Wednesday, 23 March 2016

Unataka kufanikiwa katika Maisha? Acha kufanya mambo haya


Mambo ni rahisi sana kwa uhakika kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwa kile unachokifanya. Haya ni mambo ambayo kama unataka mafanikio ni lazima uyaache mara moja. 

1. Kupuuzia Mambo
Hapa tunazungumzia kupuuzia mambo ya msingi au matatizo au ishu ambazo ni za aibu unazotamani kujificha chini ya uvungu wa kitanda.

Kuna mtu mmoja aliwahi kusema tabia mbaya huendelea kukua na kuongezeka kulingana na umri. Kwa bahati mbaya kuna watu hawawezi kasi ya maisha ya sasa na hivyo kushindwa kushughulikia matatizo yanayoambatana nayo kwa kuyapuuza na kufikiri kwamba yataisha yenyewe. 

Kwa sasa huwezi ukapuuzia nguvu ya teknolojia na ukafikiri kwamba unaweza kufanikiwa zaidi ya hapo bila kuwekea mkazo teknolojia iliyopo sokoni. Na kama una tabia mbaya wala huishughulikii haitakufanikisha bali itakuyumbisha na kukuondolea mafanikio yako kabisa.

2. Kuwa na wivu 
Watu ambao hawana mafanikio ni wenye wivu mkubwa sana na mara nyingi huwa hawafurahii wengine wakifanikiwa hivyo hushindwa kuchukua wajibu wao wa kushindwa kuweka juhudi katika wanalolifanya kwenye maisha yao. Watu wenye wivu hutafuta namna ya kuwashusha wenzao waliofanikiwa na wakati mwingine huwa sababu yakuwekea vikwazo wenzao ili wasiweze kufanikiwa. 

3. Wivu husababisha uchungu
Watu wenye wivu hutengeneza uchungu fulani dhidi ya yule aliyefanikiwa. Watu wengi ambao hawajafanikiwa kimaisha / kitaaluma na hata kibiashara huweka hasira kwa mtu mwingine badala kushughulikia maisha yake au taaluma yake mwenyewe. Kutokana na hali hiyo mtu huyo huwa hawezi kutoa ushirikiano kwa wengine, na ni moja ya watu ambao huwa wako tayari kumharibia mwenzake kazi au biashara kutokana na hali hiyo.

4. Uvivu na kutojituma 
Kutokana na kuwa na wivu na uchungu kwa wengine watu ambao hawajafanikiwa huona shida kufanya kazi na wengine hivyo huwa wavivu na kuacha kujihusisha kwa juhudi kwenye kazi kama wengine ili tu asione watu wakisogea au kufanikiwa. Hufanya kazi kwa taratibu sana kiasi kwamba matokeo au muda uliotarajiwa kukamilisha kazi hushindwa kufikiwa mapema. 

5. Kupenda kujificha wakati wa kazi 
Watu ambao hawajafanikiwa kifikra na kwenye maisha wanakuwa na tabia ya kukimbia au kujificha ili wasipewe majukumu au kuongezewa majukumu.

Hii unaweza kuwa ulishakutana na watu ambao wanatumwa kufanya kazi sehemu fulani na kwa bahati nzuri kazi hiyo ikafanikiwa kuisha mapema, watakachokifanya ni kusema kwamba bado wanaendelea na kazi ili isijulikane kwamba kazi imekwisha ili waweze kwenda kumhudumia mteja mwingine. 

8. Kutia aibu watu wengine
Kwa sababu hawa watu wanakuwa hawajiamini hivyo wanachofanya ni kujaribu kuwaaibisha watu wengine. Hupenda kuwa katikati ya watu wanaofanya sana kazi ili kuweza kuwadhalilisha wale wengine kwa kujaribu kuwachafua au kuwadhalilisha kwamba wana utendaji mbovu. Ukweli wanajaribu kupambana na ukosefu wa kujiamini ndani yao wenyewe. 




9. Kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya Kijamii
Hawa watu wanaitwa walevi wa mitandao, kama uliwahi kuona watu ambao muda wote wanatumia kwenye televisheni bila kuchoka. Vile vile na watu ambao hawajafanikiwa na wala hawataweza kufanikiwa wanatumia muda mwingi mwenye mitandao bila kufanya kitu cha maana. Muda wanaotumia kwenye mitandao hawajui kwamba unaingiliana na malengo na utendaji kazi zao kwenye maisha yao binafsi. 

10. Usumbufu wa chini chini na Usaliti
Tabia hii inakubidi uweke kichwani mwako wakati mwingine unapohisi kusalitiwa na mtu, je ulishawahi kupitia hali ya kwamba mlikuwa mnajaribu kufanya jambo pamoja halafu jambo limepotea juu juu au kujikuta limefanyika sehemu nyingine kabisa bila ya wewe kujua?

Ukweli watu ambao hawana furaha na hawajafanikiwa hawatapenda kuona umefanikiwa hivyo wakati mwingi watataka kusaliti mipango na miradi yako ili usifikie malengo huku wakija na sababu lukuki kwanini imetokea hivyo.

