Kijana asiye na kazi aitwaye Nolesy aliamua
kumwoa rafiki yake wa
muda mrefu
aliyekuwa
akifanya kazi katika
benki moja mashuhuri.
Nolesy alijitosa
katika ndoa licha ya hofu na
ushauri mwingi
aliopewa na ndugu kuwa ni
vibaya kuoa ukiwa
huna kazi.
Kila mwezi yule binti
alimpa mmewe
mshahara
wake wote wa 800,000
baada ya kutoa fungu
la
kumi kwa ajili ya
kanisani.
Nolesy yeye alitoa
200,000 na kumpa mkewe
kwa ajili ya matumizi
binafsi na zilizobaki
kijana aliamua atumie
kwa matumizi gani. Na
hali hiyo ilidumu kwa
miaka mitatu
mfululizo.
Furaha na amani
viliitawala nyumba ile na
kwa
wanandoa wale pia kwa
miaka mitatu pamoja
na kuwa marafiki
wengi wa yule dada
walimfuata na
kumwambia huwezi ukawa
unalipa bill zote za
nyumba na kufanya kazi
zote wewe tuu na mmeo
kakaa tuu kwa nini
msiachane?
Kuna mwezi mmoja
kijana yule alitumia zaidi
ya 500,000 akizunguka
mikoa mbalimbali kwa
ajili ya intavyuu za
kazi.
Hatimaye kijana
alifanikiwa kupata kazi
Mbeya
katika kampuni ya
Green Entertainments na
kuwa meneja mkuu huku
akipokea mshahara
wa milioni tatu na
nusu kama kianzio.
Akanunua gari yake ya
kwanza mpyaa kwa bei
ya shilingi 18M na
akampa funguo mkewe na
kuendelea kutumia
usafiri wa daladala kwa
zaidi ya miaka
miwili.
Baada ya hapo
akanunua gari la pili jipya
lenye
thamani ya 30M na
kumpa mkewe na
kulichukua gari la
zamani na kulitumia yeye
na
mpya kumpa
mkewe.Miaka michache baadae
wakahamia kwenye
nyumba yao.
Siku moja mke alikuwa
akitafuta dokyumenti
zake katika
makabrasha mbalimbali pale
chumbani kwao,
alishangazwa kuona kuna
bahasha ndogo
imefichwa na ndani kuna
picha
yake wakati wa harusi
na akaona kuna
dokyumenti nyingine
za manunuzi kiwanja na
magari na vyote
vikiwa vimeandikwa kwa jina
lake kabla ya kuona
maandishi yaliyoandikwa:
''MKE WANGU NI KILA
KITU KWANGU.
ALIKUBALI KUOLEWA NA
MIMI NIKIWA SINA
KITU, NA SASA NAAMINI
HATA NIKIWA NA
VITU VYOTE NI VYAKE
KWANI MOYO WAKE NI
ZAIDI YA KILA KITU
KWANGU NA FAMILIA
YETU.AISHI
MILELE"
Machozi yalimtoka
dada yule na alifurahia
sana
ujumbe ule kabla ya
kukumbuka kuwa wiki
chache baadae ilikuwa
ni kumbukumbu ya
miaka yao ya ndoa.
Hivi sasa MUNGU
amewabariki na wana
watoto
wawili wakike na
wakiume na wanapendana
mara mia zaidi ya
mwanzo.
Jamani mapenzi ya
kweli yapo mpaka sasa.
Je una uhakika kuwa
mapenzi uliyonayo kwa
mwenza wako ni sawa
au yanaweza
kulinganishwa na
haya?
Pamoja na vyote
lakini kumbuka
mnachaguana
ili kuishi kwa shida
na raha na haijalishi nani
ananunua mahitaji ya
nyumbani au kulipa bili
kwa sasa.........
HAKUNA HALI
INAYODUMU MILELE

No comments:
Post a Comment