza kuwa kubwa na kuathiri maisha yao. Wanaume hupatwa hofu kuwa kuvimba kwa tezi dume kunasabihiana na upataji wa kansa ya tezi dume. Hii siyo kweli kwani uwezekano wa kupata kansa wa mtu mwenye tez i iliyovimba hauzidi ule wa mtu asiye na tatizo hili la tezi.

Sababu ya kuongezeka ukubwa wa tezi dume haijajulikana, lakini wataalamu wengi wanaamini kuwa inahusiana na mabadiliko katika homoni yanayotokea umri wa mtu unapokuwa mkubwa.
Tiba ya Tezi Iliyokua



Tiba ya tezi hutolewa kulingana na hali iliyofikiwa. Kwa dalili ndogo au za kati, hakuna tiba maalumu inayotolewa isipokuwa uangalizi na vipimo vya mara kwa mara ili kuona maendeleo ya tezi hiyo. Utashauriwa kubadili mtindo wako wa maisha, kama kupunguza utumiaji wa kahawa na pombe, na kufanya mazoezi ya mwili. Pamoja na kubadili mtindo wa maisha, dawa zinaweza zikatolewa, zikiwemo finasteride na dutasteride. Dawa hizi huzuia ufanyaji kazi wa homoni iitwayo dihydrotestosterone na kuweza kupunguza ukubwa wa tezi dume.

Upasuaji unaweza kufanyika endapo dalili za kati au mbaya za tezi dume zimeshindikana baada ya matumizi ya dawa.

Madhara yanayoweza kutokea kutokana na benign prostate enlargement ni; maambukizi kwenye njia ya mkojo – UTI, kutokana na kuwa wadudu kama bakteria waliomo kwenye njia ya mkojo hawataweza kusukumwa nje wakati wa kukojoa, na Acute Urinary Retention (AUR) ambayo ni hali inayotokea ghafla ya kushindwa kusukuma mkojo nje ya mwili. AUR inatakiwa kutibiwa mara moja kwani kushindwa kufanya hivyo kutasababisha mkojo kurudi nyuma hadi kwenye figo na kuziharibu.

Dalili Za AUR ni:

. Kushindwa kutoa mkojo ghafla
. Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo
. Kuvimba kwa kibofu cha mkojo kunakoweza kuonekana kwa kujipapasa na mikono
Prostatitis

Prostatis ni tatizo ambapo tezi dume huvimba. Mara nyingine hali hii hutokana na maambukizi ya bakteria, ingawa mara nyingi hakuna maambukizi ya bakteria yanayoonekana na inashindwa kufahamika sababu ya hali hiyo kutokea.

Tofauti na kukua kwa tezi dume (BPH) au kansa ya tezi dume ambavyo huathiri zaidi wanaume wenye umri mkubwa, prostatis inaweza kutokea kwa wanume wa umri wo wote. Hasa, huonekana zaidi kwa wanaume wenye umri kati ya miaka 30 na 50.

Baadhi ya dalili za prostatis ni:

. Maumivu kwenye nyonga, viungo vya uzazi vya nje, sehemu ya chini ya mgongo na makalio
. Maumivu wakati wa kukojoa
. Kujisika haja ndogo mara kwa mara
. Kukojoa kwa shida, kama kuanza au kuuminya mkojo
. Maumivu wakati wa kukojoa manii, ambayo yanaweza kusababisha uume kutosimama au kukosa hamu ya mapenzi

Wakati mwingine unaweza kusikia uchovu, miwasho kwenye maungio ya mifupa na misuli, baridi na joto kali.

Dalili hizi kwa kawaida huanza taratibu na huja na kutoka kwa kipindi cha miezi kadhaa, ingawa wakati mwingine huweza kutokea ghafla.


Nini Chanzo Cha Prostatitis?

Kuna aina kuu mbili za prostatitis:

. Prostatitis sugu (Chronic prostatitis) – dalili hutokea na kupotea katika kipindi cha miezi kadhaa, hii ni aina ya prostatitis inayoonekana zaidi

. Prostatitis kali (Acute prostatitis ) – dalili zake ni kali zaidi na hutokea ghafla; hujionyesha mara chache, lakini huwa ni hatari na huhitaji tiba ya haraka

Acute prostatitis husababishwa zaidi na maambukizi ya bakteria katika njia ya mkojo (figo, kibofu cha mkojo, na mirija inayoviunganisha) wanaoingia kwenye tezi dume.

Kwenye prostatitis sugu , madaktari mara nyingi hawaoni maambukizi kwenye tezi dume na sababu za tatizo huwa hazieleweki.


Tiba Ya Prostatitis

Tiba ya prostatitis hulenga kuziondoa dalili za tatizo hilo. Dawa za kuondoa maumivu kama paracetamol au ibuprofen zinaweza kusaidia kuondoa maumivu.

Tiba iitwayo alpha-blocker (kama tamsulosin) inaweza luandikwa kama kuna matatizo katika kukojoa, na hizi husaidia kulegeza misuli katika tezi dume na kwenye kibofu cha mkojo.

