Somo hili ni mahsusi kwa wale wanaotaka kujifunza somo la ujasiriamali na wanaoanza kufanya ujasiriamali pia, pia ni somo zuri kwa wale wanaoanzisha,kusimamia na kuendesha biashara zao.......
Nini maana ya Ujasiriamali?
Neno Ujasiriamali lina asili ya Kifaransa”Entreprendre" sawa na Kutekeleza/Kufanya shughuli fulani mwenyewe katika uwanja wa kibiashara.Ni sawa na kuanzisha biashara/shughuli ya kujiajiri.
Nini maana ya mjasiriamali?
Mjasiriamali ni mtu ambaye ana hamasa kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika hali yake ya kiuchumi ambaye ana tabia za kipekee ili kufanikisha azma yake hiyo kwa kujishuhulisha (yaani kujiajiri) ili awe na hali nzuri zaidi kiuchumi.Pia katika hali nyingine Mjasiriamali anaweza kuwa mtu yoyote ambaye anajishughulisha mwenyewe (amejiajiri) katika sekta fulani mfano: kilimo, ufugaji au biashara.
Mchumi Joseph Schumpeter wa Ausralia ameielezea dhana ya ujasiriamali kwa kuegemea mihimili ya ugunduzi na ubunifu, katika nyanja hizi
-Bidhaa Mpya
-Njia Mpya za uzalishaji/uendeshaji.
-Masoko Mapya
-Mifumo mipya ya Vikundi na Mashirikisho
Na katika kueleza dhana yake hiyo anasema; Utajiri unapatikana pindi ugunduzi unapoenda sambamba na mahitaji, kwa mtazamo huu tunaweza kusema ya kwamba kazi ya Mjasiriamali ni sawa na kuunganisha mbegu za vigezo fulani katika hali ya Ugunduzi na Ubunifu ili kutengeneza ubora na thamani kwa mteja kwa imani ya kwamba thamani itakayopatikana itafidia gharama za mbegu hizo, na hatimaye kutengeneza faida ya kutosha inayopelekea utajiri.
Kwa hiyo, tunaweza kuona sasa Kwamba, ujasiriamali ni mtazamo katika akili ya mtu katika kutafuta fursa, kuwa tayari kukabiliana na matatizo na kuwa na uwezo wa kutengeneza faida, kwa kuanzisha ama biashara mpya au kuongeza tija katika taasisi fulani. Ujasiriamali hujumuisha shughuli nyingi ikiwa ni pamoja na kuwa na wazo, kutengeneza na kuendesha biashara au shughuli yoyote halali.
Kwamba mjasiriamali ni mtu anayefikiri kwa ubunifu na uvumbuzi akiwa tayari kukabiliana na hatari inayoweza kusababishwa na fursa zilizopo kwa lengo la kuzalisha faida, ajira na ustawi wa kijamii na kiuchumi. Ujasiriamali siyo lazima uhusishe kuanzisha biashara lakini pia kuleta tija au kubadili utamaduni wa shirika au taasisi.
Wajasiriamali huanzisha kampuni ambazo huwa kichocheo katika ukuaji wa uchumi na utengenezaji wa utajiri. Vitu kama kompyuta, simu za mkononi, mashine za kufulia, ATM, kadi za benki na huduma za usafirishaji ni mifano wa mawazo ya ujasiriamali yaliyobadilishwa kuwa bidhaa au huduma.
Historia ya Ujasiriamali
Historia ya Elimu ya Ujasiriamali ilianzia katika vyuo na vyuo vikuu huko Marekani ambapo kozi ya kwanza ya Masters of Public Administration (MBA) ilianzishwa mwaka1947 katika Shule Kuu ya Biashara ya Chuo kikuu cha Harvard chini ya kichwa cha habari “Uendeshaji wa Biashara Mpya” (Katz 2003). Kuanzia miaka ya 1980 na kuendelea, elimu ya ujasiriamali ilianza kuenea kwanza Ulaya Kaskazini, na baadaye kuenea katika sehemu za Ulaya ya Kati na Ulaya ya Kusini katika miaka ya 1990. Elimu ya ujasiriamali baadaye ilienea katika sehemu nyingine za dunia. Kimataifa, Amerika ya Kaskazini ndio mfano wa kuigwa katika ustawi wa miradi na pia Amerika ya Kaskazini ni kiongozi katika elimu ya ujasiriamali hadi sasa. Hakuna asiyejua mchango mkubwa wa kiuchumi wa Kampuni ya Microsoft, Amazon, Intel, Cisco, Lulu au Google na makampuni mengine yenye ushawishi mkubwa huko Marekani. Ukilinganisha na nchi zingine, Marekani ndio nchi yenye historia kubwa katika elimu ya ujasiriamali duniani, na pia ndio nchi yenye mpangilio, utamaduni na mazingira rafiki ya ujasiriamali kuliko nchi yoyote duniani (Kourilloff, 2000). Nchini Tanzania, elimu ya ujasiriamali haikuwepo enzi za ujamaa wakati wa Azimio la Arusha. Wakati huo Watanzania waliaminishwa kuchukia kila kitu kinachohusiana na ubepari, ukiwemo ujasiriamali. Mjasiriamali alichukuliwa ni kama msaliti na alilinganishwa na mnyama katili wa mwituni. Msemo “Ubepari ni Unyama” ulisikika kwenye radio kila baada ya taarifa ya habari, na vyombo va habari viliandika kila uchao. Ujasiriamali uliwavutia tu wale ambao walichukuliwa kuwa ni watu waliopotoka kimaadili.
