Rais, Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki wa Acacia Mining Limited, Prof. John L. Thornton na kukubaliana kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania ili kulipa fedha zilizopotea.
Prof. John L. Thornton aliyesafiri kwa ndege binafsi akitokea Canada, amekutana na Rais Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam katika mazungumzo yaliyohudhuriwa na Balozi wa Canada nchini Ian Myles na Waziri wa Sheria na Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi.
Baada ya mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.
No comments:
Post a Comment