1. Degree
yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class
katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubutu wako.
2.
Mwanamke anaemuheshimu mumewe ni mwanamke bora ambae kila mwanaume angetamani
kuwa nae.
3. Tabia
yako na misimamo yako ndio itakayomfanya mumeo ajute au afurahie kukuoa wewe.
4. Kuwa
mke bora inakubidi uwe vizuri katika maarifa ya kutawala hasira zako na sio
kuwa mtu wa kulipiza visasi.
5. Kuwa
kiongozi huko kazini kwako lakini kuwa mtu wa kunyenyekea nyumbani kwako kwa
mumeo. Hiyo ni busara.
6. Usiweke
mashindano na mumeo, mpe hongera na mtie moyo kwa kila hatua anayopiga katika
maisha.
7. Kuwa na
ubinadamu, sio kosa dogo tu mumeo amefanya ukatamani kulipiza kisasi. It won't
help u.
8. Kuwa
mkarimu, kila mwanaume anamuheshimu mwanamke mkarimu na mwenye msimamo.
9.
Usijaribu kumpa adhabu mumeo ya kumnyima chakula cha usiku kitandani, hii
itamlazimu kutafuta chakula nje ya ndoa.
10. Hakuna
kitu kibaya kama utakubali kuwa ulikosea kama kweli ulikosea. Kuwa mrahisi
kukubali kama kweli ulikosea. Na omba radhi pale inapobidi.
11.
Jiandae kumsamehe mumeo pale anapokosea kwa maana mke atoae msamaha kwa mumewe
ni mke mwema tofauti na yule aliejaa visasi.
12.
Tengeneza maamuzi ya kuwa mke mwema, pasina kuwa na hofu yoyote na Mungu
atakubariki.
13. La
mwisho na la muhimu tambua kwamba mwanamke aliejaliwa umbo zuri na sura nzuri
pasina maarifa kichwani anafaa kwa usiku mmoja, lakini yule mwenye maarifa na
ufahamu yeya afaa kwa maisha yote.
No comments:
Post a Comment