Ujasiriamali ni
neno la kiswahili linalotokana na maneno mawili yafuatayo
1.
Ujasiri 2.
2.
Wa mali
Hii
ina maana ya mtu mwenye ujasiri wa kuwekeza mali alizonazo ili apate faida
Hatua 7 muhimu ili kuwa mjasiriamali kamili
(J7)
1. Jitoe bila woga
na kuwekeza ulicho nacho
2. Jipange (mpango
mkakati)
3. Jipime Ili kujua
uwezo na madhaifu yako
4. Jiwezeshe kwa kupata mafunzo
5. Jihadhari ili usitumbukie kwenye hatari
6. Jitadhmini, jikosoe kwa kujitathmini
7. Jipange upya kwa kufanya maboresho
1.
Jitoe Bila Woga na Kuwekeza Ulicho Nacho.
Maamuzi magumu
yanatakiwa unapotaka kuwa mjasiriamali. mke, mume, wazazi, wajomba ndugu,
marafiki, wakuu wa ukoo wako na hata mazingira yako yanaweza kukataa au kuwa
pingamizi kubwa ili usifanye shughuli za kijasiriamali. Kwa mazingira haya ni
rahisi kukata tamaa na kama hukuamua kutoka moyoni mwako fikra zako za kuwa
mjasiriamali zitaishia hapo na hutakaa ufanye biashara. Kuamua na kujitoa ni muhimu
sana ili uweze kuendelea an maono yako yatakayokukomboa kiuchumi Ili uweze
kujenga himaya yako (ufalme wako) (your kingdom) wa utajiri unahitaji kufanya
maamuzi yako peke yako wala sio ya hao waliotajwa hapo juu japo ushauri kutoka
kwao ni ruksa na utakusaidia kufanya maamuzi bora zaidi. Kujitoa unakusaidia
wewe kuhesabu gharama ya hatari zitakazokuwepo mbele yako kwenye ujasiriamali
wako. Utahitajika saa nyingine kuwekeza mali ya kipekee uliyonayo. kama vile
nyumba, gari, kiinua mgongo nk. Kama wewe ni mwoga hutadhubutu kuwekeza kajumba
kako kapekee eti kwa sababu ya ujasiriamali. Kama kweli ukiamua na kujitoa
maisha yako yatabadilika sana kuanzia siku ile ya maamuzi magumu. Safari ya
ujasiriamali huwa na tabia ya kwenda juu au chini kama meli inayoyokabiliana na
tufani baharini. Unashauriwa kutizama lengo na sio tufani ya bahari. Kama
umeamua kutoka moyoni kuwekeza utafika tu kwenye lengo kuu. Epuka kukopa ili
uanzishe biashara, ni hatari sana. Kusanya vyazo vyako vya mitaji (mali binafsi
)
2.Jipange (Mpango Mkakati)
Weka maono ya biashara yako, unataka kufikia
ngazi ipi kimafanikio. Je unataka kuwa na hoteli kubwa ya kitalii au kiwanda
kikubwa cha kuuza nguo Tanzania au Afrika nzima? Weka na kazi muhimu
utakazozifanya ili kufikia maono husika. Unaweza weka malengo mahsusi kila
baada ya miaka mitatu au mitano. Inashauriwa malengo hayo mahsusi yawe kati ya
3 na 5. Jiwekee malengo ya muda mrefu na muda mfupi. Malengo yagawanywe mpaka
kwenye kazi za kila siku. Jiwekee maadili na tunu za mafanikio. Bila hizi tunu
na maadili huwezi kuyafikia malengo yako. Jiwekee ratiba mbalimbali za
kiutekelezaji bila kusahau kuweka kwenye ratiba shughuli muhimu.
3.
Jipime Ili Kujua Uwezo na Madhaifu yako Kiingereza wanaita SWOT Analysis
Jipime juu ya mambo makuu manne
yaliyogawanyika kwenye makundi mawili
1. Mazingira ya biashara ya ndani
2. Mazingira ya biashara ya nje
AU
1. Mazingira wezeshi
2. Mazingira
hatarishi
Haya makundi mawili
nayo yamegawanyika katika Mazingira ya ndani ni
1. Uwezo wako kibiashara
2. Udhaifu wako kibiashara
Mazingira ya nje ni
1. Fursa zilizopo ili kunufaisha biashara yako
2. Hatari zilizopo
ili kuua biashara yako
Mazingira wezeshi ni kama ifuatavyo
1. Fursa zilizopo
ili kunufaisha biashara yako
2. Uwezo wako kibiashara Mazingira hatarishi
ni kama ifuatavyo
1. Hatari zilizopo ili kuua biashara yako
2. Udhaifu wako
kibiashara unaoweza kuzorotesha maendeleo ya biashara yako
4.
Jiwezeshe kwa Kupata Mafunzo
Jiwezeshe ni hatua inayojibu matokeo ya hatua
ya kujipima ambayo imekuwezesha kugundua madhaifu yako na kuyapatia ufumbuzi
kwa kujiwezesha ambazo mara nyingi ni mafunzo. Udhaifu ni yale mambo ya
kimaarifa usiyoyajua kiutendaji ili biashara yako isonge mbele. Inaweza kuwa ni
ujuzi wa kufuga samaki kama unataka kuanzisha mradi wa kufuga samaki nk.
5.
Jihadhari ili Usitumbukie Kwenye Hatari
Katika hii hatua hakikisha kila uamuzi au
tendo unalofanya halitakuingiza kwenye hatari kubwa usiyoweza kumudu bali
inakuweka kwenye changamoto ambazo unazimudu. Kingereza wanaita (Moderate Risk).
Usijaribu kufanya biashara zenye hatari kubwa na ya uhakika. Usijaribu kuingia
ubia/ushirika na watu ambao unawajua ni hatyari kwa biashara zako. Usijaribu
kuingiza teknolojia kwenye biashara yako ambayo una uhakika kuwa sio rafiki.
6.
Jitadhmini,
Jikosoe kwa Kujitathmini. Fanya tathmini za
mara kwa mara ili kujua kama unakwenda sawasawa na makusudio ya mwanzo. Fanya
tadhmini ndogo kila baada ya nusu mwaka, na tadhmini kubwa kila baada ya miaka
mitatu.
7.
Jipange Upya kwa Kufanya Maboresho
Matokeo ya tadhmini yatumike kama msingi wa
kujipanga upya na kufanya maboresho makubwa yatakayoitoa biashara yako kutoka
kwenye ngazi moja ya mafanikio kwenda ngazi ya juu zaidi ya mafanikio. Tumia
matokeo ya tadhmini zote mbili kujikosoa na kufanya maboresho yenye lengo la
kujibu kasoro zilizoonekana kwenye ripoti ya tadhmini.
Karibu tuendelee
kujifunza zaidi
Mmassy
Jerome-Arusha,Tanzania
No comments:
Post a Comment