Sunday, 13 March 2016

MAGUFULI LEO HII KARUDI TENA TAKUKURU NA TRA; SOMA HAPA ALICHOKIFANYA



Taarifa ambayo imetolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa mawasiliano, IKULU Gerson Msigwa imesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.

Waliothibitishwa ni Alphayo Kidata, aliyekuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambaye sasa ni anakuwa Kamishna Mkuu wa TRA naValentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).

Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13 Machi, 2016

No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...