Sikuwahi kuwa member wa hii forum
lakini nimeguswa na kuvutiwa kutokana
na mjadala ambao umemhusisha Mbunge
wangu MH HAMIS ANDREA KIGWANGALA
(SAIDI NASSOR BAGAILE) sikutaka
kujadili jambo lolote lakini
kilichonileta hapa kuchangia ni
mambo makubwa mawili ambayo
nitayataja hapa chini, leo
nimefahamu kwanini Mh Kigwangala
tulipokutana mara ya mwisho pale
MOVENPICK Ijumaa katika kujadili
baadhi ya mambo na umuhimu wa social
network nikamwambia nataka nijiunge
na wana bidii, alinishauri
NISIJIUNGE WANABIDII KWAKUWA NI
SEHEMU ISYOFAA WATU WANAPINGA KILA
KITU, nimefahamu sababu kumbe
hakutaka nifahamu kuwa mbunge wagu
yupo huku akipotosha taarifa nyingi
sana. Sikupenda kujibu hoja zake
imenibidi,hizi chini ni sababu kuu
zilizonisukuma kujibu.
(1) Mbunge wangu amenitaja kwa jina
katika baadhi ya mambo.
(2) Kuweka rikodi sawa sawa juu ya
baadhi maswala ya Msingi.
Hizo ni sababu kubwa zilizonifanya
niingie na kujibu baadhi ya
mambo,nimesoma hoja za Mbunge
ameongelea maeneo makuu yafuatayo,
(1) UHALALI WA JINA LAKE (2) URAIA
WA BASHE (MIMI BINAFSI) (3) AMESEMA
HAKUBEBWA ( 4) AMONGELEA USHINDI
WANGU (5) AMEONGELEA SWALA LA WAMA
( 6) AMEONGELEA KUWA ALIRUDISHA
UNITY KTK CHAMA (7) ASILI YAKE. Haya
ni maeneo makuu niliyoweza kuyaona
katika majibu yake alotoa hapa.
Nianze kwa kusema HAKUNA JAMBO BORA
DUNIANI KAMA KUFAHAMU MAPUNGUFU
YAKO, KUYAKUBALI NA KUKUBALI
KUYAFANYIA KAZI, PIA HAKUNA JAMBO
BORA KAMA KUMSHUKURU MUNGU KWA JAMBO
LOLOTE UNALOKUTANA NALO kama
nilivoshukuru mimi tar 2 august 2010
baada ya kuapata ushindi wa kura za
maoni, na kushukuru pia baada ya
kutoteuliwa na chama vyote
nilimshukuru mungu.
Nimesema haya maneno kutokana na
mbunge wangu kutokuwa mtu
wakushsukuru mungu kwa bahati
alopata ambayo imetokana na tabia na
mila za watu kumalizana kutokana na
kuwa na misimamo,mitazamo,fikra,na
maoni tofauti tofauti juu ya baadhi
ya mambo.SAIDI be a Gentleman kubali
ubunge wa jimbo la Nzega haukuwa
wako hukuwa na political Vission,
Mission, wala strategy ya kupata
ubunge ule,bcs of CCM politics Mimi
na Lucas selelii hatukuteuliwa and
you KNOW it.
NIANZE NA UHALALI WA JINA:
Usipotoshe watu jina la Hamis Andrea
si jina lako kijana mwenye jina hili
yupo Nzega unafahamu na baada ya
Wewe KUTEULIWA Chama na Wana CCM
kilikushauri uende mahakamani kuapa
kupata kiapo cha mahakama kubadili
jina na kulichukua rasmi jina la
Hamis Andrea na ulifanya hivo, jina
la hamis andrea umelichukua Rasmi
baada ya KUTEULIWA na kabla ya
kuchukwa Form na kuhisi utawekewa
Pingamizi, lakini deep in your heart
uanafahamu wewe na mimi tumesoma same
primary school na mimi na wewe
hatukufaulu DARASA LA SABA KITONGO
PRIMARY SCHOOL.
