Tuesday, 25 April 2017

NDOA YAKE, KIFO CHAKE. HEART TOUCHING STORY


Ilikuwa ni Jumamosi tulivu, sikuwa na kazi nyingi sana. Siku hiyo nilikuwa na miadi na mmoja wa wateja ofisini kwangu kituo cha msaada wa Kisaikolojia HT&L CLINICAL THERAPY.

Mteja wangu alikuwa akiitwa Claudia (sio jina lake halisi). Alikuja kwangu na kulalamika ni kwa jinsi gani amegundua kuwa mumewe sio muaminifu na anatoka nje ya ndoa.

Alikuwa anahisi kusalitiwa mno na alikuwa amechanganyikiwa, alikuwa akinielezea hali jinsi ilivyo huku akitokwa na machozi. Nilijitahidi kumpa moyo na kumueleza kuwa haya yataisha.

Nikamuomba anipe namba ya simu ya mumewe na nikamuahidi kukutana na wote, yeye na mumewe tuweze kupata suruhisho la matatizo ya ndoa yao. Pia nikamhakikishia kwamba kwa Neema ya Mwenyezi Mungu amani itarudi ndani ya ndoa yao.

Baada ya wiki moja niliweza kuwasiliana na mumewe na hakuwa mkaidi alikuja ofisini kwangu na tukawa na 'session' pamoja yeye pamoja na mkewe. Baada ya maongezi ya kirafiki, alikubali kwamba ni kweli anao mchepuko. Na amekuwa akichepuka mara kwa mara.

Alimtupia lawama zote mkewe na kuniambia kwamba haya yote mpaka yeye kuchepuka nje na kutojali ndoa yake amesababisha mke wake mwenyewe.

Akaniambia matatizo yalianza pale dada wa mke wake yaani shemeji yake alipokuja kuishi nao. Walikuwa na ndoa changa ndio kwanza ikikuwa. Kwa maneno yake alinisimulia;

" Tulikuwa tumepanga chumba kimoja tu, na niliona si vema huyu shemeji yangu nae awepo kwenye chumba kidogo kama kile"

"Tulikua tunahitaji muda mrefu kidogo tukiwa peke yetu ili kujenga ndoa yetu changa bila kuingiliwa na ndugu au mtu yeyote, hivyo dada wa mke wangu alitunyima kabisa uhuru wa mimi na mke wangu kuwa pamoja"

"Shemeji yangu, yaani dada yake na mke wangu alikuwa anao uhuru wa kupitiliza, aliingia tunakolala na mke wangu, alikuwa akilala kitanda chetu muda wowote anapojisikia na alikuwa haniheshimu hata kidogo hata mbele ya mdogo wake"

"Na kila nilipokua nikimueleza mke wangu juu ya tabia za dada yake na kumsisitizia amwambie arudi kwao, mke wangu alinijia juu na kuniambia nina mdharau ndugu yake, na kama anataka aondoke basi na yeye ataondoka"

"Nilichanganyikiwa kwa kweli, shemeji yangu alikuwa na kiburi, kila nikimueleza arudi nyumbani kwao hakunisikia, nilishangaa mno kwa nini alikua aking'ang'ania kukaa nasi kwenye chumba kimoja na huku ndoa yetu ikiwa ndio kwanza ipo changa"

"Mara ya mwisho mimi kumgusia hilo suala, ilikuwa ni siku ambayo mke wangu aliniambia mbele ya dada yake kwamba dada yake hataenda sehemu yoyote. Sikuweza kuvumilia, ukizingatia nilikuwa nimekaa kama miezi miwili hivi bila kushiriki tendo la ndoa."

Sikuweza kuvumilia kwa kweli, nilivaa viatu vyangu nikatoka. Sikuwa na uelekeo maalumu, nilizunguka zunguka tu mpaka nikafika Bar fulani iliyo nje ya mji kdogo. Nilikaa katika hiyo Bar nakuanza kunywa bia, pembeni yangu alikaa dada mmoja ambae alikuwa mrembo kweli"

"Nilimkaribisha mezani kwangu, tulikunywa sana bia pamoja na baadae nikachukua chumba pale pale maana Bar ilikuwa na vyumba pia. Niliingia nae na nikafanya nae mapenzi"

"Na hapo ndipo nilipoanza kuchepuka, yule dada niliyekuatana nae pale Bar alikuwa akiitwa Diana (sio jina lake halisi). Na alikuwa akiishi bagamoyo. Tukatokea kupendana sana. Nikawa nikisafiri kwenda Bagamoyo. Mara nyingi nilichelewa kurudi nyumbani au siku nyingine nikawa sirudi hata siku mbili tatu hata wiki" Mume wa yule dada alinipa hayo maelezo yake.

