Tuesday, 15 March 2016

Ni kweli Rais Magufuli kawapunguzia Ulinzi wastaafu Jakaya Kikwete na Mkapa? ninayo hii kutoka IKULU



Kwenye Gazeti la JamboLEO, toleo namba 2381 la tarehe 15 March 2016 limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho “Magufuli awapunguzia ulinzi marais wastaafu”

Taarifa yake kamili ipo katika ukurasa wa nne na inaeleza kuwa Rais Magufuli amewapunguzia ulinzi Marais wastaafu na imewataja marais hao kuwa ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete.

Ikulu inapenda kuwataarifu watanzania kuwa taarifa hizo sio za kweli na inalitaka gazeti hilo kukanusha habari hiyo mara moja, vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Taarifa iliyotolewa kupitia kwa kaimu mkurugenzi wa mawasiliano, IKULU Gerson Msigwa ni kwamba pia IKULU inasisitiza kwamba Watanzania wanatakiwa kufahamu kuwa utaratibu wa ulinzi wa Marais wastaafu haujabadilishwa


No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...