Mara nyingine, matumizi ya antibiotics (kama ciprofloxacin) ya wiki 4 hadi 6 huweza kuandikwa hata kama maambukizi hayakuonekana. Hii hufanywa kuona kama kutatokea mabadiliko.

Tiba ya prostatitis sugu inaweza kuleta changamoto, kwa sababu kuna elimu kidogo sana kuhusu sababu za hali hiyo. Watu wengi hupona taratibu baada ya tiba, ingawa inaweza kuwachuka miezi au miaka.

Watu wengi wenye prostatitis kali hupona kabisa katika wiki chache, ingawa mmoja katika kumi hujikuta wakipata prostate sugu baadaye.

Watu wengine hujikuta wakirudiwa na matatizo baada ya tiba, hali ambayo itahitaji tiba zaidi. Prostatitis siyo kansa na ushahidi wa kuonyesha kuwa inaweza kuongeza uwezekano wa kupata kansa ya tezi dume.


Kansa Ya Tezi Dume (Prostate Cancer)

Nchini Uingereza, kansa ya tezi dume ndiyo aina ya kansa inayoonekana zaidi kwa wanaume, kukiwa na wagonjwa zaidi ya 40,000 wanaobainika kila mwaka. Haijajulikana kinaga ubaga kwa nini aina hii ya kansa inatokea, lakini yamkini ya kupata aina hii ya kansa huongezeka na umri. Kansa hii huwapata wanaume hasa wenye umri wa zaidi ya miaka 65, ingawa wanaume waliozidi miaka 50 nao huwa kwenye hatari.

Uwezekano wa kupata kansa ya aina hii ni mkubwa pale unapokuwa na kaka na baba mwenye tatizo hili, na watu weusi wa maeneo ya Caribbean.






Dalili za kansa ya tezi dume hufanana sana na zile za kukua kwa tezi dume na ni vugumu sana kuzitofautisha. Dalili zinaweza kuwa:

. Kujisikia kukoja mara nyingi (na hasa usiku)
. Kusikia mkojo ghafla
. Shida katika kuanza kukojoa
. Kukojoa kwa shida na kuchukua muda mrefu
. Mkojo kutiririka kwa kiwango kidogo
. Hali ya kujisikia kutomaliza mkojo

Kansa ya tezi dume huanza na kukua taratibu sana. Watu wengi hufa na kansa ya tezi dume, na si kwa sababu ya kuwa nayo. Kansa ya tezi dume, kwa hiyo, haina haja ya kutibiwa mara moja.


Tiba Ya Kansa Ya tezi Dume



Kwa wanaume wengi kansa ya tezi dume haihitaji tiba ya mara moja.Kansa ikiwa kwennye hatua za awali na haina dalili, kitakachofanywa ni kuchukua uangalizi wa karibu.

Wakati mwingine, kansa inaweza kutibiwa ikiwa kwenye hatua za awali. Tiba inaweza kuwa upasuaji wa kuondoa tezi dume, tiba ya mionzi au tiba ya homoni (hormone therapy).

Kansa nyingine hugundukia wakati ambapo tayari zimeanza kuenea. Kansa iliyoenea kwenye sehemu nyingine za mwili, mara nyingi kwenye mifupa, haiwezi kutibika na kitakachofanywa ni kuchukua hatua za kumwongezea mgonjwa muda wa kuishi na kuondoa dalili za kansa hiyo.

Tiba nyingi za kansa hufanywa kukiwa na uwezekano wa kupata madhara mengine, kama kupoteza uwezo wa jogoo kuwika au kupata hali ya mkojo kutoka wenyewe. Kwa sababu hiyo, wanaume wengi huahirisha tiba hadi wanapoona kuwa kansa hiyo itasambaa sehemu nyingine za mwili.

Kwa sababu kansa ya tezi dume hukua taratibu sana, unaweza kuishi nayo miaka mingi bila kukusababishia dalili mbaya au kuhitaji tiba. Lakini inaweza kuathiri maisha yako au kukusababishia matatizo ya jogoo kushindwa kuwika na mkojo kutiririka wenyewe.

SABABU ZA UGUMBA KWA MWANAMKE






Katika ukurasa uliopita tulijadili sababu za mwanamke kutopata mtoto zinazotokana na mapungufu ya mwanamme. Katika ukurasa huu tatarejea kwenye mada kuu ya kuona sababu za ugumba au utasa kwa mwanamke na kutazama mapungufu katika mwili wa mwanamke yanayochangia tatizo hili. Kama ada, katika ukurasa mwingine tutaona njia zinazotumika kuondoa tatizo hili la mwanamke kukosa kizazi.

