Showing posts with label JAMII NA SIASA. Show all posts
Showing posts with label JAMII NA SIASA. Show all posts

Friday, 16 June 2017

Uzalendo wa “Itikadi” Binafsi kutumia Mgongo wa Maslahi ya Jumla ya Taifa



Kuna kitu kimoja kimeendelea kwa muda mrefu sasa na si ajabu tangu tupate Uhuru wetu nacho chaendana sambamba na jinsi Chama Tawala (TANU/ASP mpaka sasa CCM) ambapo kuna nguvu kubwa sana za muonekano wa kutetea na kulinda maslahi ya Taifa lakini kila mwaka na kila awamu mpya, udhahiri wa Maisha ya Mtanzania bado uko pale pale na hauendani na “uendelevu” wa vitu vionekanavyo kwa macho (Majengo ya Kisasa, Majumba, Magari ya Kisasa, Miundombinu, Uwekezaji) na kusadikika ni kwa manufaa ya Taifa. Aidha kuna uendelevu mwingine wa ukuaji wa maslahi binafsi wa watendaji na wapambe wa Viongozi wakuu wa nchi.

Natafakari sana jinsi gani Awamu ya Tano inavyojikita katika kutoa sifa na hoja za uwasili na utimilifu wa Safari mpya ya Maendeleo ya Tanzania na nguvu kubwa inayotumika kurembesha na kusifia mipango na “matokeo” ya umakini wa utendaji wa Awamu ya Tano hasa Rais Magufuli n ahata uwepo wa vikundi na mikakati ya vitisho na ukware wa hoja na matendo kwa wale wanaohoji au kupinga “kazi safi” ya Awamu ya Tano.

HIli limenirudisha miaka yangu ya kupevuka, mwisho wa awamu ya kwanza wakati Malimu Nyerere alipoachia ngazi na kumpisha Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi, Mzee Ruksa. Kisha najikuta namtazama Mzee wa Uwazi na Ukweli, Mstaafu Benjamin Mkapa na miaka yake 10 ya utawala.Ukigeuka kwa Mjomba wa Msoga, Mheshimiwa Jakaya Kikwete, nako kwenye Ari,kasi, nguvu mpya, Maisha bora kwa kila Mtanzania na komeo la Big Result Nowbado kuna ufanano mkubwa wa wapambe na wauza propaganda, dhidi ya wanaohoji na kupinga mambo yaliyofanywa na awamu zote hizi.

Lakini kuna common denominator ya awamu zote hizi nne, unono wa ghafla wa maslahi wa wapambe na watendaji wa karibu wa marais wetu hawa wanne.

Pima sera za “kitaifa” zilizoletwa na Marais wote hawa wanne, mfumo wa propaganda na ulinzi wa hali ya juu wa hoja, mipango, maamuzi n ahata matokeo ya kila kilichowekwa kuwa ni msingi mkuu wa awamu na dira ya Rais. Angalia kwa kina jinsi gani Chama CCM ambapo kwa namna moja au nyingine, kimekuwa mstari wa mbele kunadi kwa Watanzania hizi Sera n ahata ukikitazama Chama, unaona kinaneemeka kwa uharaka sana.

Je propaganda hizi za kuuza seraza Rais ni mfumo mwingine wa kujichumia kwa wale washauri wa karibu wa Marais wetu?

Naangalia enzi za Mzee Mwinyi na wale walionufaika na kutajrika. Mkapa pale alipojiuzia mgodi na mawaziri wake wawili wakubwa wa usimamizi wa uchumi wa nchi walivyopatikana na “hatia” an kufungwa. Hata kwa Kikwete si watendaji pekee, bali wapambe na tuhuma dhidi ya familia.

Sasa hivi, tunaona shaping up ya wapambe ambayo inajijenga kimfumo wa kiutawala kwa kuegemea Ukanda na mamlaka ya kidola huku nchi nzima tukilazimishwa tuamini kuwa tunanyooshwa. Lakini angalia miradi yote mikubwa n ahata matumizi mengine ambayo yamekiuka taratibu.