Monday, 21 March 2016

NAFASI KIBAO ZAKAZI

Fuata link hii http://www.kijiwe.co.tz/2016/03/46-jobs-at-mwalimu-julius-k-nyerere.html

FAIDA 11 ZA KUNYWA MAJI YENYE NDIMU



Umesikia mara nyingi kuwa kunywa maji kwa wingi hasa asubuhi kuna faida kubwa sana za kiafya mwilini,lakini kunywa maji yenye ndimu na vuguvugu kuna faida maradufu na ni rahisi kufanya kila siku. Vitamin C nyingi iliyomo katika limao na ndimu ni siri ya faida za tunda hili,ukiachia vitamini C ndimu ina vitamini B-complex, madini ya Kalsiamu, chuma, magnesiamu na potasiumu, na fiba (Ndimu ina potasiumu kwa wingi kuliko tofaa(apple) au Zabibu).


Kunywa maji peke yake (yasiyo na kitu) wakati wa asubuhi huwapa tabu baadhi ya watu,wengine hupata kichefuchefu . Lakini maji yaliyotiwa ndimu kidogo huwa na radha nzuri zaidi na watu wote wanaweza kunywa bila shida.


Kuna faida nyingi ambazo utazipata kwa kunywa maji yenye ndimu au limao na katika makala hii tunazitaja faida 11 muhimu.


FAIDA #1: HUCHOCHEA MMENG’ENYO WA CHAKULA TUMBONI


Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula. Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.


Pia maji ya uvuguvugu husaidia kusawazisha utumbo uliojikunja na kutoa mawimbi tumboni na kufanya chakula kusukumwa vizuri.
FAIDA #2: HUBORESHA KINGA ZA MWILI


Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili.
FAIDA #3: HUSAIDIA UNYONYWAJI WA MADINI MWILINI


Vitamini C iliyomo katika limao husaidia kunyonywa kwa madini mwilini hasa madini ya chuma ambayo ni muhimu kwa utengenezaji wa damu. Hata kama maji ya ndimu yakiwa baridi.
FAIDA #4: HUSAIDIA KINGA DHIDI YA SARATANI


Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicalsmwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).
FAIDA #5: HUSAIDIA KUPUNGUZA HATARI YA KIHARUSI


Kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao(citrus fruits) inasaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya ischemic(ischemic stroke) hasa kwa wanawake.



FAIDA #6: USAFISHAJI WA MWILI NA DAMU


Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.
FAIDA #7: KUREKEBISHA SUKARI KATIKA MWILI


Limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili.


Hii inawasaidia sana wagonjwa wa kisukari katika ulaji wao.
FAIDA #8: DAWA YA KIKOHOZI NA MAFUA


Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili.
FAIDA #9: INASAIDIA UREKEBISHAJI WA NGOZI NA KUPONA MAKOVU


Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.


Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.
FAIDA #10: HUSAIDIA KUPUNGUA UZITO


Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.
FAIDA #11: KUONDOA HARUFU YA MDOMO


Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya.


Ni zoezi rahisi na haraka kabisa, weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.


Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.



MWANDISHI ALIYETEKWA AELEZA YALIYOMKUTA: HAYA HAPA



Taarifa fupi toka Mwanahabari Salma Said



Nitaeleza kwa ufupi sana kwa kweli ni unyama na uhuni mkubwa niliofanyiwa ilikuja gari pale airport wakati nikisubiri gari yangu na kuniingiza kwa nguvu katika gari na kunipeleka sehemu wakanifungia na kunipiga sana kisha wanaondoka wanarudi tena wananipiga tena kwa hivyo machungu juu ya machungu maumivu makali sana hawakuwa wanachagua mateke vibao uso ulivimba sana waliponiona pumzi zishanibana nahangaika ndio wakafunga mlango wakatoka nje wakaniacha mpaka asubuhi wakaja tena wakawa wananipiga tu na kusema maneno yao ya vitisho kumbe kosa langu kubwa ni kuandika habari za Mazombi wakinambia najifanya mwandishi na mtetezi wa haki za wanyonge huku wakinipiga na kuniahidi hawataniachia mpaka Dk Shein atakapotangazwa, Na jana ndio wakanirejesha kule kule waliponichukua karibu na kituo cha Taxi cha airport wakiwa wamenifunika uso na kunitupa tu saa 11.30 Alfajiri nilipojifunua ndio nikajikuta nipo hapo nikajiburura hadi kituoni nikaongea na mama mmoja hapo anisaidie akanambia kaa chini mwangu akawa ananiliwaza ndio baadae nikachukua taxi kwenda Aga khan hospitali daktari wangu hakuwepo ikabidi niende Regence Hospitali tokea asubuhi hadi hiyo saa 10 alipokuja Onesmo kunichukua na kwenda polisi kuweka taarifa na kuhojiwa hadi saa 4 usiku. Simu yangu muda mwingi nilikuwa nayo mwenyewe na ndio siku ya mwanzo nilipoongea walipikuja wakanipiga sana sana na muda mwingine simu wakaizima ila hawakuichukua na hawajachukua chochote kwa kuwa walisema shida yao nisiripoti uchaguzi tu
0777 Namba ya Salma Saidi Mwanahabari alietekwa Na kuteswa.

