VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam,mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa tena mwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda UKAWA.Simulizi hii inasimuliwa na KAROLI VINSENT endelea nayo
Tukio hilo la aina yake limetokea mda huu Jijini Hapa mara baada ya mkurugenzi wa Jiji kutanga kuhairisha uchaguzi huo kwa madai ya uchaguzi huo kuwekewa pingamizi mahakamani , huku jambo hilo lilowachukiza madiwani wa UKAWA wakidai kuwa hawajapata barua hiyo ya kesi hiyo.
Mara baada ya UKAWA kugomea hoja hiyo ndipo wakafikia hatua ya ya kutaka kufanya uchaguzi wenyewe huku wakisema akidi ya madiwani kufanya uchaguzi imetimia na wakaomba waendelee kufanya uchaguzi huo,
Wakati wakijiiandaa kufanya uchaguzi huo ukawa wenyewe ,ndipo Polisi zaidi ya 15 wakavamiaka ukumbi huo na kuwataka kuwakamata madiwani wa ukawa ili waondoke ukumbini kuzuia uchaguzi usifanyike,jambo lilowachukiza tena ndipo Polisi wakaanza kupambana na madiwani wa Ukawa
ENDELEA KUFUATILIA JESAM BLOG UTAPATA HABARI KAMILI
No comments:
Post a Comment