Tulisema kwamba ugumba ni hali ambapo mwanamme na mwanamke wamejamiiana kwa kipindi cha mwaka mmoja bila kinga na bado mwanamke hakuweza kupata ujauzito. Tuliona kuwa hali hii inachangiwa na jinsia zote na si mwanamke peke yake kama ilivyozooleka kuamini hapo zamani. Ilibainishwa kuwa theluthi moja ya nyumba zenye tatizo hili huwa imeathirika kutokana na mapungufu ya mwanamme, theluthi nyingine kutokana na mwanamke na inayobakia inaathiriwa na matatizo au ya wote wawili au yale ambayo hayaeleweki.Tulishauri kuwa linapotokea tatizo hili, wote wawili wanatakiwa wapimwe ili kujua ni nani kati yao ndiye chanzo cha tatizo.
Sababu Za Mwanamke Kukosa Kizazi



Ili mwanamke apate mimba, sehemu zote za mwili wake zinazohusika na uzazi zinatakiwa zifanye kazi inavyotakiwa na katika hatua zote. Hatua katika utengenezaji wa mimba ni kama zifuatazo:



1. Moja kati ya ovari mbili za mwanamke kuachai yai lililokomaa
2. Yai hii kusafirishwa na mrija wa uzazi (fallopian tube)
3. Mbegu za mwanamme kusafiri hadi kwenye cervix, kupitia tumbo la uzazi (uterus) hadi kwenye mrija wa uzazi, kulifikia yai na kulipevusha.
4. Yai lililopevushwa kusafiri kupitia mrija wa uzazi hadi kwenye tumbo la uzazi (uterus).
5. Yai kunata kwenye ukuta wa uterus na kukua

Ugumba kwa mwanamke unaweza kutokana na dosari katika hatua yo yote katika hizo tulizozitaja na mara niyingine kutokana na dosari katika hatua zaidi ya moja.

Pamoja na kuwa kuna sababu nyingi za mwanamke kutopata mimba, lakini sababu kuu tatu ndizo zinazohusika zaidi kama tutakavyozielezea hapa chini.







Kushindwa Kuzalisha Mayai (Anovulation)



Hili ndilo tatizo ambalo linachangia ugumba kwa wanawake kwa asilimia 30 lakini kwa bahati nzuri asilimia 70 ya wanawake wenye tatizo hili hupata tiba na kufanikiwa kupata watoto. Mwanamke mwenye tatizo hili hutoa mayai mara chache au hatoi mayai kabisa. Chanzo cha tatizo huwa ni moja ya yafuatayo:

1. Matatizo Ya Homoni

Matatizo ya homoni ndiyo yenye mchango mkubwa zaidi kwenye kumfanya mwanamke ashindwe kuzalisha mayai. Uzalishwaji wa mayai hutegemea mchanganyiko wa homoni utakaofanya kazi kwa kuhusiana bila kuvurugwa katika utendaji wake wa kazi.



Kuna matatizo ya aina tatu yanayoweza kuvuruga mpangilio huo.

Kuzalisha Mayai Yasiyokomaa:

Matatizo Ya Hypothalamus: Hypothalamus ni sehemu ya ubongo inayohusika na kutoa ishara kwa tezi ya pituitary (pituitary gland) ambayo nayo huamsha homoni za ovari zinazoruhusu yai kukomaa. Hypothalamus isipofanya kazi yake, mayai hushindwa kufika ukomavu. Asilimia 20 ya dosari za ukomavu wa mayai husababishwa na matatizo ya hypothalamus.

Matatizo Ya Pituitary Gland: Tumeona hapo juu kuwa tezi ya pituitary inahuvusika katika kukomaza mayai. Endapo pituitary itatoa homoni kwa kiwango kidogo au kikubwa kupita kiasi, ovari zitashindwa kuzalisha na kutoa mayai ipaswavyo. Hali hii hutokea pale tezi hii inapoharibiwa kwa ajali, kunapotokea uvimbe ndani yake au kunapokosekana ulingano wa kikemikali ndani ya tezi hiyo.


2. Makovu Kwenye Ovari

Uharibifu kwenye ovari unaweza kusababisha ovari hizi kushindwa kuzalisha mayai. Operesheni za mara kwa mara hujenga makovu kwenye ovari hizo na kuzifanya zishindwe kuzalisha mayai. Maambukizi ya magonjwa huweza pia kusababisha ovari kushindwa kuzalisha na kutoa mayai.

3. Kukoma Hedhi Mapema

Kukoma hedhi mapema ni tatizo ambalo halijaeleweka vizuri kisayansi. Baadhi ya wanawake wanaacha kupata siku zao za
kawaida kwenye umri usiotegemewa. Dhana moja ni kuwa hifadhi yao ya mayai imekwisha au nyingine ni kuwa inatokana na wanawake hawa kuwa wenye historia ya kuwa wanariadha waliokuwa na miili yenye uzito mdogo na waliofanya mazoezi
ya nguvu kwa muda mrefu. Kuna uwezekano kuwa kukoma hedhi mapema ni suala la urithi.

4. Matatizo Ya Follicle

Kuna tatizo lisilo na maelezo ya kisayansi “unruptured follicle syndrome” ambapo mwanamke hutengeneza mfuko wa kawaida wa yai wenye yai ndani yake kila mwezi lakini mfuko huo hugoma kupasuka na kuachia yai. Hivyo kwamba, yai hubaki ndai ya ovari na utolewaji wa yai nje ya ovari kutotokea.