Baada ya hapo kutumia nafasi ya mama
yako ambae wakati huo alikua ni
mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nzega
ulienda mwanzoli ukachukua jina la
HAMIS ANDREA na kuanza kulitumia
kijana huyu alifaulu yeye na watoto
wa MZEE MTANGA WAKIKE AMBAO NI TWINS
kwakuwa hakuwa na taarifa mapema na
kwa kuwa kijana huyu baada ya
kumaliza pale mwanzoli alienda kuishi
KITANGILI baada ya mitihani taarifa
za ufaulu wake zilichelewa kumfikia
kijana huyu, ulichukua nafasi yake
na wewe kwenda KIGOMA SEKONDARI.
Ni kweli kama ulivosema kwamba wewe
nimjukuu wa mzee KIGWANGALLAH,huu ni
ukoo wa mama yako na si BABA yako,na
tulipokuwa tunasoma Primary ulikuwa
unaitwa Jina la SAIDI NASSORO
BAGAILE, nayo haya majina ( nassoro
bagaile) ni ya ukoo wa mama yako
tumekuwa wote hatumjui BABA YAKO na
hakuna mtu wa Nzega ambae anamfahamu
baba yako na siku zote imekuwa HIVYO
until utakapo prove otherwise
( tunaweza kuchanga fedha hapa
wanabidii watafute team ya watu
wakafanye uchunguzi walete ripoti
hapa tujue nani mkweli). Wanabidii
mkiangalia HOJA ya kuhalalisha na U
TANZANIA WA KIGWANGALA SIKU ZOTE
ATAELEZA KWA KIREFU HISTORIA YA
UPANDE WA MAMA YAKE UPANDE WA BABA
UTABAKI UNCLEAR HATA MAELEZO YAKE
HAPA YANAONYESHA HIVO,ingawa haikuwa
strategy yangu kum disqualify SAIDI
baada ya kuteuliwa katika uchaguzi
kwa HOJA YA UIRAI bcs mimi si
MUUMINI WA UKABURU HUO. USHINDI WANGU 2010
Mh Saidi/kigwangala amekuwa mara
nyingi akitaka kupotosha ukweli juu
ya ushindi wangu labda watu wengi
wajue historia ya mimi na wewe
katika siasa za JIMBO LA NZEGA,2005
wote tukiwa tumetoka mashuleni na
ajira zetu za mwanzo tuligombea
ubunge jimbo la nzega wewe ukitumia
Gari aina ya Mark 11 na mimi Suzuki
vitara ukiwa na mkeo mimi single
ukipita kuwaambia wananzega
wakuchague kwakuwa wewe ni msomi,
kijana na una mke.
Huku mimi nikipita na kuwaambia
wanichague kwa kuwa mimi ni kijana
wao wamenisomesha na sasa nina taka
kusimamia yale ambayo waliotangulia
walishindwa kuyafanya.
Wana CCM wajimbo la Nzega walinipa
kura 109 na wewe kura 24 chini ya
25% ndicho ulichopata ukifananisha
ushindi wangu na wako, wakati huo
kaka yetu LUCAS SELELII akipata
ushindi wakura zaidi ya 300.
Baada ya hapo wewe ulikimbia jimbo
hukushiriki jambo lolote wakati mimi
nikiendelea kutekeleza yake
niliyoahidi kwa wapiga kura kama
ninavyofanya sasa, 2007 ulifanyika
uchaguzi wa chama nikapa kura 1947
kati ya kura 1982 zilizopigwa na
mimi kuchaguliwa mjumbe wa mkutano
mkuu wa CCM TAIFA.
Then katika mktano mkuu wa mkao wa
Tabora nilipata kura 487 kati ya
kura 550 zilizopigwa na kuchaguliwa
Mjumbe wa Halmshauri kuu ya CCM mkoa
wa Tabora, chaguzi hiz wewe
hukishiriki nilishinda huku
nikipingwa na watu wote wenye Nguvu
katika MKOA namaanisha WOTE. Na hapa
nilizuia wizi wkura na GAZETI LA
MWANANCHI LILIANDIKA STORY CCM
WAONYESHA NAMNA YA KUIBA KURA.
2010 KATIKA UCHAGUZI
Katika uchaguzi huu nilishinda
kihalali katika vitua 152 wewe
uliongoza vituo 3,ambavyo nata
CENTRE ulinizidi kura 7,isanzu
centre,na shila,wakati kaka yetu
SELELII alishinda vituo Viwili
ambavyo ni SILIMUKA akinizidi kura
52,na ITILO akinizidi kura 17 kama
sikosei.