Watumishi wa umma walizuiwa kujishughulisha na biashara (Rutihinda, 2002). Kwa kuwa karibu watumishi wote wa umma walikuwa ni Waafrika, hii ilimaanisha kuwa shughuli za kibiashara zilibaki kuwa za Watanzania wenye asili ya Asia pamoja na wale wazawa ambao walikuwa hawana ajira katika ofisi za umma. Watu wa aina hii walikuwa ni wale ambao hawakuwa na kiwango kikubwa cha elimu (Olomi, 2009).Labda wakati huo ilikuwa sawa kutokana na nyakati zile.Hata hivyo, maendeleo ya hivi karibuni katika ulimwengu, pamoja na sababu za ndani zimeilazimisha nchi yetu kuridhia mabadiliko. Baada ya kuanguka kwa ujamaa na Azimio la Arusha, nchi ilianza kubadilika kimfumo. Mamlaka zinazohusiana na masuala ya elimu zilianza kuiona elimu ya ujasiriamali kuwa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi katika miaka ya 2000 katikati. Walianza kuiweka elimu ya ujasiriamali kwenye mihtasari na baadhi ya shule na vyuo sasa vinafundisha katika masomo yao.
SIFA ZA MJASIRIAMALI
Wapo watu ambao mara nyingi hujiuliza ni biashara gani wafanye katika maisha yao ambayo itaweza kuwaingizia pesa nyingi ya kutosha. Ni wazo ambalo hutokea kutokana na pengine kuona kila biashara wanayoitazama kwa wakati huo kama hailipi. Hali hiyo husababisha mkanganyiko mkubwa wa mawazo ambao husababisha wabaki njia panda.
Mjasiriamali ni mtu gani?kama tulvyoona katika maana hapo mwanzoni, Huyu ni mtu ambae anaweza kutumia jamii inayomzunguka katika kuanzisha fursa mbalimbali za kibiashara ambazo zitampatia kipato,mtu huyu huweza kuitumia rasilimali watu ili kujinufaisha,watu wengi wanaamini kufungua duka ni kuwa mjasiriamali,La hasha! Unaweza kufungua duka lakini bado ulichokifungua na jamii inayokuzunguka hakina faida na ni idadi ndogo tu ya watu ndio watakubaliana nacho lakini pia umefungua duka lakini unasubiria wateja waje tu, huu sio ujasiriamali.
Baadhi ya sifa za mjasiramali:
1. Hupenda kujifunza
Hapa ndipo ugonjwa wa watu wengi ulipo mtu anajiita mjasiriamali lakini muulize kasoma vitabu vingapi vya ujasiriamali au kahudhuria semina ngapi za ujasiriamali watanzania wengi tunapenda sana vitu vya urahisi hatupendi kujifunza kama kweli unataka kuwa mjasiriamali au ni mjasiriamali lazima uwe na sifa hii upende kujifunza kutoka kwa watu wengine na uhudhurie semina au mafunzo mengi ya ujasiriamali.
2. Huwa mbunifu
Mjasiriamali yeyote ni mbunifu, ninapozungumzia ubunifu nina maana je unapata kitu tofauti kila siku ambacho jamii yako itapendezwa nacho au umeng'ang'ania aina moja siku zote? lazima kama mjasiriamali uwe mbunifu kila siku kuhakikisha unapata...................................
Ukitaka kukipata kitabu hiki nitafute 0624002807 kwani ni kitabu kilichojaa mbinu za kuanzisha za kuweza kufanikiwa katika ujasiriamali
No comments:
Post a Comment