My point is, kukosekana kwa mfumo imara wa uwajibikaji wa kuleta uwiano wa Check and Balances, na Zaidi kukosekana kabisa kwa udhibiti wa muingiliano wa maslahi- conflict of interest, kunatufanya tuendelee kuimanishwa utendaji kwa manufaa ya Taifa ilhali ni maslahi binafsi yanayojengewa mazingira wezeshi.

Siwatupii lawama za moja kwa moja (direct) marais wetu, ila kutokana na awamu zao kuendeleza mfumo ambao unapinga kwa nguvu zote uwazi, uwajibikaji na utawala bora, tutakapomaliza awamu ya tano, tutajikuta pale pale tukiwa na Masihi mpya wa kuwaaminisha Watanzania kuwa yeye ndio mwenye uchungu wa kweli dhidi ya kero zinazolea umasikini, ujinga na maradhi.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya ‘asikamatwe mtu kwa show off’ – Waziri Simbachawene

Habari

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kutotumia mamlaka yao vibaya ya kuwaweka ndani viongozi,watumishi wa umma na wananchi wengine kwa uonevu kwa kisingizio cha sheria kuwapa mamlaka hayo.





Kauli hiyo ya Waziri Simbachawene ameitoa leo bungeni ikiwa ni baada ya wabunge kuhoji uwepo wa baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kutoa amri ya kukamatwa kwa watu bila sababu ya msingi hivyo ni hatua gani serikali inachukua dhidi yao kukomesha tabia hiyo.

“Ni kweli sheria hii ya mikoa inatoa mamlaka ya kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuweza kumkamata mtu katika mazingira ambayo wanaamini kwamba mtu huyo ama anatenda kosa la jinai ama kwa ufahamu wao ametenda kosa la jinai ama anatenda kitendo chochote kinachovunja amani na utulivu ama anaona mtu huyo anatarajia kutenda au kuhatarisha amani hiyo ndiyo tafsiri ya sheria waliyopewa.”amesema waziri Simbachawene.

Akiendelea kusisitiza amesema licha ya sheria kuwapa viongozi hao mamlaka hayo wanapaswa kuwa makini wanapoitumia sheria inavyotamka kwa kuzingatia mipaka yao ya kazi katika kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa.

“Mtu yeyote anayo haki ya kuomba mtu mwingine ambaye anaweza kutenda kosa la jinai dhidi ya mtu fulani au watu fulani kuomba wakamatwe kwa hiyo haki hii sio tuu wamepewa hawa peke yao…. isipokuwa tuu cha msingi ni pale tuu ambapo inapaswa kutumika kwa kuzingatia sheria mtu huyo awe anamatarajio ya kupelekwa mahakani immediately baada ya kukamatwa na baada ya muda ule kupita asikamatwe mtu kwa ajili ya ku’ Show Off , asikamatwe kwa ajili ya kuonesha kwamba wewe una madaraka lazima akamatwe mtu huyo kama kweli kitendo chake kinahatarisha amani na utulivu na hapa ndipo nataka nisisitize kwamba wakuu wetu wa mikoa na wilaya kwa kutumia sheria hii wawe makini kwa kutumia sheria hii kama inavyotaka.“amesema Waziri Simbachawene.

Sheria ya tawala za mikoa ya mwaka 1997 sura ya 97 inawapa mamlaka wakuu wa mikoa na wilaya kumweka ndani mtu ye yote kwa muda wa saa 48 ikiwa itathibitika kuna hatari ya uvunjifu wa amani na usalama au mtu huyo ametenda kosa la jinai.

Thursday, 15 June 2017

FANYA HAYA KUZUIA WATU WASIINGILIE MAPENZI YENU

Habari msomaji wetu,
Sio mbaya kwa marafiki wa karibu au ndugu na jamaa kufahamu kushirikiana nanyi katika mapenzi yenu kama vile wakati wa sherehe au msiba. Pia sio mbaya kujuliana hali na kutambulisha mambo ya msingi yanayoendelea katika mahusiano yako wewe na mpenzi wako. 

Hata hivyo kuna wakati watu wengine wa pembeni, wawe majirani, ndugu, wazazi au marafiki wanaweza kuwa ‘sumu’ ya mahusiano yako, hasa pale unapowategemea sana kutoa msaada, maoni au maelekezo katika maisha yako ya mapenzi. Makala hii inaeleza mambo ya msingi unayoweza kufanya ili kupunguza uwezekano wa rafiki, ndugu, jamaa, au wazazi kuwa ‘sumu’ ya mapenzi yako.