Kwa kufupisha story, baada ya kumsikiliza huyu mume japo mke alikuwa amepanick, mimi niliongea nao maongezi ya kina, niliwaonesha maandiko ya Mwenyezi Mungu yanasema nini juu ya Ndoa na nikawaeleza hasara za yeye mume kuendelea kuchepuka, huku akiacha mkewe wa ndoa. Pia nikampa mbinu za kufanya ili shemeji yake aweze kuondoka pale nyumbani kwake.

Mke nae nilimueleza umuhimu wa mume wake hasa kipindi hiki ndoa ikiwa bado changa na ikihitaji jitihada za wote wawili. Na kumsisitizia aruhusu dada yake aondoke.

Walinielewa na nilifurahi kwa kuwa mume aliniahidi kurudi kwa mkewe na kuendeleza ndoa yao changa.

Ndugu msomaji, kama mchekeshaji maarufu hapa Tanzania Mjuni Mpoki alivyoimba katika kibao chake kimoja kwamba "Mapenzi yana nguvu kuliko hata breakdown." msemo huo ulijidhihirisha kwani yule mume, baada ya kukaa siku chache tu na mke wake alirudi Bagamoyo kwa mchepuko wake, ingawa shemeji yake yaani dada wa mkewe aliondoka na kuwaachia uhuru.

NA NDIPO JANGA LILIPOTOKEA!

Usiku mmoja mkewe ambae alikuwa na pumu (asthma) akiwa peke yake, wakati bwana mkubwa yupo kwa mchepuko wake Bagamoyo, pumu ilimbana sana, Blood pressure (BP) ililuwa juu, sauti haikuwa inamtoka, alihangaika sana na mwishoe akafariki kutokana na hiyo attack (shinikizo)

Ndio alifariki kifo cha maumivu mno pasina msaada wowote, aheri hata angalikuwepo mtu yeyote ndani huenda angaliweza kutoa msaada wa haraka wa kumuwahisha hospitali!

_____________________________________________

Sote tunapaswa tujifunze kuweka ndoa zetu au mahusiano yetu mstari wa mbele, panapokuwa na mapenzi ya kweli na heshima kwa kila mmoja wetu, hali kama hiyo hapo juu haiwezi kujitokeza na hata ikitokea basi huamuliwa kwa busara na matokeo hua ni chanya. Sio hasi kama yaliyotokea katika simulizi hapo juu.

Sasa tusemeje?

- Je Mwanamke alijisababishia kifo chake mwenyewe?

- Mume wake ndio alikuwa chanzo cha kifo chake?

- Ni kweli mke wake alipaswa kulaumiwa kwa yeye kuanza kuchepuka?

- Au tumlaumu dada mtu kuja kukaa kwa shemeji yake na huku akijua wanaishi chumba kimoja tu?

Toa maoni yako hapo chini.

Ndoa sio mchezo, ndoa sio masihara, if you mess up with marriage it might be the way to your grave. Be wise and pray to God.

WANAUME MNAOTAKA KUOA NA MLIOOA TAYARI



Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara.

Yote hayo ni ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Wekeni wivu pembeni na Yafuateni haya;

1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.


2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia "Mimi ni mume wa mtu" au ninae mtu tayari.

3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, "wanawake wamaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao"

4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!

5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.

6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!

7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.

8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!

9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc

10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.

"Being a male is a matter of birth, being a man is a matter of age, but being a gentleman is a matter of choice. A best choice indeed!"

MAHUSIANO..........