Mirija Ya Uzazi (Fallopian Tubes) Kushindwa Kufanya Kazi Vizuri



Magonjwa katika mirija ya uzazi huathiri asilimia 25 ya wanafamilia ambapo tatizo laweza kuwa dogo la kunata kwa yai au kubwa la mirija kuzibwa kabisa. Tiba kwa matatizo ya mirija ya uzazi mara nyingi ni upasuaji. Matatizo yanayopelekea kuziba kwa mirija ya uzazi ni kama yafuatayo:
1. Maambukizi Ya Wadudu

Maambukizi ya virusi na bacteria yanayoenezwa kwa ngono husababisha makovu na uharibifu, kwa mfano, maambukizi ya
Hydrosalpnix yanayosababisha mirija ya uzazi kuziba pande zote na kujaa maji .

2. Magonjwa ya Tumbo

Magonjwa ya appendicitis na colitis huleta madhara kwenye tumbo ambayo yanayoweza kuiathiri mirija ya uazazi kwa kujenga makovu au kuiziba.

3. Upasuaji

Hii ni sababu kubwa ya magonjwa na uharibifu wa mirija ya uzazi. Upasuaji wa kwenye maeneo ya kinena na tumbo huweza kusababisha uharibifu utakaozuia upitaji wa yai.

4. Mimba Ndani Ya Mirija Ya Uzazi (Ectopic Pregnancy)

Mimba zinazotunga ndani ya mirija ya kizazi huweza kuleta uharibifu kwenye mirija hiyo hata kama tahadhali ya juu
itachukuliwa kuziondoa.

5. Matatizo Ya Kuzaliwa Nayo

Mara chache huweza kutokea kuwa mwanamke akazaliwa akiwa na dosari katika mirija yake ya uzazi.


Endometriosis


Endometriosis ni kuota kwa seli (endometrial cells) zinazofanana na zile zinazotanda ndani na nje ya mfuko wa uzazi (uterus) kwenye eneo nje ya mfuko wa uzazi. Endometrial cells ndizo zinazoufunika mfuko wa uzazi na seli hizi hubadilishwa kila mwezi wakati wa hedhi. Seli hizi huweza kuota kwenye maeneo mengine yaliyo nje kabisa ya mfuko wa uzazi na huitwa endometriosis implants. Maeneo ambayo seli huweza kuota ni kwenye ovari, mirija ya uzazi (fallopian tubes), kuta za nje za nyumba ya uzazi, utumbo, pelvis, kuma , cervix, kibofu na mara chache kwenye maini, mapafu na ubongo.






Endometriosis imegundulika zaidi kwenye kundi la wanawake wenye umri kati miaka 25 na 35, ingawa mara chache
imeonekana kwa wasichana wadogo wa miaka kama 11. Endometriosis ni nadra kuonekana kwa wanawake waliokoma hedhi. Wanawake warefu , wembamba wenye uzito mdogo huonekana zaidi na tatizo hili. Kupata ujauzito katika umri mkubwa sana, kutozaa na kukoma siku mapema huongeza uwezekan wa kutokea endometriosis.

Kuota kwa seli hizi za ziada – na tendo la kuziondoa kwa operesheni – huweza kusababisha makovu ambayo huweza kuzuia yai la mwanamke lisiungane na mbegu ya mwanamme. Kuathirika kwa utando huu juu ya uterus huweza kuzuia kutungwa kwa yai lililopevushwa.


Sababu Nyinginezo



1. Sababu Za Kitabia

Baadhi ya tabia zetu huathiri afya zetu ikiwa ni pamoja na afya ya viungo vya uzazi na kupunguza au kuondoa uwezo wetu wa kuzaa watoto. Bahati nzuri tabia hizi zinaweza kudhibitika.

. Chakula Na Mazoezi: Ili tuwe na uwezo mzuri wa kuzaa watoto tunahitaji kupata chakula kizuri na kuipa miili yetu mazoezi ya kutosha. Wanawake wenye unene wa kupindukia au uzito mdogo sana wanapata shida kushika mimba.

. Uvutaji Wa Sigara: Uvutaji wa sigara umethibitika kupunguza kiwango cha mbegu (low sperm count) kwa wanaume, kuongeza uwezekano wa mimba kutoka, kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo au kabla ya wakati (njiti) kwa wanawake.

. Pombe: Unywaji wa pombe huongeza uwezekano wa kuzaa mtoto mwenye matatizo na unywaji uliozidi huweza kuleta ugonjwa, Fetal Alcohol Syndrome. Kwa mwanaume, pombe hupunguza kiwango chake cha mbegu.

. Madawa: Madawa kama bangi (marijuana) hupunguza kiwango cha mbegu kwa wanaume. Utumiaji wa cocaine kwa wanawake huathiri figo za watoto watakaozaliwa.


