Saturday, 12 March 2016

HUYU HAPA KATIBU MKUU WA CHADEMA

Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi hapa Jijini Mwanza.

Wananchi hapa wanasubiri ujio mkuu leo.Ujio wa Katibu mkuu wa Chama chenye ufuasi mkubwa nchini cha Chadema.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Freeman Mbowe ndiye atakayesimama leo mbele ya Baraza Kuu kutegua kitendawili kinachosubiriwa kuteguliwa na mamilioni ya wafuasi ndani na nje ya nchi.

Tayari majina kadhaa yasiyopungua kumi yamekuwa yakibashiriwa kwamba moja kati ya hilo ndilo litakalopita katikati ya moshi mweupe pale kwenye ukumbi wa Gold Crest.

Hekima na busara nyingi za Freeman Mbowe zimesababisha mpaka leo jina hilo kuwa siri kuu.Hata hivyo uchunguzi wa kuaminika kutoka kwa watu wa karibu na washauri wakuu wa Freeman Mbowe unasema Katibu mkuu mpya atakuwa ni mpenda chama na wananchi,kiongozi asiyeyumbishwa,mtetezi wa Katiba ya chama na jasiri asiyeyumbishwa atakayekuwa na uwezo wa kutamka jambo na nchi inasimama.

Waandishi wa habari wa ndani na nje ya nchi wamefurika kwenye viunga vya ukumbi huu kujiandaa kuwa wa mwanzo kurusha jina la Katibu mkuu mara litakapotangazwa.

Mtandao huu wa JESAM utakuletea jina hilo mata tu litakapotajwa 

No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...