LAKINI VITUO HIVO SI KATA KIKATA
MIMI NILISHINDA KATA ZOTE 21, na
wewe unalifahamu hili tulikua na
Vituo 152 katika kata 21,vituo vyote
tuliweka mawakala wote sisi wagombea
wakuu 3 katika uchaguzi huo na
matokea yakawa Bashe 14,420,SELELII
2500 KIGWANGALA(SAIDI)1530 kama
sijakosea ukitazama kura hizo ni
sawa ni 11 to 12% ya kra nilizopata.
Wana Bidii hata leo tukirudia
Uchaguzi JIMBO LA NZEGA NITASHINDA
KWA KURA NYINGI SANA na ikiwezekana
tuakaandikishane tukafanye kampeni
nauhakika nitamshinda lakini UBUNGE
aendelee nao hili sina shaka juu
yake.
Utakumbuka wakati wa kura za maoni
niliwaahidi kuwashinda kwakuwa
nilikuwa nafahamu kuna njama hizi
nilikuambia wewe na wengine
,ninafahamu mpango wa kunikata jina
lakini nitahakikisha ninawashinda kwa
kura nyingi sana ili
hatamtakaponikata watanzania na
wananzega watapiga kelele kwa niaba
yangu na historia itakuwa imeandikwa
na hili lilitokea.
Wapo wanahabari waliokuwa wananieleza
juu ya mipango hii mliokuwa
mnaifanya na ilifahamika mapema ,but
I said to my self sijajiunga CCM kwa
ajili ya UBUNGE tu nitagombea
nitashindwa nitakatwa lakini nitabaki
ndani ya CCM kutimiza wajibu
wangu,na unafahamu hili kwa 2015 u
will face me again if god
wish,politically u have never been
threat to me jimbo la nzega
ninafahamu mtu pekee ambae ninaamini
ni threat kwangu ni LUCAS LUMAMBO
SELELII not you.
HOJA YA WAMA
Sipendi kuliongelea sana hili lakini
ni AJABU unapokana kuwa HUKUWAHI
KUFANYA KAZI NA WAMA ni kama mimi
nije katika PUBLIC nisema siajawahi
kuajiriwa na ROSTAM AZIZ ni kukana
ukweli ulio wazi binafsi sina
uhakika kama uteuzi wako una
mahusiano na kazi zako WAMA.
Bali nina uhakika umefanya kazi za
WAMA kama MUWEZESHAJI na MTOA
mafunzo yapo maeneo ambayo
uliwahikutoa TRAINING ambayo mimi
nafahamu,mfano KANDA YA ZIWA umewahi
kufanya maeneo kama shinynga ,BARAZA
KUU LA UVCCM ambalo mimi nilikuwepo
DODOMA 2008 feb uliletwa na WAMA why
useme UONGO jambo baya sana
najisikia AIBU MBUNGE WANGU ANAPO
DANGANYA.inawezekana mpaka leo
tunasubiri maandamano ya kufunga
mgodi hakuna umetudanganya naanza
kupata mashaka na wewe.
USHINDI WA JIMBO LA NZEGA
Be honest huweza kufanya mkutano wa
HADHARA hata mmoja mpaka ALIPOKUJA
MH RAIS na sote tuliahidi
kukusaidia,mimi ni mmoja wa watu
ambao waligombana na MARAFIKI zangu
kuja kukuombea KURA ni utamaduni
mwema mtu kushukuru unafahumu deep
inside in ur heart hukuwa na team ya
kampeni aliekuwa kampeni meneja wako
MR RWANGISA ndie aliekuwa kampeni
MENEJA WA KAKA YETU SELELII,leo
unasema HUKUBEBWA ULIBEBWA NA CCM na
wana nzega walichagua chama
kilichotuokoa NZEGA kama chama ni
UPINZANI kugawanyika CUF na CHADEMA
ur un popular katika JIMBO NA HILI
UNALIFAHAMU.
