Monday, 29 February 2016

MAGUFULI ALETA TAHARUKI ARUSHA


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais John Magufuli amewasili Jijini Arusha tayari kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama. Akiwa uwanjani amepokelewa na Mbunge Arumeru Mashariki ndugu Joshua Samwel Nassari wakiwemo viongozi wengine wa chama na serikali.Ujio wa Magufuli jijini hapa umeleta taharuki miongoni mwa watumishi wa umma katika ofisi kadhaa kiasi cha kufanya wakuu wa taasisi mbalimbali kuishi kwa hofu kutokana na utendaji kazi wa Rais Magufuli ambaye mara kadhaa amekuwa akifanya ziara za kushtukiza na kuwasimamisha watendaji kadhaa wa ofizi za umma nchini. Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa, pamoja na kwamba mkutano utaanza siku mbili zijazo, kilichomfanya Rais awahi zaidi Arusha ni kutaka kufuatilia utekelezaji wa shughuli kadhaa za serikali ikiwemo kupat taarifa mbalimbali za kiutendaji kutoks vigogo wa serikalini.Moja ya maeneo ambayo kuna presha kubwa kwamba muda wowote Rais anaweza kufanya ziara ya ghafla ni Hospitali ya Mount Meru iliyoko mita chache kutoka Ikulu ndogo iliko.Pia uongozi wa kiwada cha General tyre nako hali si shwari kutokana na kiwanda hicho kutozalisha kwa miaka kadhaa huko kikiwa na wafanyakazi wanaolipwa kwa fedha za watanzania.......Endelea kufuatilia Blog hii tutaendelea kukujuza muda wowote Rais awapo hapa jijini Arusha.



FOR GOD AND MY COUNTRY

No comments:

Post a Comment

Featured post

MWANAMKE YAFUATE HAYA; NI MUHIMU KWA MAHUSIANO YAKO

1. Degree yako ya fist class uliyoipata chuo kikuu haiwezi kukufanya uwe mke first class katika ndoa yako bali ni heshima yako na uthubu...