Monday, 11 April 2016

MAGUFULI AMFUKUZA KAZI MKUU WA MKOA WA SHINYANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Anna kilango Malecela kuanzia leo.

Utenguzi huo umetokana na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo Anna kilango Malecela kutungaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hauna watumishi hewa jambo ambalo lilisababisha Ikulu kufanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili ya uchunguzi bado inaendelea.

Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akipokea hundi ya shilingi bilioni sita zilizotolewa na Ofisi ya Bunge baada ya kubana matumizi kwa ajili ya kununulia madawati Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kuagiza Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa kuondolewa ofisini mara moja.


No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...