Monday, 7 March 2016

MBOWE:HATUTAOMBA KUMPATA MEYA WA JIJI LA DAR, TUTADAI KUMPATA MEYA






Hadi time hii headline za Uchaguzi wa Meya Dar es salaam zinazidi kutawala kila siku, ni siku mojatu baada ya Baadhi ya Wabunge na Madiwani wa Ukawa kufikakatika ofisi ya Halmashauri ya jiji kutaka kujua tarehe ipi uchaguzi utafanyika lakini hawakupata majibu hayo. Leo March 5 2016 Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe alikutana na waandishi wa habari na kueleza…

’Hatutaomba tena kumpata Meya wa jiji la Dar es salaam, tutadai kumpata Meya, Serikali wasifikiri watapanga wao tarehe ya kumchagua Meya, wamekuwa na utaratibu wa kutaka tarehe ya kumchagua Meya kwa kutushtukizia masaa 24 kabla‘

‘kanuni inadai siku saba, tutataka tarehe ya kuchagua na siku hiyo atachaguliwa Meya asipochaguliwa Meya siku hiyo tusilaumiane, hatuwezi kususia uchaguzi wa Meya kwa sababu ni haki yetu kuongoza jiji’.

No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...