Kanuni
za ujasiriamali zinaweza kusomwa au kufundishwa na mtu akaelewa na
kuzifuata,lakini tabia zingine hazifundishiki
hizi ni zile tabia ambazo mtu anazaliwa nazo. Kila binadamu anauwezo tofauti
katika kufikiri,kufanya maamuzi,kufanya kazi kwa bidii,tofauti hizi ndizo
ambazo haziwezi kufundishika. Jambo la kutia moyo ni kwamba tabia ambazo
zinafundishika ni muhimu sana kwa mjasiriamali au mtu yeyote anayetaka
kufanikiwa katika biashara. Zifuatazo ni kanun muhimu za ujasiriamali.
1. Kuthubutu
hii
ni tabia muhimu sana kwa mjasiriamali,hapa tunazungumzia uwezo na utayari wa
kufanya maamuzi ya kuingia katika biashara fulani au mradi fulani huku ukiwa
umeondoa nidhamu ya woga. Watu wengi ni waoga wa kuchukua hatua au kuthubutu
kuingia katika biashara,mradi n.k,watu wanaogopa hasara,hawajui jinsi ya
kuendesha mradi weyewe. Mtu ili aitwe mjasiliamali ni lazima awe na uwezo wa
kuhtubutu kufanya jambo, lakini jambo atakalo thubutu kufanya lazima afanye
utafiti wa kutosha il baadaye limletee tija. Waswahili mwanasema” UWOGA NI
UMASIKUNI”.
2. Nidhamu
Hii
pia ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali,mjasiriamali lazima awe na na
nidhamu katika biashara yake,awe na nidhamu katika matumizi yake ya pesa na ni
lazima awe na nidhamu ya kufanya kazi kwa bidii.nidhamu ni chanzo ch mafanikio.
Mfano mfanyabiashara wa duka ni lazima awe na nidhamu kwa wateja wake ili wasimkimbie.
3. Umakini
na uelevu
Wale
waliofanikiwa sio tu walikuwa tayari kufanya kazi bali waliweka umakini mkubwa
katika kazi waliyokuwa wakifanya. Mjasiriamali anatakiwa kuwa makini kwa kila
jambo,anatakiwa kujua soko linaendaje na pia ni lazima awe muelevu wa kutambua
mabadiliko yanayojitokeza katika soko ,uzalishaji na uendeshaji kwa ujumla.
4. Kuwa
na uwezo wa kuongoza
Mjasiriamalia
lazima awe na uwezo wa kuongoza na kutoa maamuzi. Baadhi ya watu wanadai
uongozi ni karama ombayo mtu anazaliwa nayo au anapewa na Mungu,ni
kweli mtu anaweza kuzaliwa na kipaji cha kuongoza,lakini mtu anaweza kujifunza
na akawa kiongozi mzuri. Katika ujasiriamali uongozi ni jambo muhimu
sana,mjasiliamli lazima aweze kuongoza biashara yake au mradi wake vizuri.
Mjasiriamali lazima awe na uwezo wa kusimamia wafanyakazi na kutumia
mbinu za uongozi ili apate matunda kwa kile ambacho anafanya.
5. Kupenda
kufanya kazi (kufanya kazi kwa bidii na maarifa)
Kitu
kikubwa hapa ni lazima mjasiriamli awe anaipenda kwa dhati shughuli
anayofanya hii itamsaidia kufanya kazi kwa moyo.Kama unapenda kazi unayo fanya
basi kazi hiyo haitakuwa mgumu,bali utakuwa unafanya kitu ambacho kwako ni hobi
na mwisho wa siku utafanya kazi kwa bidii na maarifa. Watu waliofanikiwa ni
wachapakazi.hivyo ni muhimu kuwa na tabia ya kufanya kazi kwa bidii.
6. Uaminifu
na ukweli
Hii
nayo ni tabia ambayo mjasiriamali anatakiwa kuwanayo,wateja wengi wanapenda mtu
mwamifu na mkweli. Kama mjasiriamali ni lazima ufanye kazi yako katika
mazingira ya uaminifu na ukweli ili upate wateja wengi,lazima uwe mkweli katika
bei zako. Uongo katika biashara ni sumu ambayo itaua biashara yako
mapema sana
7. Dhamira
Mtu
yeyote naweza kujiita mjasiriamali lakini kiukweli mafanikio yanahitaji uelewa
wa kutosha,kufanya kazi kwa bidii huku ukiwa umeweka mbele lengo au dhamira.
Lengo au dhamira ni motisha tosha itakaoyo kupa msukumo mpaka kufikia
mafanikio. Dhamira ya kweli inahijajika kabla hujaingia katika biashara au
mradi fulani.
8. Kwenda
na wakati
Mjasiriamali
lazima aende na wakati ili aweze kutambua mabadiliko mbalimbali yanayo jitokeza
katika masoko na uzalishaji wa bidhaa kwa ujumla. Kwenda na wakati hakutampa
nafasi mjasiriamaili kuachwa nyuma katika ushindani wa kibiashara katika soko
huria,kwenda na wakati pia kunatoa fursa kwa mjasiriamali kujua njia mpya za
uzalishaji. Njia ambazo zinaweza kukusaidia kwenda na wakati ni pamoja na
kusoma magazeti,kufanya utafiti,kurambaza katika mitandao mbalimbali.
Endelea
kutembelea mtandao wetu tuendelee kujifunza zaidi.
Imeandaliwa
na Jerome Mmassy-Arusha,Tanzania.
No comments:
Post a Comment