UNITY KATIKA CHAMA
SAIDI/KIGWANGALA wana ccm waliungana
kukisaidia chama chetu nah ii
haikuwa jitihada yako binafsi wala
jitihada ya mtu mwingine wewe si
ulieleta umoja katika chama bali
itikadi z wana ccm ndizo zilizo
waunganisha watu wa nzega na
ukiangalia katika historia yetu ya
jimbo this time ni mwaka ambao watu
walijitokeza kidogo kuliko
waliojiandikisha,hukupata hata kura
za wanachama wa ccm walipiga kura
wote,utakumbuka binafsi nilipita
maeneo yote ambayo wewe ulishindwa
kuyafikia ulienda maeneo hayo baada
ya mimi kuwa nimepita na kueleza why
wachague CCM na sikuwahi kutumia
JINA lako kuombea kura chama BCS
nilijua the only instrument ya
kuwafanya wana Nzega wakuchague ni
kutumia CCM.
HITIMISHO
Wana bidii mara nyingi MH mbunge
wangu amekuwa akitaka tuamini kwamba
yeye A kumbe ni B its good kusimama
kwa RANGI yako sikupanga kuyaongea
haya lakini imenilazimu kufanya hivo
baada ya kuwa mara zote nikiangalia
mkuu wangu akipotosha ukweli juu ya
mambo mengi.
Jambo la msingi kubali hukushinda
nzega ,hukuwa chaguo la wana
nzega,umefaidika na migogoro ya
kisiasa ndani ya mkoa na Taifa
hili,leo usilazimishe watu wakaanza
kufanya kazi kuangalia CREDIBILLITY
ya hata ELIMU YAKO NI QUESTIONABLE,
ukiangalia unaongela umesoma MASTERS
ya Bsness Administration, KAROLINSKA
institute a lot of questions with no
answer.
Tutaangalia credibility ya Degree
yako ya Muhimbili,tutaangalia
uhalali wa wewe kuchukua kiapo cha
kubadili jina siku tatu kabla ya
kujaza fomu,usilazimishe tujadili
ambayo si sawa kuyajadili wewe ni
kiongozi sasa acha siasa za
uongo,upotoshaji,simamia
unachokiamini na si wanachokiamini
wengine.
Tutahoji moral authority juu ya
mambo mengi unayoongea wakati wewe
ni mmoja wa walio benefit na
STIMULUS package 2009/10 ambazo
hazikuwafaidisha wakulima zaidi ya
kujinufaisha wewe binafsi kununua ma
Range mjini na kuja kugombea ubunge
Nzega kwa Fedha za walipa Kodi
kupitia kampuni ya MSK ambayo
wananchi wa Nzega hiuta jina la
Ambalo unalifahamu,,tutakuhoji
uadilifu wako wakati wewe ni mtu
alilazimisha wananchi wa nzega waache
kulima mazao ya chakula walime PAMBA
kujinufaisha wewe binafsi na biashara
yako na kushindwa kuwapa pembejeo
matokea yake PAMBA wakose na chakula
wakose.
Na sasa wanakabiliwa na njaa ukitumia
nafasi yako ya ubunge kuhamasisha
kilimo cha pamba na matokeo yake
kuwatia watu umasikini na sasa wana
nzega wanakabiliwa na njaa,
Umefika wakati wa wewe kusimamia
ahadi ulizotupa jimboni Tunasubiri
maandamano siku 21 zimeisha,na hapa
nilikushangaa lakini nikakubali
kujifunza kitu kipya Mgodi ule upo
pale kisheria,ni ilani ya chama
uliyoinadi,leo unaandaa maandamano
kuondoa?
Nikasema labda new approach ktk
siasa zetu,Umetuahuahidi mikopo kina
mama nzega umechukua viingilio vyetu
hujatoa mkopo mpaka leo ni either
urudishe 6000 ulizochukua ama uwape
mikopo,sio kupita na kuchinja
Ng”ombe na pilau vijijini ndio
maendeleo tuliotaka wana nzega.
Sikutaka kujakutoa maelezo marefu
hapa,kama nilivokushauri juzi wakati
tunachangia mfuko wa maendeleo wa
mkoa wa TABORA Yule kijana unajua
unatumia jina lake unajisikiaje
anabeba mizigo sokoni na
GANAGANA,msaidie mtafutie mtaji
akafanye biashara hata nje ya Nzega
kwa Mungu utaoneka umeshukuru,bila
ya Jina lake leo may be usingekuwa
hapo ulipo una RESPONSIBILITY YA
KIBINAADAMU KUMSAIDIA YULE BWANA
HAMIS.
Mwisho kuwa mkweli ukweli utakuweka
HURU
No comments:
Post a Comment