Friday, 26 February 2016

CHUO CHA MT.JOSEPH ARUSHA CHAFUNGWA RASMI,SABABU NI HIZI HAPA CHINI

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kukifutia kibali Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania (SJUIT), kampasi ya Arusha na kuwahamisha wanafunzi wote waliokuwa wanasoma katika kampasi hiyo kwa gharama za Chuo hicho.
Akieleza sababu za kufutwa kwa Chuo hicho,  Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini Prof. Yunus Mgaya amesema ‘Kwa muda mrefu na kwa wakati tofauti kumekuwapo na matukio ya migogoro baina ya uongozi wa Chuo na Wanafunzi, Kwa kipindi hicho chote tumekuwa tukifuatilia kwa ukaribu chimbuko la migogoro hiyo na kuchukua hatua stahiki
Kwa sehemu kubwa migogoro hiyo imekuwa ikitokana na matatizo ya ubora, Uongozi, ukiukwaji wa sheria na taratibu za uendeshaji wa Chuo hicho, Kutokana na hali hiyo, tunapenda kuuarifu Umma kwamba Tume imefuta kibali kilichoanzisha Kampasi ya Arusha ya Chuo Kikuu cha Mt. Yosefu Tanzania  (SJUIT)

No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...