2. Sababu Za Kimazingira

Uwezo wa mwanamke kutunga mimba unaweza unaweza kuathiriwa na uwepo wake kwenye mazingira yenye sumu au kemikali. Hii inaweza kuwa kwenye mazingira ya kazi au sehemu anayoishi. Baadhi ya kemikali zilizobainika na kuandikwa kuwa
zinapunguza uwezo wa mwanamke kupata mimba ni:

. Lead – husababisha mimba kutoka.
. Tiba – tiba ya mionzi ya mara kwa mara na chemotherapy huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na matatizo ya ovari.
. Ethylene Oxide – kemikali inayotumika kuua wadudu kwenye vifaa vya upasuaji na kutengenza dawa za kuulia wadudu huleta dosari kwenye mimba changa na kusababisha mimba kutoka.
. Dibromochloropropane (DBCP) – Kemikali inayopatikana kwenye dawa za kuulia wadudu husababisha mwanamke kukoma hedhi mapema.

UJUE UGONJWA NA TIBA YA UTI






UTi ni ugonjwa ambao unasumbua watu wengi; watoto, vijana na watu wazima. UTI ni kifupisho cha Urinary Tract Infection. Huu ni ugonjwa ambao hushambulia figo (kidneys); ureters; ambayo ni mirija inayounganisha figo na kibofu cha mkojo, kibofu cha mkojo (bladder) na urethra; sehemu inayotoa mkojo toka kwenye kibofu cha mkojo hadi nje ya mwili. Kwa kifupu ugonjwa wa UTI hushambulia viungo vinavyohusika katika kupitisha mkojo kabla haujatoka nje ya mwili. Hebu tuvitazame viungo hivi kabla ya kueleza chanzo cha ugonjwa na tiba ya UTI baadaye hapa chini.

Kuelewa vizuri tunachokizungumzia hapa tazama picha ya viungo hivi na kwa kifupi hapa tutatoa maelezo ya picha hiyo. Figo ni viungo viwili vilivyopo kimoja kila upande wa uti wa mgongo eneo la kiunoni. Figo hufanya shughuli nyingi katika mwili wa binadamu ikiwepo ya kutoa uchafu na maji ya ziada katika damu, na huvitoa vitu hivi kama mkojo. Kwa sababu hii, figo ni muhimu sana katika kuweka msukumo wa damu kwenye kiwango kizuri. Figo pia husikia
mapema sana mabadiliko ya kiwango cha sukari mwilini na mabadiliko katika kiwango cha msukumo wa damu (blood pressure). Kiwango cha sukari na msukumo wa damu vikizidi, vyote huweza kuleta madhara kwenye figo.








Ureters ni mirija miwili myembamba yenye urefu wa yapata nchi 10 hivi kila mmoja ambayo huchukua mkojo kutoka kwenye figo na kuumwaga ndani ya kibofu cha mkojo.

Kibofu cha mkojo ni kijimfuko kidogo kinachopokea mkojo kutoka kwenye mirija ya ureters na kuuhifadhi. Mkojo ukifikia kiwango fulani ndani ya kibofu cha mkojo, tunasikia haja ya kuupunguza (kukojoa) na ndipo misuli ya nje ya kibofu cha mkojo hujibana na kuukamua mkojo nje ya kibofu.

Urethra ni mrija unaounganisha kibofu cha mkojo na nje ya mwili.

Sehemu yo yote katika hizi tulizozitaja hapa juu, inaweza ikapata maambukizi ya UTI na kadri maambukizi hayo yatakavyokuwa ndani zaidi ukitokea nje, ndivyo ugonjwa huu utakavyokuwa umefikia hali mbaya zaidi. Wasichana na akina mama hupata maambukizi haya kwa wingi zaidi kuliko wavulana au akina baba. Asilimia kama 40 ya wanawake na asilimia 12 ya wanaume hupata maambukizi haya ya UTI katika maisha yao.


Chanzo Cha UTI Ni Nini?





Mkojo kwa kawaida ni kitu kisicho na wadudu wo wote wabaya. Maambukizi yanakuja pale wadudu wanapoingia kwenye mkondo wa mkojo kupitia kitundu cha kutolea mkojo nje ya mwili na kufuata mkondo huo kuelekea kwenye figo. Wadudu hao wakisha ingia huanza kuzaliana. Asilimai 90 ya maambukizi yasiyo mabaya sana huwa ni ya bacteria waitwao Escherichia Coli au kwa kifupi E. Coli. Kwa kawaida bacteria hawa huishi katika utumbo au karibu na maeneo ya mkundu. Wadudu hawa wanaweza wakatembea kutoka eneo la mkundu wakaelekea kwenye tundu la mkojo na kuingia. Lakini, kutojisafisha kwa namna nzuri (kwa mfano, kutawadha kuanzia nyuma kuja mbele) au ngono ndizo njia mbazo huambukiza
bacteria hawa kirahisi zaidi.