Mahusiano ni suala tata sana kuliko hata kutafuta pesa, pesa ni rahisi sana kuzitafuta panapo utulivu wa ubongo na pasipokuwa na mgogoro wa nafsi.
Wanawake siku zote huuliza, "Nitajuaje kama huyu ni mwanaume bora kwangu na aliye ndoto ya maisha yangu?"
Jibu langu siku zote litakuwa hili, wanaume hutofautiana sana kutokana na malezi waliyopitia, aina ya maisha, influence ya marafiki, etc.
Hata hivyo kuna mambo ya kawaida ambayo kama mwanaume uliyenae hayatimilizi, kunaweza kuwa na tatizo.
1. Mwanaume bora huihudumua familia yake, mwanaume ambae hata kuhudumia familia ni mtihani hilo ni tatzo, mwanaume ambae hata kumnunulia mwanamke wake mafuta, nguo, viatu au kitu chochote kidogo hawezi huyo hawezi kuwa bora.
2. Mwanaume aliye sahihi kwako hukufanya wewe mwanamke uwe bora, hukupatia maono yake, hukueleza ndoto zake, hupata tabu sana endapo utakua katika hali ya sintofahamu.
3. Mwanaume asiye bora kwako, huwa mpole tu pale anapotaka kufanya mapenzi na wewe, ikifika hatua hii hujishusha na siku hiyo hua karibu na wewe sana, na baada ya kufanikisha hurudi katika hali yake ya kawaida mpaka msimu mwingine wa Sex unapokaribia. Sex pekee haiwezi kujenga Ndoa.
4. Mwanaume asiye sahihi kwako hawezi kukueleza mipango yake, hana Mungu ndani yake, anathamini marafiki zake zaidi yako, huthimini pombe kuliko kitu chochote.
5. Hawezi kukuchukua na kukupeleka Lodge au ghetto kwake tu, bali hukupeleka na kukutambulisha kwa wazazi wake, ndugu na marafiki, ukiona hataki kukutambulisha hapo shtuka, anapitisha muda tu kwako.
6. Siku zote Hatakumbuka ni lini Period yako inaanza na itakua kwa muda gani pekee bali atakumbuka pia siku yako ya kuzaliwa, na kukumbusha mipango ambayo mmeipanga ili muweze kuitumiza.
7. Hatakukumbusha ni lini mnatakiwa kukutana kwa ajili ya kufanya tendo la ndoa bali pia atakukumbusha kusali na kufunga ili muweze kurithi kwa pamoja ufalme wa Mungu.
Unahitaji mwanaume mwenye mawazo ya kina, mwanaume mwenye hofu ya Mungu, Mwanaume anaeweza kukupa kitu fulani katika maisha yako mbali na kukaa lisaa limoja kwenye tendo la ndoa.
Hata hivyo baadhi ya wanaume wasio na hofu ya Mungu hu 'pretend' baadhi ya mambo alimradi ampate mwanamke na kuzini nae, Ni vema na busara mwanamke akawa na Mungu ili Mwanaume amtafute kwanza Mungu ndipo awe na wewe.
"A real man can't stand seeing his woman hurt. He is careful with his decision and actions, so he never has to be responsible for her pain."

Endelea kufuatilia makala kadha wa kadha kupitia blog yako hii pendwa

MSICHANA SOMA HAPA,ISIKUPITE



                                          Barua kwa wasichana wote

Dear Ladies

Sio kila mwanaume ni Husband material. Baadhi yao wanafaa kuwa marafiki tu, baadhi yao ni boyfriend materials, sex mate materials,baby papa materials, husband materials na wengine ni husband materials.


Olewa na mwanaume ambae ni Kaka bora, mume bora na baba bora. Baadhi yenu huingia ktk ndoa na wanaume ambao kimsingi hawakua na nia ya kuoa.

Ndoa si kwa kila mtu. Baadhi ya wanaume kimsingi hawajawa tayari na majukumu ya ndoa. Kamwe usiruhusu kiu ya ndoa au msukumo wa marafiki na wanajamii kwa ujumla ukusukume kuingia mikononi kwa mwanaume ambae hayuko tayari na ndoa (matrimony).

Tizama kwa makini, wanaume wengi huoa kwa sababu ya status. Hawa ndio huoa na kuwachia mama zao na baba zao wawatunzie wake zao.

Namaanisha nini?

Usikubali kuolewa kwa nadharia, ndoa njema lazima ihusishe vitendo vyenye kuleta uhai wa ndoa. Baadhi ya wanaume ni wabinafsi sana, Chukua hii kutoka kwangu mwanaume mbinafsi hawezi kuwa mume bora.

Ndoa huchanua pale panapokua na muingiliano wenye kuleta manufaa, humea pale panapokua na give-and-take situation.

Usiolewe na mwanaume kwa kuwa una mimba yake.
Usiolewe na mwanaume kisa anakufurahisha.
Usiolewe na mwanaume kwa sababu huna ajira.
Usiolewe na mwanaume kwa sababu umekua nae ktk uhusiano kwa muda mrefu.
Usiolewe na mwanaume kwa sababu umejiwekeza kwake kiuchumi

OLEWA nae kwa sababu umemchunguza kwa makini na umejiaminisha kwamba anafaa kuwe mume bora na baba bora wa watoto wako.

Wanaume wapo kila mahali, ila waume bora niwachache sana.

