Thursday, 15 June 2017

JE?MTAJI NI TATIZO KWAKO? KARIBU TUELIMISHANE


MTAJI

Mtaji nini? 
Mtaji ni kitu au rasilimali ambayo mtu anaweza kuitumia ili kuanzishabiashara, rasilimali hii ndio ambayo itamfanya mtu yeyote aweze kuanzisha biashara na kuifanya biashara yake ikuwe hautaweza kuanzisha biashara kama hautakuwa na mtaji.
Aina za mitaji


1. Wazo 

Huu ndio mtaji wa kwanza ambao mtu anapaswa kuwa nao kabla ya mtaji wowote, watu wengi hukaa wakifikiri kuwa huwezi kuanzisha biashara hadi uwe na pesa lakini wamesahau kuwa wazo ndio kitu cha kwanza, je hebu jiulize unawazo gani la biashara au huduma? ukijigundua hunawazo lolote la biashara basi itakuwa ngumu sana kufanikiwa kwenye biashara hata kama utapewa pesa,mfano unakuta mtu anakwambia sina mtaji lakini ukimwambia nikikupa mtaji wa pesa utafanya biashara gani anakwambia biashara yoyote tu,huyu hata ukimpa,pesa lazima atafilisik.Hapa ndipo unakuta wapo wafanyabiashara wengi huwa wanaanzisha biashara na zinakufa kwa sababu anamuona mwenzie kafungua botiki na yeye anaenda kukopa pesa benki anafungua botiki kwa kuamini pesa pekee inatosha kumfanya kuwa mfanyabishara,kwa kuwa lile halikuwa wazo lake hivyo hata weza pambana na vikwazo mwisho wa siku anafilisika anaanza kwenda kwa waganga.Tafuta wazo lako rafiki unataka kufanya nini.Wangapi tumewaona wanastaafu wanapewa mamilioni ya pesa na wanakufa masikini kwani tatizo pesa? Hapana tatizo hawana wazo.tafuta wazo la biashara lifanyie utafiti kisha fuata mtaji wa pili.



2. Jitihada na maarifa 

Hapa ndipo kwenye tatizo ambalo weengi hawalijui kuwa ndio umasikini wao ulipo, watanzania wengi ni wavivu, hatuko tayari kujitoa,kujitahidi wala kujituma,tunasubiri kila kitu tufanyiwe,ngoja nikwambie rafiki hakuna ambaye atashughulika na ndoto zako wala mawazo yako.Ukisha kuwa na wazo sasa lazima uwe na jitihada, msaada hauwezi kukukuta nyumbani.Siku zote hata kama unataka kusafiri kwa mfano unatoka Arusha kwenda Babati halafu hauna nauli unadhani ukiendelea kukaa ndani na wazo lako la kwenda Tanga gari litakufuata ndani? hapana ukitaka kuanza safari hata kama huna nauli anza kutembea kwa miguu kidogokidogo ukiwa barabarani atatokea msamaria atakupa lifti na utafika lakini ukiendelea kukaa ndani hakuna ambae atajua kama unawazo ila safari.Hivyo hivyo kwenye biashara ukishakuwa na wazo zuri la biashara basi weka jitihada mtafute mtu ambae anapesa muonyeshe wazo lako sio hadi akukopeshe pesa waweza mwambia mfanye wote hiyo biashara faida mtakuwa mnagawana baada ya muda utapata pesa zako za kufanya kitu kikubwa.acha kulala mtanzania.Tatizo watu wengi wanapenda faida za haraka hakuna maisha rahisi lazima upambane.

3. Fedha 

Huu ndio mtaji wa mwisho kabisa baada ya kuwa na mitaji hiyo miwili.Ni rahisi sana kufanikiwa kwenye biashara kama ukiwa na wazo na jitihada hata kama hauna pesa kwa sababu utakapopata pesa na unawazo basi utatimiza wazo lako kwa uangalifu zaidi.ewe Msomaji wangu, acha kukalia utajiri wako kwa kusubiria mitaji mikubwa ya pesa tafuta wazo, weka jitihada kwenye mawazo yako pesa utapata.Na usisubiri kuanza biashara hadi uwe na mtaji mkubwa hili ndilo tatizo letu tulio wengi unasubiri hadi awe na mtaji mkubwa hapana ukisha kuwa na wazo lako la kuchoma chapati basi usisubiri hadi uanze na kilo kumi za unga anza hata na nusu kilo halafu hizo kilo zingine zitafuata ukisubiri hadi ziwe nyingi utakula na hizo ndogo.Zipo biashara ambazo unaweza anza bila hata kuwa na mtaji na ukajikuta unapata mtaji mkubwa sana kama kweli uko makini na biashara.

Usimamizi wa fedha ni muhimu sana kwenye biashara. Ili biashara iweze kudumu ni lazima iweze kutengeneza mapato makubwa kuliko matumizi na uzalishaji. Ni lazima iweze kuzalisha fedha za kutosha kuiendesha na ibaki faida. Ukosefu wa fedha unaotokana na mauzo kidogo na matumizi makubwa ndio chanzo cha kufa kwa biashara nyingi. Mambo muhimu unayopaswa kujua kuhusu fedha kwenye biashara yako.