WANAFUNZI WANAJISIWA MOSHI: NI MAAJABU YA KARNE YA 21

Watoto wanne wa kike wenye umri wa miaka nane, wamebainika kubakwa na kunajisiwa kwa karibu mwaka mmoja huku vijana wawili wanaowafanyia vitendo hivyo wakiwalipa Sh500 kila mmoja.

Habari zinasema watoto hao wanaosoma darasa la tatu katika shule ya msingi ya Msaranga katika Manispaa ya Moshi, wamekuwa wakienda kufanyiwa vitendo asubuhi kabla ya kuingia darasani.

Uchunguzi wa madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa Kilimanjaro ya Mawenzi umethibitisha watoto hao kuingiliwa sehemu za siri na kunajisiwa na pia wameambukizwa magonjwa ya zinaa.

Watoto hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo kati ya saa 12:30 na saa 1:30 asubuhi na baadae hutakiwa kurudi saa 4:00 wakati wa mapumziko ili kuchukua Sh500 kama malipo ya kazi hiyo.

Tukio hilo ambalo limeibua hasira za wananchi, linafanana kwa kiasi na lile la mwanamuziki Nguza Viking “Babu Seya” na mwanae Jonson Nguza “Papii Kocha” wanaotumikia kifungo cha maisha jela.

Wanamuziki hao raia wa Congo walihukumiwa kifungo hicho mwaka 2004 kwa tuhuma za kubaka na kunajisi watoto 10 wenye umri wa miaka 6 na 8 wa shule ya msingi Mashujaa ya Jijini Dar Es Salaam.

Mzee Alex Massawe (sio jina lake halisi), mkazi wa Msaranga mjini Moshi, alisema kuwa Jumatano iliyopita, alishuku mwenendo usio wa kawaida wa mjuu wake mwenye umri wa miaka nane.

“Ilikuwa kwenye saa 12:30 au saa 1:00 asubuhi nilikuwa natoka misa ya asubuhi nikakutana naye anavuka na wenzake wanavuka barabara kwenda upande tofauti na ilipo shule,”alisema mzee huyo.

“Nilipomuuliza unaenda wapi akasema mwalimu amewatuma madekio lakini nikamuona anatetemeka. Nikamwamuru arudi shule mara moja. Mie nikaendelea na safari yangu lakini roho inakataa”.

Mzee huyo anasema saa 2:00 asubuhi siku hiyo hiyo akarudi shuleni kwa lengo la kukutana na mwalimu mkuu lakini akakutana na mwalimu wa zamu na kumweleza mashaka yake.

Kwa mujibu wa mzee huyo, mwalimu wa zamu aliahidi kuchunguza jambo hilo, lakini siku hiyo mjukuu wake aliporudi nyumbani alimuuliza na baada ya kumchapa kidogo akaeleza kila kitu.

Siku iliyofuata mzee huyo akarudi shuleni na kumweleza mwalimu mkuu taarifa zile ambaye aliita walimu wenzake na kumwita mtoto huyo na kumuuliza kama ni kweli alichoeleza babu yake.

“Mwalimu mkuu akamwambia usiposema ukweli nitakuadhibu ndio akasema kuna wavulana fulani wanaendaga kwao kufanya hayo mambo na akawataja wenzake watatu ambao huendaga nao,”alisema.

Mlezi huyo alidai mbele ya walimu alieleza kuwa huwa wanakwenda huko asubuhi na kufanyiwa ufirauni huo kwa zamu katika chumba kimoja halafu hutakiwa kurudi saa 4:00 kuchukua Sh500.

“watoto wawili akiwemo huyu mjukuu wangu walikiri na kuwataja kwa majina hao vijana na kutueleza fulani huwa anatufanya mbele na fulani anatufanya nyuma. Wawili waligoma kueleza,”alisema.

“Wakatuambia saa 4:00 wakati wa break (mapumziko) ndio wanaenda kuchukua hiyo mia tano mia tano halafu siku zingine hurudi saa 8:00 mchana kufanya mambo hayo kadri wanavyokubaliana”.

“Hivi tunavyoongea nimekosa usingizi siku zote hizi. Sina amani moyoni. Najiuliza maswali mengi ambayo nakosa majibu. Kwanini ushetani huu kwa watoto wadogo kama hawa?”alihoji mzee huyo.

Mtoto huyo alipoulizwa, alieleza maelezo yanayofanana na ya babu yake na kuwataja kwa majina vijana hao, mmoja jina lake likianzia na herufi J na mwingine jina lake likianzia na herufi W.

Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa, alilithibitishia kuwapo kwa tukio hilo na kueleza kuwa tayari polisi wamemtia mbaroni mtuhumiwa mmoja wa tukio hilo.

“Ni kweli kuna shauri hilo limefunguliwa na tayari tumemkamata mmoja wa watuhumiwa na tunaendelea kumtafuta mwingine anayetajwa na watoto hao,”alisema Kamanda Mtafungwa.

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...