Nakuombea wewe ambae bado hujaolewa kwamba hutakabiliwa na ndoa yenye majeraha. Na kwa wale ambao wanajuta kufanya makosa ya kuchagua na wapo ktk majeraha mazito, Mungu aingilie kati ndoa zenu.Mungu wetu ni muanifu, atatenda vile aonavyo yeye ni vema!

SOMA HAPA UELIMIKE KUHUSU NDOA



                                      NDOA NI KAZI NGUMU,HAIHITAJI MCHEZO!!!

Nimezoea kutafsiri kwamba "ndoa sio kwa ajili ya wavulana wadogo" nikimaanisha wavulana wadogo kiumri, ni mpaka pale nilipomtembelea bibi mshauri wa masuala ya mahusiano aliyedumu ktk ndoa kwa miaka 47.

Nilimuuliza nini siri ya mafanikio ya ndoa yako kudumu miaka yote hiyo 47? Alijibu binti yangu, matarajio unayoyaweka juu ya ndoa yako yanweza kuharibu au kustawisha ndoa yako. Niliolewa na mume wangu bila ya matarajio ya kufurahia pesa na utajiri wake, au kuninunulia motokaa.

Ila kadiri muda ulivokua ukisonga, uvumilivu wangu, uchapaji kazi, hofu ya Mungu vilipelekea kupata utajiri, nyumba kadhaa, watoto wenye afya na mengineyo

Unaona? Kama mwanamke utaendelea kulalamika ndani ya nyumba, unasukumua spirit ya mwanaume kutofurahia uwepo wake nyumbani, kama hutamfurahisha mumeo unatengeneza nyumba isiyotawalika.

Hivyo basi niliolewa pasina matarajio makubwa sana, ila nilijitahidi kumtengenezea furaha siku zote kadiri nilivyoweza. Kwa miaka yote 47 nimekuwa wa kwanza kuamka na wa mwisho kwenda kulala.

Naogesha watoto, nawaongoza ktk sala, naandaa breakfast kwa ajili ya mume wangu na watoto na kumchemshia maji ya kuoga, namnyoshea nguo za kazini, namkiss na kumtakia heri kazinj na mizunguko yake yote ya siku.

Nikamuuliza bibi, kwa kufanya hayo yote ulikuwa unapata mrejesho gani mzuri toka kwa mumeo? Akacheka na kuniambia; unaona! Hili ndio tatizo kubwa nyie mabinti wa siku hizi katika ndoa. MNAFANYA KITU KWA KUTEGEMEA NAWE UTAPEWA FADHILA KUTOKA KWA MWENZI WAKO. Hiyo sio sahihi. Kama tabia ya kumhudumia mpenzi wako ikijijenga, naturally utapata mrehesho kutoka kwa mwenzako.

Akaendelea, binti yangu kamwe usifikirie kuhusu utajiri au umasikini wa nyumbani ulikotoka na ukafananisha ktk ndoa yako. Hata hivyo umejua kabisa status ya familia yako na ukaamua kuoa au kuolewa na huyo mtu. Mapenzi ndio huvutia wawili kuingia ktk ndoa, ila si mapenzi pekee bali ni uelewa, uvumilivu, mawasiliano na muhimu zaidi n msamaha.

Matarajio makubwa ktk ndoa ni dalili ya kuvunjika kwa ndoa mapema. Muda mwingine utasikia nataka kuolewa/kuoa na mfanyabiashara, tajiri, mpole, asiye na dosari etc...huwezi kuvipata vyote hvyo kwa mtu mmoja ila kulingana na muda unaweza ukamtengeneza. Punguza matarajio makubwa.

Mambo haya yafuatayo yaepukwe kwa gharama zozote na wanandoa!

1) Kamwe usiseme umemtengeneza mumeo au mkeo from nobody ti somebody. Inaumiza. Mungu amekutumia wewe kama wakala tu wa kumbadilisha. Mpe utukufu yeye.

2) Muache mwanaume awe kichws cha nyumba, na wewe mwanamke kuwa roho ya nyumba huku ukitumia ulimi wako vizuri!

3) Tendo la ndoa ni chachu ya kuimarisha ndoa, jitahidi kuwa romantic kwa mwenzi wako.

4) Mtegemee zaidi Mungu kudumisha ndoa yako na si wanadamu katika kutatua migogora ya hapa na pale

5) Mwanamke usitumie muda mwingi kuweka make up ya mwili wako, bali make up ya tabia zako ndio ipewe kipaumbele.

Fanya kila jitihada kufanya ndoa yako idumu na Mungu atusaidie.

Amen.

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...