1. Udhibiti wa taarifa kwa wengine: 

Kadri unavyoelezea mahusiano yako kwa watu wengine ndivyo unavyowapa nafasi watu kutoa maoni, na hata kudhani kuwa wana dhamana ya kukuelekeza unavyotakiwa kuishi na mwenza wako. Hivyo basi, chukua muda wa kutosha kutafakari na kufanya uchunguzi kuhusu maswala yako ya mahusiano kabla haujaanza kutafuta maoni, ushauri kwa watu wengine. Ni bora ukasoma vitabu, na makala mbalimbali, hususani zihusuzo tabia na maisha ya mahusiano, zitafakari vema ili kuona zinahusiana vipi na unayokumbana nayo katika mahusianao yako.


2. Upekee wa mambo: 

Tambua kuwa tabia ya mpenzi wako inaweza kuwa ni ya kipekee, mazingira pia ya tukio linalokufanya utake ushauri au maoni kwa wengine yanaweza kuwa ni ya kipekee, hivyo ushauri au maoni utakayopokea yanaweza yasikusaidie moja kwa moja katika suluhisho lako. Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo katika mahusiano na kutafuta suluhisho kabla ya kutegemea watu wengine.


3. Mwenye maamuzi ni wewe:

Ni kweli kuwa kuna nyakati ni muhimu kupata ushauri kutoka kwa watu wengine, na zaidi sana watu wenye uelewa sahihi na unaowaamini, hakikisha kuwa unatambua kuwa wewe mwenyewe ndio mwenye kubeba lawama ya maamuzi utakayochukua. 


4. Kuwa na subira:

Usichukue maamuziya haraka katika mahusiano hususani uamuzi wa kuamua kuwashirikisha watu wengine habari ya mambo yahusuyo uhusiano wako. Unapofanya uamuzi wa kuwashirikisha wengine kwa haraka unajinyima nafasi ya kulichunguza jambo kwa ufasaha hususani madhara yanayoweza kutokea kwa kuwaeleza wengine, au kama ni tatizo, basi kufikiria njia sahihi ambazo ungeweza kuzitumia kupata suluhu ya tatizo. 


5. Fungua njia za mawasiliano kati yenu:

Pengine chanzo cha wewe kutaka kuzungumza mambo ya ndani yanayohusu mahusiano yenu kwa watu wengine ni kwakuwa umekosa nafasi ya kuzungumza kwa ufasaha na mwenzi wako. Tafuteni nafasi za kutosha, jengeni mazingira ya kuzungumzia mambo yenu kabla ya kutaka kuwashirikisha watu wengine. 


6. Kuweni peke yenu: 

Hata kama hautaki kueleza watu kuhusu mambo yanayoendana na maisha yenu, mazingira unamoishi yanaweza kuchangia watu kutaka kuingilia mahusiano yenu –kwa kutoa maelekezo, ushauri au maoni kuhusu muishivyo wewe na mpenzi wako. Inapobidi hakikisha hamuishi karibu na wazazi wenu, ndugu au rafiki wa karibu. Au haufanyi kazi na mwenzi wako sehemu moja, kwani hiyo itakuwa njia rahisi sana ya watu kuona mnavyoishi. Inapobidi kuwa karibu na watu wengine , hakikisha mnakubaliana wewe na mwenza wako namna bora ya kuendesha mawasiliano kati yenu mbele za watu, ili msiwape nafasi ya wao kuwa‘soma’ na kisha kuanza waje waanze kutoa ‘maelekezo’ ya vile wanavyoona mnapaswa kuishi.


7. Nenda ‘darasani’ : 

Kumbuka mahusiano yanahitaji sana uelewa mkubwa wa jinsi ya kufanya mawasiliano fasaha, kuelewa hisia za mwenzi wako, kutambua mbinu za kusuluhisha migogoro, na zaidi sana kufanya mipango ya muda mrefu ya uhusiano wenu. Jizoeshe kusoma makala na vitabu mbalimbali vyenye kuboresha ufahamu wa mambo ya msingi kama hayo tuliyoeleza hapo juu.

JEROME NA ANNA

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...