Saturday, 5 March 2016

SUALA HILI MDAU ANALALAMIKA LICHUNGUZWE:

Naomba urejee taarifa kwenye vyombo vya habari, SIKU TANO ZILIZOPITA.


Waziri wako wa Kazi na Ajira, Jenista Mhagama alikutana na baraza la uwezeshaji wananchi wa Tanzania kiuchumi (NEEC) ambalo majukumu yake ni kuwawezesha wa Tanzania kiuchumi na kupunguza tatizo la ajira Tanzania. Na Akasisitiza na kutoa amri kuwa serikali ya awamu ya tano inapenda kuona kazi inafanyika kwa vitendo na matokeo yananufaisha wananchi na si vinginevyo.....




Hii vinginevyo aliyosema waziri Mhagama alikuwa akimaanisha kuwawezesha Raia/ Wananchi wa UGANDA (Jana alimteua Raia wa Uganda kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF).


Naamini kuwa Waziri Mhagama kafanya maamuzi hayo baada ya kupata ruhusa toka kwa katibu mkuu kiongozi Ikulu, Ombeni Sefue ambaye amekuwa akituhumiwa kuwa anakubambikia majina ya watu ambao hawakidhi viwango vyako kama Eric Shitindi na Jenista Mhagama.


Pia tusisahau kuwa Katibu mkuu wizara ya kazi na ajira, Eric Shitindi ndiye aliyempigia chapuo huyu Mganda kupata kazi SSRA.


Kutokana na unyeti wa nafasi hii ya mkurugenzi mkuu NSSF, naamini kuwa OMBENI SEFUE, ERIC SHITINDI & JENISTA MHAGAMA hawana nia njema na Kipenzi chetu, Rais John Pombe Magufuli,PHD.


Ombi kwa Mheshimiwa Rais, wawajibishe hawa watu na wengine wote waliohusika kukuhujumu, kuhujumu nchi hii.


Mheshimiwa Rais tunakuomba uombe ma faili ya hawa watu watatu niliowataja (ERIC SHITINDI, OMBENI SEFUE & JENISTA MHAGAMA)


Ikumbukwe kuwa ulipoanza awamu yako ulikuwa hujagusa maslahi yao lakini leo ulipoanza kugusa maslahi yao wameamua kwenda kinyume na misimamo yako ya kuweka watanzania mbele.


Na kukumbusha tuu Mheshimiwa Rais, huyu waziri JENISTA MHAGAMA ulibambikiwa na haendani na viwango vyako kwa maana teuzi zako zilikuwa zimejaa watu wasomi waliobobea. Iweje leo umeenda kumteua JENISTA MHAGAMA kusimamia Wizara nyeti hii amabayo anapanga sera, mambo mambo ya bunge, kazi na ajira wakati hata degree moja hana.




Mheshimiwa Rais, ukitaka Ushaidi katika hili tafadhali mheshimiwa Rais wasiliana Katibu wa Bunge Ndugu Kashilila akupe mafaili na vyeti vyake vya elimu.

No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...