Bacteria wa E.Coli



Wanawake hupatwa zaidi na maambukizi haya kwa sababu ya ukaribu wa mkundu na kijitundu cha kutolea mkojo na kwa sababu ya ufupi wa urethra katika miili yao ukilinganisha na wanaume. Wanawake wanaoshiriki ngono mara nyingi na watu tofauti hupatwa na maambukizi zaidi kuliko wale wanaoshiriki kwa kiwango kidogo.

Wanawake wanaotumia diaphragms kama njia ya uzazi wa mpango hupatwa zaidi na tatizo hili pia akina mama waliokoma hedhi kwa sababu ya ukosefu wa homoni ya estrogen. Kukosekana kwa estrogen kunasababisha mabadiliko katika mkondo wa mkojo na kuufanya uweze kuambukizwa kwa urahisi zaidi.

Matatizo yo yote yanayosababisha mkojo usitoke nje kwa urahisi huongeza uwezekano wa kupata maambukizi ya UTI. Mifano ni; watoto kuzaliwa na matatizo katika mikondo yao ya mkojo ambayo huzuia mkojo usitoke nje kirahisi, matatizo ya kidney stones na prostate kukua kupita kiasi; na watu wanaotoa mkojo kupitia kifaa maalumu (catheter).

Tendo la kukojoa huwatoa bacteria hawa nje ya mwili lakini wakiwa wengi sana, kukojoa hakuwezi kuwatoa wakaisha. Wadudu hawa husafiri kwenye urethra hadi kwenye kibofu cha mkojo ambako watazaliana. Wanaweza kuendelea kusafiri kupitia ureters hadi kwenye figo ambako pia watazliana na kuleta matatizo makubwa endapo tiba nzuri haitatolewa kwa wakati muafaka.


Ni Nini Dalili Za UTI?





Dalili za ugonjwa huu huwa tofauti kulingana na hatua ambayo ugonjwa umeshafikia.






Lower UTI ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na kibofu cha mkojo (bladder). Katika hatua hizi, mgonjwa atasikia dalili zifuatazo:

. Maumivu wakati wa kukojoa
. Kujisikia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu
. Damu katika mkojo
. Mkojo wenye rangi ya chai
. Mkojo wenye harufu kali
. Maumivu ya kiuno kwa wanawake
. Maumivu ya sehemu za nyuma kwa wanaume

Upper UTI ni maambukizi ya ndani ya figo. Hii ni hatua mbaya sana endapo bacteria wataanza kuingia kwenye mkondo wa damu kutoka kwenye figo – SEPSIS. Sepsis huweza kusababisha msukumo wa damu kuwa mdogo sana (Low Blood Pressure), mshituko au kifo.

Dalili za upper UTI ni:

. Maumivu ya maeneo ya juu ya mgongo
. Homa
. Kusikia baridi
. Kusikia kichefuchefu
. Kutapika


Hatua Za Kujikinga Na UTI



Kuna hatua unazoweza kuchukua ili usipatwe na maambukizi ya ugonjwa huu kirahisi. Hii ni pamoja na kujifuta au kutawadha ukianzia mbele kwenda nyuma baada ya haja kubwa au ndogo. Kunywa maji mengi, glasi 6 hadi 8 za maji kila siku na kuhakikisha unakunywa maji baada ya kushiriki tendo la ndoa. Haifai kuubana mkojo kwa muda mrefu, timiza haja mara itokeapo. Kusafisha maeneo nyeti mara kwa mara. Kuoga kupitia bomba la mvua ni bora zaidi kuliko kutumbukia kwenye josho. Ni vema kuvaa chupi zilizotengenezwa kwa pamba.


Tiba Ya UTI



Tiba kwa ugonjwa wa UTI kwa hatua zote ni antibiotics. Daktari ataamua kukupa tiba na kukuruhusu kuendelea na tiba nyumbani kwako au kukulaza kulingana na alivyoiona hali ya ugonjwa wako. Tiba ya lower UTI ikitolewa kwa wakati mwafaka na inavyotakiwa, hakuna matatizo makubwa yanayoweza kutokea.



Garlic Oil Softgel








Garlic oil.



Kazi Na Faida Zake


Inazuia na kuua aina nyingi za wadudu wa magonjwa
Inapunguza uzito wa damu na kupunguza kiwango cha cholesterol katika damu
Inazuia atherosclerosis na magonjwa ya moyo yatokanayo
Kulinda mifumo ya mishipa ya moyo na ubongo kwa kupunguza msukumo wa damu mwilini



Yafaa Kwa:
Magonjwa ya ufanyaji kazi wa viungo kama pressure ya juu, kisukari na cholesterol kuwa nyingi
Watu wenye magonjwa sugu ya maambukizi kama candidiasis


Maelezo Muhimu:

Kuhusu Garlic:
Garlic imejizolea umaarufu mkubwa Afrika na huko Asia kwa thamani yake katika mapishi. Utafiti wa kisasa umehakikisha faida za tiba ya garlic kwa sababu ya uwingi wa viungo vilivyomo ndani yake, kama alliin, alliinase, allicin, S-allylcysteine, diallyl sulfide na allyl methyl sulfide. Garlic ni chanzo cha selenium katika chakula. Ikiwa imepewa jina la "smelling rose", garlic inajijengea umaarufu ambao hauwezi kupata mpinzani katika medani hii maarufu ya virutubisho vya kiada.

