Sunday, 28 February 2016

WALIMU WOTE SHULE ZA SERIKALI DAR WATASAFIRI BURE KABISA

Walimu wa shule za msingi na sekondari za umma mkoani Dar es Salaam wataanza kusafiri bure kwenye daladala kuanzia tarehe 7 Machi 2016.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paulo Makonda na viongozi wa vyama vya usafirishaji abiria jijini Dar wamezungumza na wanahabari na kuwathbitishia hilo.
Walimu  wote wa shule za serikali watatengenezewa vitambulisho maalum ili kuwaondolea usumbufu.
Huduma hiyo ni katika kuwapunguzia adha ya usafiri na ugumu wa maisha ikiwa ni pamoja na kuunga mkono juhudi za serikali za kutoa elimu bure.
Muda wa kuwasafirisha bure ni saa 11.30 hadi 2 asubuhi na saa 9 hadi 11 jioni.



No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...