Friday, 16 December 2016

Wenye nyumba waagizwa kuwa na picha za wapangaji

Serikali imewataka wamiliki wa nyumba mkoani Dar es Salaam ambao nyumba zao zina wapangaji, kuhakikisha wanakuwa na picha za wapangaji wao wote ili kuwatambua na kupunguza uwezekano wa kuhifadhi wahalifu.


Agizo hilo limetolewa leo na Kamishna wa Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule mara baada ya kufanya oparesheni ya kufunga madanguro na kuwasaka raia wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha sheria.

Msumule pia amewaonya watu wanaowaajiri raia wa kigeni bila vibali, kuoa ama kuolewa na raia wa kigeni bila vibali kufika katika ofisi za uhamiaji na kufuata utaratibu wa kisheria wa wao kuishi nchini ili kuondokana na usumbufu utakaojitokeza pindi watakapo chukuliwa hatua za kisheria.

Pia amesema kuwa, tayari wamewakamata waajiri na waajiriwa wa kampuni ya Jantu Constraction Company ambayo imewaajiri raia wa kigeni bila ya kuwa na vibali vya kuishi nchini Tanzania.


No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...