Kuzuia Bakteria (Anti-microbial property):
Utafiti wa kisayansi katika nchi nyingi unaonyesha kuwa garlic oil inazuia na kuua aina nyingi za vijidudu kama bakteria, fungus waletao magonjwa, virusi, amoeba protozoon, trichomoniasis na vimelea (parasites). Garlic Oil Softgel inaweza kutumika kama antibiotic ya kiasili.

Antioxidant:
Ufanyaji kazi wake kama antioxidant unausaidia mwili kuondoa radikali huru, ambazo zinaweza kuvuruga ufanyaji kazi wa mwili na kusababisha kansa.

Kupunguza Cholesterol Katika Damu:
Garlic oil inapunguza kiwango cha lipids nyepesi au cholesterol mbaya, hatua ambayo inasaidia dhidi ya magonjwa ya moyo yanayosababishwa na atherosclerosis. Muhimu zaidi ni kuwa inapunguza kiwango cha cholesterol na triglycerides katika mwili kwa jumla. Kemikali zilizopo ndani ya garlic oil zinasidia ujenzi wa cholesterol (HDL) cholesterol).

Kupunguza Pressure:
Garlic Oil inafanya kazi ya kupunguza uzito wa damu na imedhihirika kufanya kazi ya kuzibua mishipa ya damu na kuzuia atherosclerosis. Uwezo huu wa Garlic wa kuifanya damu kuwa nyepesi ni muhimu katika kuzuia kiharusi na kuziba kwa mishipa ya damu. Kutumia garlic oil vile vile kunasaidia katika kushusha kiwango cha sukari katika damu.

Kupunguza Sukari Mwilini:
Kunywa vidonge vya garlic oil softgel kumeripotiwa kuwa kunapunguza viwango vya sukari katika damu na kuongeza serum insulin. Upunguzwaji wa sukari katika damu unategemea kiungo kilichoko ndani ya garlic oil, allicin, kitu kinachochangia harufu kali ya kipekee ya garlic.







Lakini tiba ispotolewa kwa wakati, maambukizi haya ya mkondo wa mkojo huweza kuleta matatizo makubwa. Pamoja na mengine mgonjwa anaweza:

. Kupata maambukizi ya mara kwa mara
. Kupata uharibifu wa figo wa kudumu na kuhitaji huduma maalumu ya kutibu figo (dialysis).
. Kutokea uwezekano wa kuzaa watoto wenye uzito mdogo au wanaozaliwa kabla ya wakati. . Wanaume wanaougua UTI mara kwa mara wanakuwa kwenye hatari ya kupata madhara kwenye tezi dume (prostatitis). Uvimbe huweza kutokea kwenye tezi dume na kusababisha maumivu wakati wa haja ndogo au kutoa shahawa. . Sumu katika damu. Mara chache huweza ikatokea kuwa bakteria wakasambaa kutoka ndani ya figo na kuingia kwenye mfumo wa damu (sepsis) na baadaye kusambaa hadi kwenye viungo vingine muhimu vya mwili. Hali hii ikitokea, itabidi mgonjwa awekwe chini ya uangalizi mkali wakati akipewa tiba ya kuwaua bakteria hao.

DAWA YA MIKUNYANZI YA NGOZI: UNATAKA KUONDOA WRINKLES?






Jee, ulishawahi kufikiria kutafuta dawa ya mikunyanzi ya ngozi ya juu ya mwili wako au kwa maneno mengine wrinkles ? Kwa walio wengi jibu ni ndiyo na sababu kubwa ikiwa ni kujaribu kupata mwonekano wa ujana zaidi. Katika mada nyingine, tuliona kuwa mtu huonekana mzee kutokana na vitu viwili. Kwanza ni namna anavyotenda vitendo vyake vya mwili, kwa mfano kutembea.

Tuliona kuwa mwili wa mtu unaongeza mahitaji ya madini ya calciumu kadri umri unavyoongezeka na ukikosa madini hayo kutokana na chakula anachokula, mtu huyu hushindwa kukidhi mahitaji ya mwili na mwili hulazimika kupata mahitaji yake kutoka kwenye mifupa na hivyo kuifanya mifupa kuwa dhaifu. Sababu ya pili ya kuwa na mwonekano wa uzee ni kutokana na mikunyanzi ya juu ya ngozi ya mwili (wrinkles) na tulisema kuwa ukosefu wa collagen mwilini husababisha mikunyanzi hiyo. Katika mada ya leo, tutaijadili collagen na jinsi inavyofanya kazi ya kuondoa mikunyanzi au wrinkles kwenye ngozi.

Kuna njia nyingi zinazotumika kuondoa mikunyanzi ya ngozi ikiwa ni pamoja na creams na lotions. Njia nyingine ambayo hutumika ni kuondoa tabaka la juu la ngozi lililoathirika kwa kuikwangua au kwa kuiyeyeyusha kwa kutumia kemikali. Mara nyigine mionzi hutumika kuondoa mikunyanzi ya juu ya ngozi.


