Wednesday, 2 March 2016

MANOWARI ZA IRAN ZIKO BANDARINI DSM,JE KUNA NINI?

Manowari ndogo kadhaa za jeshi la wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zilizobeba ujumbe wa amani na urafiki zimetia nanga katika bandari ya mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam.Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika hafla ya kuzilaki manowari hizo mjini Dar es Salaam leo, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Mehdi Agha Jaafari amesema, lengo la manowari hizo za jeshi la wanamaji la Iran ni kufikisha ujumbe wa amani na urafiki wa wananchi wa Iran kwa watu wa nchi za mashariki mwa Afrika hususan Tanzania.

Amesema kutembelea na kutia nanga manowari za jeshi la majini la Iran katika bandari ya Dar es Salaam ndani ya kipindi cha chini ya miaka miwili kunadhihirisha uhusiano mzuri uliopo baina ya Iran na Tanzania na hamu ya nchi mbili ya kustawisha ushirikiano baina yao katika nyanja za ulinzi.

Manowari ndogo za jeshi la majini la Iran ambazo zinatembelea Tanzania katika utaratibu wa safari ya mafunzo zitakuwepo katika bandari ya Dar es Salaam kwa muda wa siku nne.

Kwa mara ya mwisho, msafara wa manowari ndogo za jeshi la majini la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulilitia nanga katika bandari hiyo ya mji mkuu wa Tanzania mwezi Juni mwaka 2014...


No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...