Jambo la kwanza; Fedha ndio damu ya biashara. Kama ambavyo binadamu tunategemea mzunguko wa damu ili kuendelea kuwa hai, biashara inahitaji mzunguko wa fedha ili kuendelea kuwa hai. Bila ya mzunguko wa fedha hakuna biashara kwa sababu mzunguko wa fedha ndio unaleta fedha na bidhaa au huduma nyingine muhimu kwenye biashara yako.Elewa kitu kimoja muhimu hapa, kuwa na fedha nyingi pekee hakutoshi kuikuza biashara yako. Bali unahitaji kuwa na mzunguko wa fedha, mzunguko huo ndio unakuza biashara yako. Mzunguko wa fedha hata kama ni mdogo ni bora kuliko kutokuwepo kwa mzunguko kabisa.

Mara zote hakikisha una mzunguko mzuri wa fedha kwenye biashara yako. Pia dhibiti mzunguko huu ili kuhakikisha biashara inaendelea kuwa na afya.

Jambo la pili; Fedha ni zao la thamani.Watu wanakuja kununua kwenye biashara yako, siyo kwa sababu yako, bali kwa sababu zao binafsi. Kwa lugha nyingine, watu wanakuja kununua siyo kwa sababu wamekuona unauza, ila kwa sababu wana shida na matatizo ambayo wewe unaweza kuyatatua kupitia biashara yako.

Hivyo jambo muhimu sana unalopaswa kujua ni kwamba fedha ni zao la thamani. Unapata unachopata sasa kulingana na thamani unayotoa. Hii ina maana kwamba kama unataka kuongeza kipato kwenye biashara yako, basi anza na kuongeza thamani ambayo unatoa kwa wengine. Watu wanakulipa kulingana na thamani unayowapa kupitia biashara yako. Toa bidhaa na huduma bora, zinazotatua changamoto za watu na watakuwa tayari kukulipa vizuri.

Jambo la tatu; Fedha za biashara ni tofauti na fedha zako binafsi.Hapa ndipo wafanyabiashara wengi huwa wanachanganya na inawapelekea kushindwa kuona ukuaji wa biashara zao. Wao hufikiri kwa sababu biashara ni yao basi wanaweza kutumia fedha watakavyo. Kwa sababu biashara ni yako basi unaweza kujiamulia kuchukua fedha kwenye biashara na kupeleka kwenye matumizi yako binafsi, si kitu kile kile tu?

Hili ni kosa kubwa mno, fedha za biashara ni mali ya biashara, na fedha zako binafsi ni tofauti kabisa. jifunze kuitenganisha biashara na wewe binafsi, siyo kitu kimoja. Unapotoa fedha kwenye biashara kwa matumizi yako binafsi, maana yake unaidumaza biashara. Na kama utaendelea hivyo, utaiua kabisa kiashara.

Jambo la nne; Jua tofauti ya mauzo na faida.Wafanyabiashara wengi, hasa wachanga huwa hawaelewi vizuri tofauti ya mauzo na faida. Wafanyabiashara wengi huona mauzo makubwa na kufikiri ni dalili kwamba biashara ni nzuri. Ni kweli mauzo makubwa ni dalili nzuri, lakini siyo mara zote inatafsiri kwamba biashara iko vizuri. Kupata faida halisi kwenye biashara yako, chukua mauzo, toa manunuzi halafu toa gharama zako zote za uendeshaji wa biashara ikiwemo nauli, mawasiliano n.k. Hapa ndipo utaona kama biashara inajiendesha kwa faida au kwa hasara.

Jambo la tano; Wekeza sehemu ya faida kwenye biashara yako.

Jambo la mwisho msingi hapa ni uwekezaji kwenye biashara yako. Biashara nyingi huwa zinadumaa, yaani hazikui tena tangu kuanzishwa, na nyingine zinakufa kabisa kwa sababu wafanyabiashara wanajisahau kwenye uwekezaji kwenye biashara hiyo. Watu wanaanza biashara, na kila faida ya biashara wanayopata wanaitumia yote. Hawakumbuki kuwekeza sehemu ya faida hiyo kwenye biashara ili kuikuza zaidi. Kwa njia hii biashara inashindwa kabisa kukua.

NJIA BORA ZA KUPATA MTAJI WA KUANZA ZA BIASHARA

Moja ya changamoto ambazo watu wengi wanaotutafuta huwa ni wanawezaje kupata mtaji wa kuanza biashara. Hiki kimekuwa kikwazo kwa watu wengi kuingia kwenye biashara. Hata wale ambao tayari wapo kwenye biashara, wamekuwa wakitamani kukuza biashara zao ila wanashindwa kutokana na kukosa fedha za kuingiza kwenye biashara.

Tatizo kubwa ambalo linawazuia wengi kutopata mtaji wa biashara ni kwa sababu inapokuja swala la mtaji wanafikiria sehemu moja tu, ambayo ni mkopo. Na kwa bahati mbaya sana watu wengi wanakuwa hawana sifa zinazowawezesha kupata mkopo wa kibiashara kama vile ardhi, nyumba ya kuweka rehani n.k. Kwa kukosa sifa hizo huishia kukaa na kulalamika nataka kuingia kwenye biashara ila mtaji sina.



Kama wewe unapenda biashara, na umepanga kuingia au umeshaingia lakini hujaweza kukuza mtaji wako, hapa nakupa njia mbalimbali za kupata mkopo kwa ajili ya biashara yako,soma na fanyia kazi hizi.....................................Endelea kufuatilia blog hii itaendelea baadaye leo

JEROME NA ANNA

No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...