Kudungwa sindano za botox huondoa mikunyanzi inayotokana na kujikunja kwa ngozi kwa kuonyesha hisia kwenye maeneo ya macho na midomo. Katika mada yetu ya leo tutajadili jinsi ya kuondokana na mikunyanzi ya juu ya ngozi (wrinkles) kwa kutumia njia rahisi – collagen.

Kwanza tuone ni sababu zipi zinafanya ngozi ya mwili wako kuwa na mikunyanzi. Imebainika kuwa kuna sababu nyingi sana ambazo kwa pamoja huchangia hali hiyo, baadhi ya sababu hizo zinaweza kuzuilika na baadhi haziwezi kuzuilika kabisa.

Umri: Umri unapokuwa mkubwa ngozi yako hupunguza uwezo wake wa kunyumbuka na kuwa ngumu. Utengenezaji wa seli mpya hupungua na kufanya tabaka la chini ya ngozi (dermis) kupungua unene wake. Kupungua kwa utengenezaji wa mafuta hufanya ngozi yako ikauke. Mafuta yaliyo chini ya ngozi yako hupungua na
kuifanya ngozi yako kulegea, kutengeneza vijibonde na kufanya mistari ionekane juu ya ngozi hiyo.

Mionzi ya jua ( ultraviolet (UV) light): Mionzi ya ultraviolet inayoongeza kasi ya kuzeeka ndicho chanzo kikubwa cha
kuwa na mikunyanzi juu ya ngozi ya binadamu. Mionzi hiyo huvunjavunja vitu vya kuunganisha ngozi – collagen na elastin ambavyo huwa chini ya ngozi kwenye tabaka la dermis. Bila vitu hivi vya kuiunganisha na kuifanya kuwa imara, ngozi huanza kulegea na mikunyanzi kuanza kujitokeza. Uvaaji wa kofia kubwa na uvaaji wa nguo zinazofunika sehemu za mwili husaidia kutopata wrinkles haraka.


Uvutaji wa tumbaku: Kuvuta tumbaku kunapunguza kiwango cha damu kinachoifikia ngozi kwa kupunguza kipenyo cha mishipa ya damu inayoelekea kwenye matabaka ya juu ya ngozi . Kemikali zilizomo ndani ya tumbaku pia huharibu collagen na elastin.

Kujikunjakunja kwa mara kwa mara kwa ngozi wakati wa kuonyesha hisia: Mistari ya juu ya kope za macho na ile inayoanzia kwenye kona za macho inaaminika kujenga mistari kutokana na matendo ya kuonyesha hisia.




Matendo kama ya kutabasamu, kukunja sura kuonyesha hasira na kukonyeza yanachangia katika kuleta mikunyanzi ya ngozi.


Collagen Ni Nini?



Collagen ni protini ngumu, isiyoyeyuka na iliyoumbwa kama nyuzinyuzi. Protini hii inayotengenezwa na amino acids hufanya theluthi moja ya protini yote iliyomo ndani ya mwili. Kuna aina nyingi za collagen, kama aina 16 hivi. Collagen hizi za ndani ya mwili ni ngumu sana na aina nyingine za collagen ni ngumu kuliko hata chuma.

Collagen hupatikana zaid kwenye ngozi na mifupa na hufanya kazi ya kuupa mwili uimara na nguvu ikiambatana na elastin. Kwenye tabaka la dermis, collagen hasaidia kujenga mtandao wa nyuzinyuzi unaosaidia seli mpya kukua juu yake. Kwa vile uzalishaji wa collagen mwilini hupungua na umri, ngozi hupoteza hali yake ya kunyumbuka na kuifanya ngozi kubonyea chini. Hivyo, mistari na mikunyanzi hujitokeza. Kupungua kwa collagen husababisha pia
udhaifu wa cartilage kwenye maungio ya mifupa (joints). Collagen huzalishwa na seli mbalimbali lakini haswa na seli za kuunganisha viungo (connective tissue cells). Mwili wa binadamu huendelea kuzalisha collagen vizuri hadi umri wa mtu unapofikia miaka 40 hivi, baada ya hapo uzalishaji hupungua na kuwa kidogo sana umri unapofika miaka 60.

Collagen hutumika kuondoa mistari na mikunyanzi ya juu ya ngozi (kuondoa wrinkles) na pia husaidia kuondoa makovu juu ya ngozi, yale ambayo hayana ncha kali. Collagen inayotumika inatokana na binadamu na wanyama wa jamii ya ng’ombe.

Collagen ni protini ambayo, kama protini nyingine inatengenezwa na amino acids. Kuna amino acids 9 ambazo ni muhimu katika utengenezaji wa collagen na ambazo hupatikana kutokana na chakula tunachokula . Chakula kizuri kwa kutoa collagen ni kile kinachotokana na wanyama, kama vile; jibini, mayai, samaki, maziwa na nyama ya kuku.

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...